Jannatul Firdaus
JF-Expert Member
- Aug 4, 2026
- 446
- 1,112
Kampuni ya Sandaland Fashion Wear Limited imetangaza nia ya kuchukua hatua za kisheria dhidi ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, kufuatia kauli yake aliyoitoa hivi karibuni kwenye mitandao ya kijamii iliyoponda ubora na uhalali wa jezi mpya za timu ya taifa ya mpira wa miguu (Taifa Stars).
Sakata hili limeibuka kufuatia taarifa iliyotolewa leo, Septemba 18, 2026, na kampuni hiyo nchini Tanzania, ikijibu ujumbe wa Waziri Makonda uliowekwa Septemba 16, 2026 kwenye ukurasa wake wa Instagram unaosema:
"Hii sio jezi ya Taifa Stars, Taifa Stars kwa ubora wake hatuwezi kuwa na jezi za kiwango chini hivi, acheni kutumia picha za Naibu wangu huku Ofisi yangu haina taarifa."
Sandaland imeeleza kuwa imechukua hatua hiyo kwa sababu kauli ya Waziri imesababisha sintofahamu na kuiletea kampuni madhara makubwa, ikifafanua kupitia taarifa yao kuwa:
"Kauli hiyo iliyozua taharuki na sintofahamu mpaka sasa imekwishasababisha madhara makubwa sana ya kihadhi na kiuchumi."
Wamesisitiza kuwa wana mkataba halali na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wa kutengeneza na kusambaza jezi hizo ambazo tayari zimeshatumika katika mashindano mbalimbali ya timu za taifa za wanaume na wanawake.
Pia soma: Sandaland Kuiburuza Mahakamani Wizara ya Michezo Kuhusu Jezi za Taifa Stars