View attachment 1607466
Kampuni ya simu TECNO yazindua rasmi TECNO Spark 5pro. Uzinduzi wa simu hiyo umefanyika Kidimbwi Beach tarehe 18/10/2020 na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali akiwemo komediani maarufu Jaymond na wadau wa simu za TECNO.
View attachment 1607471
Uzinduzi wa Spark 5pro ulifanyika katika mfumo wa party ambapo DJ Maphorissa kutoka South alitoa burudani ya kutosha na kuufanya uzinduzi wa Spark 5pro kuwa wa aina yake.
View attachment 1607473
“Spark 5pro sio simu ya kwanza kwa kampuni ya TECNO kuzinduliwa kwa mfumo wa party na hii imejirudia kwasababu Spark 5pro ni simu yenye kutulenga vijana wa kileo na ili kuweza kutufikia kwa uharaka zaidi basi ni lazima kutumia njia zetu kama hivi
Baadhi ya sifa zinazopatikana katika simu hii ya TECNO spark 5pro ni uwezo wa simu hii kuwa na ukubwa wa memory ya GB 64ROM + GB 3RAM, selfie ya megapixel 8 na kamera ya nyuma ni megapixel 16M+2M+2M+AI Lens, battery ya ujazo wa mAh 5000, alisema msanii maarufu wa comedian Jaymond ambaye ndio mgeni mualikwa katika uzinduzi huo”.
View attachment 1607488
“Uzinduzi wa Spark 5pro ni wa aina yake sisi kama wateja wa simu za TECNO tumefurahi kuona namna TECNO inavyotujali na kututhamini, tumekula tumekunywa lakini pia tumepata nafasi yakupiga picha na mgeni mualikwa alisema Bwana Haji Omary”.
TECNO Spark 5pro sasa inapatikana katika maduka yote ya simu nchini Tanzania.
Ili kufahamu mengi zaidi tembelea mara kwa mara ukurasa wa Instagram
Login • Instagram