Kampuni za Insurance/ Bima

Kampuni za Insurance/ Bima

jumbenylon

Senior Member
Joined
Jun 12, 2011
Posts
115
Reaction score
10
Habari za leo wadau. Naombeni kufahamishwa. Je ni kampuni gani nzuri na ya uhakika kwa huduma za bima ya nyumba/ mali. Nahitaji kuweka bima kwenye asset za familia. Asante
 
Ebana hapo me naomba usipate tabu sana nina mengi yakukuambia au kukujulisha kuhusu ilo ila nenda NIC shirika la bima la taifa ao awanaga longolongo kaka.me nimtumiaji wa magari sana na nishapata sana maaajali na nishalipwa sana na ao majamaa na uwaga aizid hata miez miwili kila kitu uwaga kinakuwa poa nakushauli uende pale makao makuu wakakupe maelezo ya kina kwa mahitaji mengine ila me kwenye magari sijawahi kupata shida
 
kwa kuwa umesema umeshawahi pata ajali mara nyingi, naomba unipe uzoefu, kwa bima kubwa ukipata ajali unatakiwa kuambatanisha nyaraka gani kwenye madai yako.
kama hutajali tuwekee mlolongo wake tujue.
asente.
 
Bumaco insurance ltd ni kampuni ya uhakika inayomilikiwa na wazawa.
 
Kaka ukipata ajali unatakiwa kupima eneo la ajali na ionekene kweli ni ajali ambayo gari ndilo lenye shida na sio wewe pia veko atachora mchoro kuonesha jins ajali ilivyo pia kuna nyaraka utapewa na veko kutoka mahakaman na utalipia 500 yaani risit kutoka kituo cha polisi utaambatanisha kopi ya kadi ya gari,kopi ya leseni,kopi ya bima alafu unapeleka bima kwa kwenda kutasmin jins ya kukulipa
 
Kampuni zote za bima zinatakiwa kumlipa kila mteja anayekuwa amepata ajali kwa wakati muafaka baada ya kusubmit document zote zinazotakiwa na hiyo ni Sheria ndio inasema hivyo.

Tatizo watu wengi hawako aware na sheria za Bima ndio maana malipo hucheleweshwa na kutolipwa kabisa, kwa sababu ya kutokamilisha documents.

Nenda Kampuni yoyote iliyosajiliwa Insure mali zako na wakati wa malipo peleka nyaraka zote zinazohitajika na utalipwa. Ukizungushwa nenda Mamlaka ya Bima TIRA peleka malalamiko yako na utalipwa.
 
kama binamu charminglady alivyosema hapo juu wewe nenda kampuni yoyote ya bima utalipwa vilevile utakavyo na usiwe na longolongo lolote ile
 
Habari za leo wadau. Naombeni kufahamishwa. Je ni kampuni gani nzuri na ya uhakika kwa huduma za bima ya nyumba/ mali. Nahitaji kuweka bima kwenye asset za familia. Asante

Ni vigumu kupata jibu sahihi maana wengi wetu tunafanya biashara na mawakala wa bima na siyo kampuni za bima. Anaweza kukupa ushauri wa uhakika ni "Insurance Brokers" maana hawa wanafanya kazi na kampuni zaidi ya moja, hawa wanafahamu ni kampuni ipi ukipata shada itakufidia haraka.
 
kama binamu charminglady alivyosema hapo juu wewe nenda kampuni yoyote ya bima utalipwa vilevile utakavyo na usiwe na longolongo lolote ile
ladyfurahia wateja hawafanyi biashara na kampuni za bima, tunaunganishwa na kampuni za bima kupitia mawakala; Jibu lako si sahihi sana maana katika kulipa madai, kampuni za bima hutofautiana, kuna ambazo zinalipa haraka na nyingine ni mpaka wakala afuatilie sana
 
Last edited by a moderator:
oky kwa ufafanuizi una lingine ?

ladyfurahia wateja hawafanyi biashara na kampuni za bima, tunaunganishwa na kampuni za bima kupitia mawakala; Jibu lako si sahihi sana maana katika kulipa madai, kampuni za bima hutofautiana, kuna ambazo zinalipa haraka na nyingine ni mpaka wakala afuatilie sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom