Kampuni za Alpha hazilipi kodi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kampuni za Alpha hazilipi kodi!

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by mudavadi, Apr 22, 2011.

 1. m

  mudavadi Member

  #1
  Apr 22, 2011
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna taarifa kutoka katika chanzo cha uhakika kwamba kampuni la Alpha ambazo zinamilikiwa na familia ya Edward Lowassa ambazo zinatengeneza mabilioni ya shilingi katika mitandao yake ya kibiashara, zimekuwa zikikwepa kodi mbalimbali ambazo zinatakiwa kulipwa na wafanyabiashara wote, kama vile kodi ya mapato, import duties kwa bidhaa wanazoagiza pamoja na kufanya mawasilisho ya VAT wanayokusanya kutoka kwa wateja wao.

  Taarifa zinasema kwamba mchezo huu mchafu ambao hauzingatii hata sheria na mamlaka zinazotakiwa kutoa misamaha hiyo, zinafanyika kwa ushirikiano na vigogo wa TRA ambao wako kwenye pay roll ya wamiliki wa kampuni hizo. Kutokana na ukubwa wa biashara za Alpha na ukubwa wa mapato yao, mapato wanayokwepa yanakadiriwa kuwa ni kwenye mabilioni ya shilingi kila mwezi na yangeweza kuinua pakubwa katika pato la taifa na kwa kufanya hivyo, nchi hii inazidi kudidimizwa na wale wale ambao leo wanataka kupewa dhamana za uongozi katika taifa hili.

  Wakati suala hili linaweza kuonekana ni la kawaida hapa nchini kwetu kutokana na kukosekana kwa nia thabiti ya kudhibiti vitendo vya kudhibiti mapato na rasilimali za taifa, katika nchi zilizoendelea kama Marekani mmiliki wa biashara hizi asingethubutu hata kuomba ujumbe wa nyumba kumi akakubaliwa. Huu ni wakati wa watanzania kuamka na kuelewa kwamba tunaposema kwamba Lowassa si mtu safi na aisyestahili kupewa heshima anayopewa na baadhi ya wapambe ambao wameleweshwa na fedha haramu! Umefika pia wakati wa kuifagia TRA maana madudu yao yanazidi kuwawamba watanzania katika msalaba mkali sana wa maisha!
   
 2. n

  ndutu Member

  #2
  Apr 22, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi jamani nchi hii itakamuliwa mpaka lini? Hakika familia hii ni ya kunyongwa (kama ingekuwa nchini China). Halafu watu wasio na akili timamu wanatuambia kwamba huyu ni mtu anayestahili hata kusogelea madaraka ya dola! Ni wizi kila mahali utadhani hatakufa!
   
 3. Freema Agyeman

  Freema Agyeman JF-Expert Member

  #3
  Apr 22, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,284
  Likes Received: 1,432
  Trophy Points: 280
  Weka ushahidi mwana ili TRA wapate go ahead ya ku...
   
 4. T

  Tiote Senior Member

  #4
  Apr 22, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 139
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna mtu anaitwa CAG pamoja na Kamati za Bunge ambazo zinajifanya kucharukia baadhi ya taasisi na huku wakiacha mianya mikubwa kama hii. Mimi naona hawa jamaa kuvuliwa gamba hakutoshi maana kimsingi unawapumzisha wakale mabilioni yao kwa usalama. Huyu jamaa na familia yake wanatakiwa kuhakishiwa safari yake ya Keko au Ukonga maana hata huyo Liyumba dhambi yake haifiki hata moja ya kumi ya dhambi za huyu jamaa na washirika na familia yake. Eeh Mungu mpe ujasiri Rais wetu awatie adabu hawa jamaa!
   
 5. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #5
  Apr 22, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  Huyu jamaa kazidi kuiibia wananchi.Ni wakati muafaka sasa ashtakiwe na tumsahau kwani wizi na hujuma anazofanya ni za wazi kabisa
   
 6. b

  banyimwa Senior Member

  #6
  Apr 22, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kwa jinsi hii ishu ilivyokaa ushahidi hapa unatakiwa utoke kwao Alpha na TRA kwa kutoa receipt na vielelezo vitakavyokanusha na kuuthibitishia umma kwamba tuhuma hizi ni uzushi. Washushe ili tujue kwamba jamaa karopoka, lakini kama ni kweli basi kweli nchi hii ni shamba la bibi.
   
 7. b

  banyimwa Senior Member

  #7
  Apr 22, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hapa tunataka TRA na hao Alpha waje watuambie tena kwa ushahidi na vielelezo kwamba hawa jamaa wamekuwa wakilipa kodi. Lakini tunajua hilo halitawezekana maana minon'gono hiyo imekuwa ikisika, na ndicho kinachodaiwa kuwa sababu ya Kitilya kuendelea kuula pale hata kama uwezo wake na uadilifu wake ni matatizo makubwa.
   
 8. Mzalendo

  Mzalendo Senior Member

  #8
  Apr 22, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 180
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kaka yatamkuta tu kuliko ya gwm na maharage kuwa futari badala ya mboga toba!!!
   
 9. Freema Agyeman

  Freema Agyeman JF-Expert Member

  #9
  Apr 22, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,284
  Likes Received: 1,432
  Trophy Points: 280
  Nani ana mamlaka zaidi kati ya Kitilya na body ya wakurugenzi? la zaidi, nini kazi ya body ya wakurugenzi (najua ina prominent professionals).
   
 10. w

  watenda Member

  #10
  Apr 22, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 73
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Natamani ningepata bunduki na risasi kama kumi tu, niwaondolee udhia watanzania!
   
 11. i

  imara Member

  #11
  Apr 22, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  magereza pamejaa?
   
 12. w

  watenda Member

  #12
  Apr 22, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 73
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Board ni chombo cha kutunga sera na yaliyobaki yako chini ya Menejimenti ya Kitilya na kama hakuna chochote kilichoifikia Board ni vigumu kwao kujua na kutolea maagizo au maazimio. Prominent professionals nao huwekwa sawa mkuu!
   
 13. 2

  2 heads up Member

  #13
  Apr 22, 2011
  Joined: Jun 5, 2010
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mmh! Lao lingine!
   
 14. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #14
  Apr 22, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  Ndugu zangu wanajf,kila unapopita nchi hii utasikia malalamiko waliyonayo wananchi juu ya lowassa.Hivi ni kweli atakuwa anasingiziwa? akizidi kuendekezwa ataiba hadi geti la ikulu.
   
 15. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #15
  Apr 22, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Hivi vita vya wenyewe kwa wenyewe ndani ya ccm zinamwaga maovu mengi sana ya vigogo wao.

  Wananchi kazi kwetu.
   
 16. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #16
  Apr 22, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Halafu wanaibuka mabwege wanaojiita GT ua NSSF Damu ambao kazi yao ni kuimba mapambio ya kuwasifu kwa udhalimu na unyama wao kwa wa-tz, na kuendesha harakati za kuwatakasa. Lakini ukweli unabaki kwamba huyu jamaa ni kama nguo chakavu, kila unaposhona hapa panaachia pale. Lakini pamoja na kwamba Rais wetu JK ameshiba dini na kujaaliwa uvumilivu wa hali ya juu, iko siku ataamka na kuwatia adabu kama ambavyo amekwishaanza na ule moto wa CC. Tunasubiri majeshi ya kukodiwa, wakiwemo wanasiasa machachari na wenye heshima wa upinzani watujie na porojo za kuhamisha mada na kuwatakasa!
   
 17. s

  sokoine. Member

  #17
  Apr 22, 2011
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Vizuri havidumu...namkumbuka Hayati Sokoine.
   
 18. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #18
  Apr 22, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  Hivi ni vita kati ya wema na uovu. Umefika wakati wa sasa kuwaeleza watanzania kwamba si kila king'aacho ni dhahabu. Hata kama wahenga walisema mchawi mpe mwana akulelelee lakini mchawi huyu atamnyonga mwana mchana kweupee! Mimi nasema huyu bwana akichekewa tutavuna mabua.
   
 19. Chechetuka

  Chechetuka JF-Expert Member

  #19
  Apr 22, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 549
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Malalamiko haya yalikuwapo siku nyingi, wafanyakazi wa TRA wamekuwa wakimlaumu sana Kamishna Mkuu wa TRA kwa kusaidia na kuwakinga wafanya biashara wanaokwepa kodi. Hili siwezi kushangaa kwani mara nyingi sana mtoto wa "kambare mamba" huyo amekuwa akionekana na Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo muhimu yenye jukumu la kukusanya mapato ya watanzania.
   
 20. laigwanani

  laigwanani Member

  #20
  Apr 22, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sisi Masai yote napenda ng'ombe na ndito basi,nashangaa hii inapenda mbesa mpaka nywele anabadilika rangi.
   
Loading...