Kampuni ya ndege ya TanzanAir inayosakamwa na serikali ni ya nani? Ikawaje na uwanja binafsi ndani ya JNIA?

Ngaliba Dume

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
1,710
3,669
image.jpeg
image.jpeg

Juzi niliona kwenye taarifa ya habari ya Azam Two na humu JF kuleta uzi toka Azam Two Fb kuwa Naibu waziri wa Uchukuzi na Mawasilaino ametembelea Airport JNIA(Julius Nyerere Internationa Airport) na kukuta kuna kampuni inaitwa Tanzania Air ambayo inamiliki uwanja wake binafsi ndani ya Uwanja wa ndege wa nchi wa JNIA.

Humu JF huwa hakiharibiki kitu,nimekuwa interested kufahamu,inakuwaje kampuni hii ya mtu binafsi imiliki uwanja wa ndege unaojitegemea ndani ya uzio wa uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere?Na je kampuni hii ya Tanzania Air inatumika kusafirisha abiria kwenda wapi?Kuna mtu humu JF amewahi kutumia ndege za kampuni hii kusafiri kwenda mahali popote hapa Tanzania??

Nimepita mtandaoni nimeona nembo ya kampuni hii ni Twiga kama ilivyo Air Tanzania,japo hii ni kichwa tu cha twiga,Kuna mahusiano yoyote ya kibiashara kati ya Air Tanzania na Tanzania Air?

Je,suala la usalama na uthibiti wa magendo umekaaje kwa uwanja binafsi wa ndege kuwa ndani ya kiwanja cha ndege cha kimataifa cha nchi?Na kama raia/mfanyabiashara akitaka kumiliki uwanja wake binafsi wa ndege kama huo wa Tanzania Air,sheria za nchi zinasemaje ili watu waone uwezekano wa kujenga viwanja vyao vya ndege??

Jf hakiaribiki kitu,bila shaka tutajuzana.
 
Hii ni kampuni inayomiliki ndege ndogo na kama za Tropical Air, Auric Air, Coastal nk, safari zake nyingi huwa ni kati ya Zanzibar na Dar, Mafia, songosongo, Kilwa, Saadan na hata sehem kama Mwanza, Geita na mikoa mingine ila mara nyingi huenda huko mikoani kwa kukodiwa na si route kama za Fast Jet. Kwa hapa JNIA zinatua na kuegeshwa Terminal one (Uwanja wa Zamani).

Kuhusu mmiliki ni nani hapo kuna mengi ya kuelezwa labda waje wataalam wa kuchimbua kama barafu, BAK na wengineo
 
Mkuu barafu tunahitaji msaada wako
Mkuu mimi pia nimeona habari hiyo kupitia mitandao,nilishangaa sana.Nimeshangaa kwa sababu Samaras amekuwapo hapo toka miaka ya 1960's(kama sijakosea),wakati hiyo Terminal Two imejengwa hapo na Nyerere miaka ya 1980's,kama nakumbuka vizuri jiwe la msingi aliweka marehemu Abdul Jumbe.

Hiyo kampuni ya Mzee mmoja wa kigiriki anaitwa Samaras Dinos,alikuwa ni mkulima wa katani huko Morogoro toka enzi za mkoloni,wakati wa utaifishaji, mashamba yake aliyachukua Nyerere.

Jamaa alikuwa na kindege chake kidogo miaka hiyo ya 1950's alitumia kukagulia mashamba yake Morogoro, watu wa Moro wanampata sana Samaras(Mgiriki). Alikuwa anaruka na kindege chake toka hapo ulipo leo hii huo uwanja wanaotaka kumpoka.

Mashamba yake yalipochukuliwa na Serikali, akaamua kujikita katika biashara ya usafiri wa anga,enzi hata Air Tanzania haijaanzishwa,tukiwa bado kwenye East Africa Airways. Akaanzisha kampuni ya Tanzanian Air Services Ltd(Maarufu kama TanzanAir)

Hilo eneo amekuwa nalo miaka na miaka,wakati serikali ya mkoloni ikiwa bado inatumia uwanja wa ndege eneo la karibu na Uwanja wa Taifa mpira,hata wanavyohamia kuleee Terminal One, Samaras alikuwa kashaanza mambo yake pale alipo leo. Serikali ndio ilimfuata.

Hii kampuni ina ndege za kukodi tu,wanasiasa wamezitumia sana wakati wa kampeni, ndege moja yenye hadhi ya VIP hutumiwa na Waziri Mkuu na makamu wake kwa kukodisha. Sijui huyu Naibu Waziri atauweza huu mbuyu kweli??

Ana ndege maalumu kwa ajili ya Corporate Flights,Aerial Survey, Medical Evacuations, hunting, kupiga picha nk.

Samaras mwenyewe alifariki,bkaacha watoto wake wawili, wa kike na wa kiume.

Kwa kifupi hii ndio kampuni pekee yenye mkataba wa kusafirisha madini yoooote ya Tanzania toka katika migodi yote iliyopo huko porini na kuyaleta Dar tayari kwa kupelekwa nje ya nchi.

Ina eneo lake la abiria, karakana ya kutengeneza ndege na strong room ya kutunza madini ambayo hata serikali ya Tz haina pale uwanjani(labda wajenge sasa).

Kwenye jengo la hii kampuni,ndio ule mzigo wa almasi ya Mwadui iliyotaka kusafirishwa nje "kiuwizi" ilikamatwa. Kwa hiyo madini yote hubebwa na kampuni hii na kutunzwa ktk jengo lao kabla ya kusafrishwa. Sijajua kwa siku hizi au awamu hii kama na serikali pia imeamua kujenga strong room hapo,nitauliza wadau wangu wa hapo JNIA.

Mwaka 2009, yaani mwaka mmoja kabla ya Samarasi kufariki, Serikali ilimpa tuzo maalumu ya "The Father of Aviation Indusrty", sasa sijui huyu Naibu Waziri hajui kwanini huyu mtu alipata hii tuzo? Ni kwa sababu 1969 wakati nchi ikiwa haina ndege, yeye alikuwa nayo binafsi!
 
Hii ni kampuni inayomiliki ndege ndogo na kama za Tropical Air, Auric Air, Coastal nk, safari zake nyingi huwa ni kati ya Zanzibar na Dar, Mafia, songosongo, Kilwa, Saadan na hata sehem kama Mwanza, Geita na mikoa mingine ila mara nyingi huenda huko mikoani kwa kukodiwa na si route kama za Fast Jet, kwa hapa JNIA zinatua na kuegeshwa Terminal one (Uwanja wa Zamani) kuhusu mmiliki ni nani hapo kuna mengi ya kuelezwa labda waje wataalam wa kuchimbua kama BARAFU, BAK na wengineo
Mkuu haziegeshwi Terminal One,hizi zinaegeshwa kwenye TanzanAir Terminal.Huyu jamaa ana terminal yake,ana maegesho yake,ana karakana yake(Hangar for servicing) na ana walinzi wake na mashine zake za ukaguzi wa abiria wake.Ni kiwanja kinachojitegemea ndani ya Uwanja wa JNIA.Yaani huu uwanja ni kama Vatican ndani ya Italia,nchi ndani ya nchi.Inashangaza kidogo,lakini historia yake ni ndefu.

Huyu Mzee alikuwa rafiki mkubwa sana wa Mwalimu Nyerere,baada ya kuchukua mashamba yake ya mkonge kule Morogoro,jamaa akamua kumuachia tu Nyerere,lakini akasema anaanzisha kampuni ya ndege,na hapo inasemwa hata "hati ya umiliki" wa miaka 99 aliipata enzi za Mwalimu.

Sijajua huyu Naibu Waziri kama anajua historia ya hili eneo na serikali.Kuna sehemu unaweza kugusa ukaondoka wewe,mwenye eneo akabaki
 
Mkuu mimi pia nimeona habari hiyo kupitia mitandao,nilishangaa sana.Nimeshangaa kwa sababu Samaras amekuwapo hapo toka miaka ya 1960's(kama sijakosea),wakati hiyo Terminal Two imejengwa hapo na Nyerere miaka ya 1980's,kama nakumbuka vizuri jiwe la msingi aliweka marehemu Abdul Jumbe.

Hiyo kampuni ya Mzee mmoja wa kigiriki anaitwa Samaras Dinos,alikuwa ni mkulima wa katani huko Morogoro toka enzi za mkoloni,wakati wa utaifishaji,mashamba yake aliyachukua Nyerere.

Jamaa alikuwa na kindege chake kidogo miaka hiyo ya 1950's alitumia kukagulia mashamba yake Morogoro,watu wa Moro wanampata sana Samaras(Mgiriki).Alikuwa anaruka na kindege chake toka hapo ulipo leo hii huo uwanja wanaotaka kumpoka.

Mashamba yake yalipochukuliwa na Serikali,akaamua kujikita katika biashara ya usafiri wa anga,enzi hata Air Tanzania haijaanzishwa,tukiwa bado kwenye East Africa Airways.Akaanzisha kampuni ya Tanzanian Air Services Ltd(Maarufu kama TanzanAir)

Hilo eneo amekuwa nalo miaka na miaka,wakati serikali ya mkoloni ikiwa bado inatumia uwanja wa ndege eneo la karibu na Uwanja wa Taifa mpira,hata wanavyohamia kuleee Terminal One,Samaras alikuwa kashaanza mambo yake pale alipo leo.Serikali ndio ilimfuata.

Hii kampuni ina ndege za kukodi tu,wanasiasa wamezitumia sana wakati wa kampeni,ndege moja yenye hadhi ya VIP hutumiwa na Waziri Mkuu na makamu wake kwa kukodisha.Sijui huyu Naibu Waziri atauweza huu mbuyu kweli??

Ana ndege maalumu kwa ajili ya Corporate Flights,Aerial Survey,Medical Evacuations,hunting,kupiga picha nk.

Samaras mwenyewe alifariki,kaacha watoto wake wawili,wa kike na wa kiume.

Kwa kifupi hii ndio kampuni pekee yenye mkataba wa kusafirisha madini yoooote ya Tanzania toka katika migodi yote iliyopo huko porini na kuyaleta Dsm tayari kwa kupelekwa nje ya nchi.

Ina eneo lake la abiria,karakana ya kutengeneza ndege na strong room ya kutunza madini ambayo hata serikali ya Tz haina pale uwanjani(labda wajenge sasa)

Kwenye jengo la hii kampuni,ndio ule mzigo wa almasi ya Mwadui iliyotaka kusafirishwa nje "kiuwizi" ilikamatwa.Kwa hiyo madini yote hubebwa na kampuni hii na kutunzwa ktk jengo lao kabla ya kusafrishwa.Sijajua kwa siku hizi au awamu hii kama na serikali pia imeamua kujenga strong room hapo,nitauliza wadau wangu wa hapo JNIA.
Kwa maana hii anahusika na utoroshwaji wa madini??
 
Duh, aisee.
Kumbe wako njema namnna hii??
Ila sasa kwenye swala la usalama wa madini yetu hapo ndio utata,
Kama vipi wautaifishe tu huo Uwanja wake
 
jingalao
Sijui kama anahusika na utoroshwaji wa madini,sina ushahidi wa moja kwa moja.Nachojua ni kuwa,kampuni hii imeingia mkataba na makampuni ya madini,ili kuweza kusafirisha madini toka katika viwanja vya migodi,kuleta uwanja wa ndege Dsm ili kusafirisha nje ya nchi.

Suala la wao kuhusika sijui,ndio maana hata wakati ule,serikali haikukamata TanzanAir,iliwakamata wale jamaa wa Mwadui.
 
Duh, aisee.
Kumbe wako njema namnna hii??
Ila sasa kwenye swala la usalama wa madini yetu hapo ndio utata,
Kama vipi wautaifishe tu huo Uwanja wake
Wako vizuri sana.Ndio wenye tender ya kumsafirisha Waziri Mkuu na Makamu wa Rais kwa ndege zao,pale ambapo ndege za serikali zinapokuwa matengenezo au kuwa na uwezo mdogo kufika viwanja korofi kama vya Nachingwea na Manyara
 
21 Reactions
Reply
Back
Top Bottom