Kampuni ya Vodacom yaunga mkono serikali ya viwanda

Sudysoko

JF-Expert Member
Aug 19, 2015
449
180
Katika kuhakikisha uchumi Wa Tanzania unastawi kampuni ya Vodacom Tanzania imeamua kuunga mkono jitihada za kustawisha uchumi katika ukuaji imara katika sekta ya viwanda kwa kuhakikisha huduma na mawasiliano ya simu inatolewa kwa ubora pamoja na kuwepo kwa Sera muhimu kwa ajili ya kuendesha shughuli za kiuchumi na ajira.

Kupitia Vodacom Tanzania kampuni ambayo inaongoza kwa kuleta maendeleo ya kiuchumi Tanzania kupitia huduma zake za mawasiliano na huduma za kifedha kupitia M-Pesa imewezesha watanzania kufanya miamala ya thamani ya zaidi ya shilingi 100 bilioni kila siku wastani wa bilioni 2.6 kila Mwezi.

Kupitia miamala inayofanyika kampuni ya Vodacom Tanzania imeweza kuchangia pato la taifa kwa kupitia kodi ya ongezeko la thamani katika huduma za Miamamla ya kifedha pamoja huduma za mawasiliano Tanzania.
Mtandao wa Vodacom umeendelea kukua kutokana ukuaji halisi wa pato la Taifa kwa wastani wa asilimia 7 kwa mwaka.

Takwimu zinaonyesha Hali ya uchumi kati ya mwaka 2003 na 2015 imefikiwa asilimia 7.9 kwa misingi ya mwaka kwa mwaka katika robo ya pili ya Mwaka 2016.
Kwasasa kampuni ya vodacom imejitanua kwenye soko la mitaji ya hisa kwa kuziweka hisa zake sokoni kuwapa nafasi Watanzania kuwekeza na Vodacom, hali hii itasaidia sana kwa kuimarisha uchumi wa nchi kuwa wenye tija na kuleta matumaini katika kusaidiana na serikali kusukuma mbele gurudumu la Maendeleo.

Anza sasa nunua hisa za kampuni ya Vodacom Tanzania ili kujenga maisha ya mafanikio na kutimiza ndoto zako kwa wakati sahihi.
Wekeza Na Vodacom
Kazi Ni Kwako.
mwijage.JPG

mwijage2.JPG
 
Rekkebisha takwimu tafadhali muamala Wa bilioni 100 kwa siku ilete muamala Wa 2.6 bilioni mbili kwa mwezi .nadhani ni 2.6 trilioni za Tanzania .AU ni muamala ya Milioni 100 kwa siku italeta muamala ya 2.6 bilioni shilingi ki ?
 
Back
Top Bottom