Ngaliba Dume
JF-Expert Member
- Oct 6, 2010
- 1,710
- 3,669
Inaitwa air force onehivi ndege ya rais wa Tanzania nayo Si inaitwa Tanzania Air au?
Nipo mkuu,huyo kwenye Avatar ni mwanao?
Viongozi wa CCM ni zaidi ya waigizajikuna vitu vinachekesha yani huyo Naibu waziri tuseme toka amekuwa waziri Miaka 2 sasa hajui kuwa kulikuwa na kampuni hiyo au?
Nilitaka kushangaa sana na mmeamko yako ya siasaViongozi wa CCM ni zaidi ya waigizaji
Mkuu mimi pia nimeona habari hiyo kupitia mitandao,nilishangaa sana.Nimeshangaa kwa sababu Samaras amekuwapo hapo toka miaka ya 1960's(kama sijakosea),wakati hiyo Terminal Two imejengwa hapo na Nyerere miaka ya 1980's,kama nakumbuka vizuri jiwe la msingi aliweka marehemu Abdul Jumbe.Mkuu barafu tunahitaji msaada wako
Mkuu haziegeshwi Terminal One,hizi zinaegeshwa kwenye TanzanAir Terminal.Huyu jamaa ana terminal yake,ana maegesho yake,ana karakana yake(Hangar for servicing) na ana walinzi wake na mashine zake za ukaguzi wa abiria wake.Ni kiwanja kinachojitegemea ndani ya Uwanja wa JNIA.Yaani huu uwanja ni kama Vatican ndani ya Italia,nchi ndani ya nchi.Inashangaza kidogo,lakini historia yake ni ndefu.Hii ni kampuni inayomiliki ndege ndogo na kama za Tropical Air, Auric Air, Coastal nk, safari zake nyingi huwa ni kati ya Zanzibar na Dar, Mafia, songosongo, Kilwa, Saadan na hata sehem kama Mwanza, Geita na mikoa mingine ila mara nyingi huenda huko mikoani kwa kukodiwa na si route kama za Fast Jet, kwa hapa JNIA zinatua na kuegeshwa Terminal one (Uwanja wa Zamani) kuhusu mmiliki ni nani hapo kuna mengi ya kuelezwa labda waje wataalam wa kuchimbua kama BARAFU, BAK na wengineo
Kwa maana hii anahusika na utoroshwaji wa madini??Mkuu mimi pia nimeona habari hiyo kupitia mitandao,nilishangaa sana.Nimeshangaa kwa sababu Samaras amekuwapo hapo toka miaka ya 1960's(kama sijakosea),wakati hiyo Terminal Two imejengwa hapo na Nyerere miaka ya 1980's,kama nakumbuka vizuri jiwe la msingi aliweka marehemu Abdul Jumbe.
Hiyo kampuni ya Mzee mmoja wa kigiriki anaitwa Samaras Dinos,alikuwa ni mkulima wa katani huko Morogoro toka enzi za mkoloni,wakati wa utaifishaji,mashamba yake aliyachukua Nyerere.
Jamaa alikuwa na kindege chake kidogo miaka hiyo ya 1950's alitumia kukagulia mashamba yake Morogoro,watu wa Moro wanampata sana Samaras(Mgiriki).Alikuwa anaruka na kindege chake toka hapo ulipo leo hii huo uwanja wanaotaka kumpoka.
Mashamba yake yalipochukuliwa na Serikali,akaamua kujikita katika biashara ya usafiri wa anga,enzi hata Air Tanzania haijaanzishwa,tukiwa bado kwenye East Africa Airways.Akaanzisha kampuni ya Tanzanian Air Services Ltd(Maarufu kama TanzanAir)
Hilo eneo amekuwa nalo miaka na miaka,wakati serikali ya mkoloni ikiwa bado inatumia uwanja wa ndege eneo la karibu na Uwanja wa Taifa mpira,hata wanavyohamia kuleee Terminal One,Samaras alikuwa kashaanza mambo yake pale alipo leo.Serikali ndio ilimfuata.
Hii kampuni ina ndege za kukodi tu,wanasiasa wamezitumia sana wakati wa kampeni,ndege moja yenye hadhi ya VIP hutumiwa na Waziri Mkuu na makamu wake kwa kukodisha.Sijui huyu Naibu Waziri atauweza huu mbuyu kweli??
Ana ndege maalumu kwa ajili ya Corporate Flights,Aerial Survey,Medical Evacuations,hunting,kupiga picha nk.
Samaras mwenyewe alifariki,kaacha watoto wake wawili,wa kike na wa kiume.
Kwa kifupi hii ndio kampuni pekee yenye mkataba wa kusafirisha madini yoooote ya Tanzania toka katika migodi yote iliyopo huko porini na kuyaleta Dsm tayari kwa kupelekwa nje ya nchi.
Ina eneo lake la abiria,karakana ya kutengeneza ndege na strong room ya kutunza madini ambayo hata serikali ya Tz haina pale uwanjani(labda wajenge sasa)
Kwenye jengo la hii kampuni,ndio ule mzigo wa almasi ya Mwadui iliyotaka kusafirishwa nje "kiuwizi" ilikamatwa.Kwa hiyo madini yote hubebwa na kampuni hii na kutunzwa ktk jengo lao kabla ya kusafrishwa.Sijajua kwa siku hizi au awamu hii kama na serikali pia imeamua kujenga strong room hapo,nitauliza wadau wangu wa hapo JNIA.
Duh, aisee.Mkuu mimi pia nimeona habari hiyo kupitia mitandao,nilishangaa sana.Nimeshangaa kwa sababu Samaras amekuwapo hapo toka miaka ya 1960's(kama sijakosea),wakati hiyo Terminal Two imejengwa hapo na Nyerere miaka ya 1980's,kama nakumbuka vizuri jiwe la msingi aliweka marehemu Abdul Jumbe.
Hiyo kampuni ya Mzee mmoja wa kigiriki anaitwa Samaras Dinos,alikuwa ni mkulima wa katani huko Morogoro toka enzi za mkoloni,wakati wa utaifishaji,mashamba yake aliyachukua Nyerere.
Jamaa alikuwa na kindege chake kidogo miaka hiyo ya 1950's alitumia kukagulia mashamba yake Morogoro,watu wa Moro wanampata sana Samaras(Mgiriki).Alikuwa anaruka na kindege chake toka hapo ulipo leo hii huo uwanja wanaotaka kumpoka.
Mashamba yake yalipochukuliwa na Serikali,akaamua kujikita katika biashara ya usafiri wa anga,enzi hata Air Tanzania haijaanzishwa,tukiwa bado kwenye East Africa Airways.Akaanzisha kampuni ya Tanzanian Air Services Ltd(Maarufu kama TanzanAir)
Hilo eneo amekuwa nalo miaka na miaka,wakati serikali ya mkoloni ikiwa bado inatumia uwanja wa ndege eneo la karibu na Uwanja wa Taifa mpira,hata wanavyohamia kuleee Terminal One,Samaras alikuwa kashaanza mambo yake pale alipo leo.Serikali ndio ilimfuata.
Hii kampuni ina ndege za kukodi tu,wanasiasa wamezitumia sana wakati wa kampeni,ndege moja yenye hadhi ya VIP hutumiwa na Waziri Mkuu na makamu wake kwa kukodisha.Sijui huyu Naibu Waziri atauweza huu mbuyu kweli??
Ana ndege maalumu kwa ajili ya Corporate Flights,Aerial Survey,Medical Evacuations,hunting,kupiga picha nk.
Samaras mwenyewe alifariki,kaacha watoto wake wawili,wa kike na wa kiume.
Kwa kifupi hii ndio kampuni pekee yenye mkataba wa kusafirisha madini yoooote ya Tanzania toka katika migodi yote iliyopo huko porini na kuyaleta Dsm tayari kwa kupelekwa nje ya nchi.
Ina eneo lake la abiria,karakana ya kutengeneza ndege na strong room ya kutunza madini ambayo hata serikali ya Tz haina pale uwanjani(labda wajenge sasa)
Kwenye jengo la hii kampuni,ndio ule mzigo wa almasi ya Mwadui iliyotaka kusafirishwa nje "kiuwizi" ilikamatwa.Kwa hiyo madini yote hubebwa na kampuni hii na kutunzwa ktk jengo lao kabla ya kusafrishwa.Sijajua kwa siku hizi au awamu hii kama na serikali pia imeamua kujenga strong room hapo,nitauliza wadau wangu wa hapo JNIA.
Wako vizuri sana.Ndio wenye tender ya kumsafirisha Waziri Mkuu na Makamu wa Rais kwa ndege zao,pale ambapo ndege za serikali zinapokuwa matengenezo au kuwa na uwezo mdogo kufika viwanja korofi kama vya Nachingwea na ManyaraDuh, aisee.
Kumbe wako njema namnna hii??
Ila sasa kwenye swala la usalama wa madini yetu hapo ndio utata,
Kama vipi wautaifishe tu huo Uwanja wake
Tusitake kumchafua mtu ile almasi ilikuwa haitoroshwi bali serikali ililalamika kuwa waraalamu wake na wale wa mgodi wameikadirikia kwa thamani ya chini ndo maana ikakamatwa, masuala ya madini ukiambiwa jiongeze na wewe kiakiliKwa maana hii anahusika na utoroshwaji wa madini??