Kampuni ya TIGO inaelekea kufa!!?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kampuni ya TIGO inaelekea kufa!!??

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by samirnasri, Dec 20, 2010.

 1. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #1
  Dec 20, 2010
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kampuni ya simu za mkononi ya tiGO ambayo imejizolea wateja wengi kuanzia mwaka 2005 baada ya kuanza kushusha garama za kupiga simu iko katika hali mbaya na huenda muda wowote ikafa na kuacha kampuni za voda na zain/airtel zikiendelea kutamba. Taarifa zaidi zinaeleza kua kampuni hiyo (tiGO) ambayo imetamba kwa muda mrefu na kuzipiga bao kampuni nyingine za simu za mkononi hapa nchini kwa kua na garama nafuu zaidi kwa kipindi kirefu hivi sasa imeshindwa kuendana na kasi ya ajabu ya kampuni mbili za vodacom na airtel ambazo nazo zimeamua kupunguza garama na kusababisha wateja wengi waliokua ama wameasi au wamepunguza kasi kutumia mitandao hiyo kurejea kundini kwa kishindo na kuanza kuuponda mtandao wa tigo. Inasemekana kampuni ya voda imekua ikikusanya fungu kubwa la pesa kupitia huduma ya M-PESA ambayo imesambaa zaidi vijijini tofauti na huduma ya tigo pesa ambayo iko zaidi maeneo ya mijini. Kitendo cha voda kuzindua huduma ya kupiga simu kwa garama ya nusu shilingi kwa sekunde kuanzia dakika ya kwanza kwa muda wa masaa 24 kumeishtua kampuni ya tigo ambayo inatoa huduma ya kupiga simu kwa nusu shilingi baada ya dakika ya kwanza tena kwa muda wa masaa 20. Wadau wa mitaani wanasema nusu shilingi ya tigo ina mipaka mingi kwa sababu inambana mtu kujiachia kuanzia mida ya sa 11jioni hadi sa 4 usiku vilevile haithamini mazungumzo ambayo hayazidi dakika moja. Wanasema tigo imeshagundua kwamba imeanza kukimbiwa na wateja ndo maa imebandika mabango yanayosomeka "usiache mbachao kwa msaala upitao". Taarifa nyingine zisizo rasmi zinadai tigo wameuza minara mingi na hivi sasa wanatumia garama nyingi sana kukodi minara hiyo kitu ambacho kitaharakisha kuanguka kwa tiGO... Source: habari za street...
   
 2. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #2
  Dec 20, 2010
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  SOURCE? Ama ndio mambo ya kupiga debe hayo.....
   
 3. shanature

  shanature JF-Expert Member

  #3
  Dec 20, 2010
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 718
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  huna hoja hahahahahahaha.......................hoi..............umetumwa na voda toa data...................hahahahaaaaahhhaaaaahha kha.........
   
 4. Monstgala

  Monstgala JF-Expert Member

  #4
  Dec 20, 2010
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 1,082
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Try again..
   
 5. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #5
  Dec 20, 2010
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145

  Samir

  Nakujibu ifuatavyo:


  1. Wewe ni ama "dealer" au "super dealer" wa Vodacom, au mwajiriwa wa Vodacom
  2. Habari hii ni pandikizi kutoka Vodacom, yenye lengo la KUIPAMBA Vodaocom kwa KUIPONDA Tigo, jambo ambalo nimelisoma kuanzia sentensi ya kwanza ya post yako hii
  3. Ukweli ni kwamba, SIO Airtel, Tigo wala Vodacom walioanzisha huma ya kupiga simu kwa nusu shilingi ndani ya mtandao, bali ni SASATEL! Pia, sio wote hao walioanzisha huduma ya kupiga simu kwa shilingi tatu kwa sekunde kwa mitandao yotem, bali pia ni Sasatel! Kampuni zote hizi zimefanya ku-copy and paste, na ZINAIOGOPA sana Sasatel! Lakini hawa wote, ukiondoa Sasatel, ni WAONGO, kwani, gharama hizo HAZIJUMUISHWI na VAT, jambo ambali Sasatel inafanya! HAYA NI MATANGAZO YA UONGO!
  4. Katika kuendelea kuigeza Sasatel, Tigo nayo - eti - sasa imeanzisha huduma ya kupiga simu bure BAADA YA DAKIKA YA KWANZA! Haitawasaidia. Sasatel walianzisha mpango wa kupiga simu bure, ndani ya mtandao, kuanzia saa 3 usiku hadi 1 asubuhi, MIEZI 12 iliyopita!
  5. Kweli, kiwango cha ubora wa huduma za Tigo kimeshuka sana, na hili litailetea matatizo hapo baadaye. Kwa sasa, kasi ya wateja wa Tigo kuuhama mtandao huo sio kubwa, kama ile ambayo imeongezeka baada ya Tigo kuanzisha huduma lukuki mpya, HUSUSAN Tigo Pesa!

  Hukumu yangu ni kwamba, Tigo haina nia, sabau wala haijakosa uwezo wa kifedha, wa kuifanya ifunge virago vyake! Tigo bado itakamua, japokuwa MIMI SI MTEJA WAO tena!
   
 6. Babuu blessed

  Babuu blessed JF-Expert Member

  #6
  Dec 20, 2010
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Kubali kataa tigo inaenda kufa na itajizika yenyewe,tangu lini huduma ya customer care ikalipiwa na ukimwamishia mtu salio kuna % unakatwa kama gharama za huduma.tigo wameflsika
   
 7. Chipukizi

  Chipukizi JF-Expert Member

  #7
  Dec 20, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 1,972
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  Tigo kuuza minara hiyo nnakataa.
  So far Vodacom ndo wana hali mbaya more than 100 people wamepunguzwa kazi.makampuni ambayo yalikuwa yanatoa huduma ktk baadhi ya vitengo ndani yavodacom e.g AfriKing imeondolewa kusevu garama.most of Vodashops including ya Mlimani city zimeuzwa kwa watu binafsi.na Pia Vodafone ya UK imenunua sharez nyingine nyingi tu so usishangae pia jina la vodacom likawa replaced na Vodafone.
   
 8. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #8
  Dec 20, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  unafanya watu hawana uwelewa hapa, umegonga mwamba, hiyo voda ndo hakuna kitu kabisa,nenda kawaambie hatuhami TIGO ndo mwanzo mwisho
   
 9. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #9
  Dec 20, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  nenda kazipeleke hizi habari zako huko huko kwenye vijiwe vyenu
   
 10. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #10
  Dec 20, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  mzee na wewe dealer au superdealer wa sasatel au pandikizi?????
   
 11. m

  mams JF-Expert Member

  #11
  Dec 20, 2010
  Joined: Jul 19, 2009
  Messages: 616
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35


  Siyo kweli na huna current data. Tigo wana robo shillingi na kama utafuatilia kwa makini wanaelekea kuwa the cheapest ever na hao waliokutuma waki match ndiyo kaburi lao.
   
 12. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #12
  Dec 20, 2010
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Unazungumzia sasatel huo mtandao unapatikana mikoa mingapi? Kubali usikubali TIGO sasa wameka kama CHELSEA yaani wameishiwa mbinu mpya, sio wabunifu tena. Sasa tigo wameku wanatafuta pesa kwa mbinu za ujanja ujanja. Just imagine huduma kwa wateja unalipia sh. 50 na ukihamisha salio unakatwa percentage fulani. Wanasema ongea bure baada ya dakika ya kwanza kuanzia sa sita usiku lakini ukiongea dakika kadhaa wanakata simu ili upige tena wakate pesa za dakika yao ya kwanza. Hizi ni dalili za wazi za kufulia na kama wangejua jinsi gani mambo hayo yanawakera wateja wao wangekwisha yaondoa siku nyingi. Tigo walikua na kigugumizi kupunguza garama za kupiga simu kwenda mitandao mingine baada ya voda na airtel kupunguza wakiamini kua wana wateja wengi wa tigo-tigo lakini walipogundua mapato yameshuka ndipo nao walipopunguza garama siku za hivi karibuni. Tigo ya enzi hizo isingesubiri muda wote huo kujibu mapigo ya voda na airtel. ...wateja wengi wa tigo sasa wamekat tamaa na mtandao wao.
   
 13. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #13
  Dec 20, 2010
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hiyn robo shilingi ya tigo inapatika na mikoa gani na muda upi? Najua wao wana nusu shilingi baada ya dakika ya kwanza inamaana ili ufaidi huduma hiyo lazima uongee zaidi ya dakika moja ha.... ha..... ha...... Voda ni nusu shilingi kuanzia sekunde ya kwanza tena kwa masaa 24 sio masaa 20. Upo hapo!.
   
 14. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #14
  Dec 20, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  ushabiki wa vijiweni huo
   
 15. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #15
  Dec 20, 2010
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Unazungumzia sasatel huo mtandao unapatikana mikoa mingapi? Kubali usikubali TIGO sasa wameka kama CHELSEA yaani wameishiwa mbinu mpya, sio wabunifu tena. Sasa tigo wameku wanatafuta pesa kwa mbinu za ujanja ujanja. Just imagine huduma kwa wateja unalipia sh. 50 na ukihamisha salio unakatwa percentage fulani. Wanasema ongea bure baada ya dakika ya kwanza kuanzia sa sita usiku lakini ukiongea dakika kadhaa wanakata simu ili upige tena wakate pesa za dakika yao ya kwanza. Hizi ni dalili za wazi za kufulia na kama wangejua jinsi gani mambo hayo yanawakera wateja wao wangekwisha yaondoa siku nyingi. Tigo walikua na kigugumizi kupunguza garama za kupiga simu kwenda mitandao mingine baada ya voda na airtel kupunguza wakiamini kua wana wateja wengi wa tigo-tigo lakini walipogundua mapato yameshuka ndipo nao walipopunguza garama siku za hivi karibuni. Tigo ya enzi hizo isingesubiri muda wote huo kujibu mapigo ya voda na airtel. ...wateja wengi wa tigo sasa wamekat tamaa na mtandao wao.
   
 16. t

  tumwe273us Member

  #16
  Dec 20, 2010
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yetu macho n cha msingi,mtz anaangalia pa urahisi n ht mimi nina tigo na voda,bt nionapo pa urahisi ndio nitakapokimbilia.
  Kwaruzaneni ila wtz tunaangalia penye unafuu.
  Napenda ushindani uendelee ili sisi wapiga simu tufaidi.
   
 17. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #17
  Dec 20, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  matangazo.
   
 18. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #18
  Dec 20, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  tiGo wapo juu sana

  Voda wamesha poteza wateja lukuki wamehamia tiGo
   
 19. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #19
  Dec 20, 2010
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Walioo....fuliaaaaaa lazima tukubali tigo inayumba na sina hakika kama mwaka 2011 utaisha tigo ikiwa salama. Anyway time will tell.
   
 20. m

  mamakunda JF-Expert Member

  #20
  Dec 20, 2010
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 371
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Inawezekana maanayake maelezo yake yote yameegemea huko!
   
Loading...