Ngaliba Dume
JF-Expert Member
- Oct 6, 2010
- 1,710
- 3,669
Juzi niliona kwenye taarifa ya habari ya Azam Two na humu JF kuleta uzi toka Azam Two Fb kuwa Naibu waziri wa Uchukuzi na Mawasilaino ametembelea Airport JNIA(Julius Nyerere Internationa Airport) na kukuta kuna kampuni inaitwa Tanzania Air ambayo inamiliki uwanja wake binafsi ndani ya Uwanja wa ndege wa nchi wa JNIA.
Humu JF huwa hakiharibiki kitu,nimekuwa interested kufahamu,inakuwaje kampuni hii ya mtu binafsi imiliki uwanja wa ndege unaojitegemea ndani ya uzio wa uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere?Na je kampuni hii ya Tanzania Air inatumika kusafirisha abiria kwenda wapi?Kuna mtu humu JF amewahi kutumia ndege za kampuni hii kusafiri kwenda mahali popote hapa Tanzania??
Nimepita mtandaoni nimeona nembo ya kampuni hii ni Twiga kama ilivyo Air Tanzania,japo hii ni kichwa tu cha twiga,Kuna mahusiano yoyote ya kibiashara kati ya Air Tanzania na Tanzania Air?
Je,suala la usalama na uthibiti wa magendo umekaaje kwa uwanja binafsi wa ndege kuwa ndani ya kiwanja cha ndege cha kimataifa cha nchi?Na kama raia/mfanyabiashara akitaka kumiliki uwanja wake binafsi wa ndege kama huo wa Tanzania Air,sheria za nchi zinasemaje ili watu waone uwezekano wa kujenga viwanja vyao vya ndege??
Jf hakiaribiki kitu,bila shaka tutajuzana.