Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,322
- 33,126
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, Diana Chilolo
Serikali inatarajia kufungua mgodi wa uranium wa Mkuju River (Mbamba Bay), katika wilaya ya Namtumbo, mkoani
Ruvuma kwa kuingia mkataba na kampuni ya Urusi ya ARMZ Uranium Holding.
Akipokea taarifa hiyo kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na
Madini, Diana Chilolo, alisema mradi huo unatajia kuunufaisha taifa, kupitia Sheria ya madini ya 2010 na utakuwa mradi mkubwa wa kwanza wa madini nchini.
Alisema katika mkataba baina ya Serikali na kampuni hiyo, hakutakuwepo na migogoro ya kutokana na Serikali kujipanga katika malipo ya wakazi wanaoishi karibu na mradi huo.
Tumeitaka Serikali iwape haki za msingi wakazi wa maeneo hayo, kwa kuwapa fidia ya mali zao, ikiwemo mashamba, nyumba, hatutarajii kuona migogoro ya ardhi inatokea kama Mwadui, Geita, alisema.
Naye Waziri kivuli wa Nishati na Madini, John Mnyika, aliitaka Serikali ichukue hatua zaidi za ukwepaji kodi na kuongeza mapato kwa serikali kwa mwaka wa fedha 2011/2012 kwa wizara ya Nishati na Madini kwa kushirikiana na wizara nyingine
Alisema mgodi huo, utaongeza ajira za kudumu kwa wakazi wa wilaya hiyo sambamba na utoaji wa elimu inayohusu masuala ya madini.
CHANZO: NIPASHE
HAYA TENA WARUSI ULAJI HUO TOKA KWA WALALA HOI WADANGANYIKA ALALAE USIMUAMSHE HATA KIDOGO.