poposindege
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 456
- 175
Kampuni ya mawasiliano ya Smart Tanzania tangu siku ya jumapili hawapo hewani na hakuna taarifa yoyote rasmi kwa wateja wao ni kipi kimewakumba.
Kuanzia jumanne walirudisha huduma kwa wateja wao wa Intaneti wanaotumia Router/mifi lakini wale wa mawasiliano ya simu mpaka leo hakuna kitu.
Kwa sasa kwenye simu kunaonekana mnara wa simu umepanda (Network) lakini hakuna mawasiliano yoyote utakayoweza kuyapata.
Kinachosikikitisha mpaka sasa kampuni haijatoa taarifa yoyote kwa wateja wake kiasi cha kuleta usumbufu mkubwa wa kujua nini kinaendelea.
Taarifa zilizopatikana ambazo sio rasmi ni kwamba kulikuwa na matatizo kwenye Seva yao jambo ambalo linaonekana halipo wazi sana.
Smart tunaomba mtujulishe nini kimetokea au tutupe laini zenu.