Kampuni ya NALA yapata uwekezaji wa bilioni 106

Kampuni ya NALA yapata uwekezaji wa bilioni 106

Natafuta mawasiliano ya moja kwa moja na huyu mmiliki wa NALA kijana Fernandes. Nina wazo nyeti ambalo ningependa kumpatia na naamini kwa uwezo wake kitaalamu anaweza kuleta suluhisho kubwa kwa watanzania na watumiaji wengine wa mataifa mengine. Niliwahi kutoa wazo nyeti kwenye moja ya makampuni ya simu nchini zaidi ya miaka 15 iliyopita na ndani ya miezi mitatu wazo hilo likafanyiwa kazi na kampuni hiyo na sasa mamilioni ya watanzania wanafaidika na hilo wazo langu.
 
Fernandez ni mtanzania? Watanzania wanadanga na kuvuta mibangi huko halafu mnajipendekeza kwa watoto wa nchi nyingine?
Hiyo bilion dollar from diaspora kila mwaka inayoingia katika Economy ya Tanzania inatoka kwa hao unaowaita wavuta Bangi, zile nyumba nyingi za mikoani, mbweni na Bunju zinazofanya makampuni yenu ya ujenzi na wauza vifaa vya ujenzi mpate millions kila mwaka ni Fernandez peke yake?piga kelele tuu lakini mfagizi wa US anachangia uchumi wa bongo kuliko hao mafisadi na V8 zao
 
Sio lazima usifie lwanachofanya lakini kwanini uponde kama sio wivu au ujinga tuu? acha wapige pesa na sisi tupate huduma tunayohitaji, wewe ishi na sumu zako
Nimeponda wapi? Nimeuliza anafanya nini tofauti na wengine wanaotoa huduma hizo za kutuma pesa, na ufadhili huo unasaidiaje wateja wake, au anaposema itamsaidia kuboresha huduma zake ni vipi na itawasaidiaje wateja wake?
Umeumizwa na nini hapo?!
 
Ukitaka kuamini kufanya kitu ambacho sio kipya ni ngumu zaidi kuliko kufanya kitu kipya jaribu kutengeneza forum kama hii ya Jamiiforums halafu uone kama utakua na ubavu wa kushindana.

Jamaa anastahili pongezi, amezikuta app nyingi tu zinazotoa huduma kama yake na bado ameweza kupenya kwenye soko na anazidi kutoboa.
Ok sawa, je nini faida ya taarifa yake kwenu wateja wake? na ufadhili huo una kusaidiaje wewe mtumia huduma? Au ikiwa utamsaidia yeye kuboresha huduma zake wewe unafaidikaje na wapi?
...Na hilo nenda ukaliangalie?
 
Ebwanawee sijui hataki kuajiri Vijana wa kisasa Ngoma ihamishwe kua digital maana Agape TV bado ipo analogy TV kibao zimewakuta Agape ilikuepo enzi hizo TV pekee ni TVT, CTN, ITV na C2C bila kusahau Channel O hapo East Africa TV bado haijaanza alafu ilivyoanza haikuitwa hivyo
Nafkiri ameamua kuifanya iwe channel au TV ya dini... Hataki haya mambo ya kisasa. Wapo wengi tu kina radio Maria, tumaini, TV Imaan, TVZ n.k
 
Nafkiri ameamua kuifanya iwe channel au TV ya dini...
Sio ya Dini nazungumzia kuihamisha toka analogy kwenda digital muonekano wa kisasa sio ule wa kizamani hata km sio HD bado ipo analogy unaposema TV za Dini zote zipo digital Tumain TV, Upendo TV, TV Imaan, Arise n Shine, Emmanuel Tv zote zipo digital zina muonekano wa kisasa isipokua Agape TV tu ndio bado ipo analogy muonekano ule ule wa 1990, TV hizo za Dini zote hazikuwepo kipindi Agape TV ina-operate mpaka hio Emmanuel Tv ya marehemu TB Joshua haikuwepo Agape TV ni ya zamani imeanza enzi hizo TBC inaitwa TVT na ndio ilikua na muonekano mzuri kuzidi hio TVT angalia TBC sasa hivi muonekano wa kisasa Agape TV ilikuepo kabla ya Channel 5 kuwepo mpaka kubadirishwa Jina na kuitwa East Africa TV yaan EATV Agape TV ilikuepo ni TV ya zamani na muonekano umebakia ule ule wa zamani haijabadirishwa kua na muonekano wa kisasa
 
Hapa tunajipendekeza tu, akina Mwajuma, Maganga, Mwakipesile, Massawe na Kokushubila ndiyo watanzania halisi
Hapana hapo utakuwa tu unambagua kisa rangi, fikiria mtu babu yake alihamia hapa kabla hata ya wangoni, sasa yeye na hao wangon nani mtanzania halisi maanq wote ni wahamiaji! Halafu dunia yote cc ni wahamiaji, maana kiasili maisha yalianzia katikati ya iran na iraq, kote huku wanadam wametawanyika tu
 
Sote tuna la kujifunza toka kwa Ben...

Wahenga husema, penye nia pana njia...
 
Hizo zote ni Proctenism tactics za chama Cha mambuzi Ili waendelee kudumu madarakani.

Usipotaka kuungana nao katika uwekezaji ndiyo yanatokea hayo ya hajakidhi vigezo 😁Yani wanataka kufanya biashara yako kama ya ukoo kila mtu awe anakuja kuomba omba pesa! RC, DAS, RPC waje kuokota kama Mwijaku!
 
Natafuta mawasiliano ya moja kwa moja na huyu mmiliki wa NALA kijana Fernandes. Nina wazo nyeti ambalo ningependa kumpatia na naamini kwa uwezo wake kitaalamu anaweza kuleta suluhisho kubwa kwa watanzania na watumiaji wengine wa mataifa mengine. Niliwahi kutoa wazo nyeti kwenye moja ya makampuni ya simu nchini zaidi ya miaka 15 iliyopita na ndani ya miezi mitatu wazo hilo likafanyiwa kazi na kampuni hiyo na sasa mamilioni ya watanzania wanafaidika na hilo wazo langu.
Ndio shida inapokujaga hapo, wazo lako unampa nani kwenye hii dunia isiyo na watu waaminifu.

Kuwa makini sana kutangaza mawazo yenye faida wengine bure bure au kukutana na watu bila ya mwanasheria wako au lutoowekea patent.
 
Leo Julai 9, 2024 saa tatu asubuhi kwa saa New York Marekeni, Kampuni ya NALA iliyoanzishwa na Kijana Mtanzania Benjamin Fernandes, imetangazwa kwenye soko la hisa la Marekani NASDAQ kupata uwekezaji wa dola za Kimarekani milioni 40 ( Tsh. Bilioni 106) uwekezaji ambao utaiwezesha kutimiza lengo lake la kukua zaidi kimataifa na kuboresha ubora na usalama wa malipo barani Afrika kwa kupita mfumo mpya wa malipo uliotengenezwa na Kampuni hiyo uitwao Rafiki.

NALA imepata uwekezaji huu kutoka kwenye Kampuni kubwa za Uwekezaji duniani kama vile Acrew Capital, DST Global, Amplo na nyinginezo ambapo itatumia uwekezaji huu kutimiza malengo yake ya kimataifa kwa kufanya vitu vikuu viwili kwa sasa ambavyo ni kuongeza huduma za kutuma na kupokea fedha nje ya Afrika na kutengeneza huduma za kibenki kwa ajili ya Wahamiaji na Watu waishio ughaibuni.

Taarifa ya NALA imesema mfumo wake mpya wa kimataifa wa malipo uitwao Rafiki unatarajiwa kutumiwa na Watu Bilioni ambapo utawahakikishia Wateja huduma za malipo zenye ubora na usalama wa kiwango cha juu, huduma nzuri za fedha za kigeni, gharama nafuu za miamala na kuwezesha biashara kutuma na kupokea malipo kwa urahisi sambamba na kuleta mapinduzi kwenye huduma za malipo barani Afrika kama yale yaliyofanywa na kampuni ya dlocal Amerika kusini pamoja na AirWallex huko barani la Asia.

NALA imeendelea kufanya vizuri zaidi kwa miezi 12 iliyopita na kushuhudia idadi ya miamala inayochakatwa kwenye NALA ikiongezeka mara 34 zaidi, idadi ya Wafanyakazi ikiongezeka kutoka watu 7 hadi 100 huku idadi ya Wateja ikifikia Watu laki 5 na kuongeza Matawi kwenye nchi 21 za Ulaya.

Benjamin akiongea na millard ayo amesema yafuatayo “Uwekezaji huu wa Bilioni 106 utatuwezesha kuongeza huduma zetu za kifedha, yaani mbali na kutoa huduma za remittances (kutuma fedha kutoka ughaibuni kwenda nyumbani Afrika) tutatoa huduma mpya za malipo za kimataifa nje ya Afrika, tutatumia hii pesa kuboresha miundombinu ya mfumo wetu mpya wa malipo (uitwao Rafiki), kuboresha ubora na uharaka wa huduma za kifedha pamoja kupunguza gharama za miamala, NALA hatushiriki tu kwenye mabadiliko ya huduma za kifedha ila sisi ndio tunafanya hayo mabadiliko" #MillardAyoUPDATES

INASIKITISHA WALLAH
 
Ndio shida inapokujaga hapo, wazo lako unampa nani kwenye hii dunia isiyo na watu waaminifu.

Kuwa makini sana kutangaza mawazo yenye faida wengine bure bure au kukutana na watu bila ya mwanasheria wako au lutoowekea patent.
Kweli kabisa mkuu. Kwenye hilo wazo nililotoa kwa hiyo kampuni kubwa ya simu wala si uongo na kama naongopa mwenyezi Mungu ananiona. Na sikufaidika na hilo wazo na hata sina pa kuanzia.
 
Walimfaaanyia figisu ndio maana hq akaipeleka kenya. Tz kuna shida na ujima mwingi we fikiria mpaka leo hata paypal haipokei pesa tz. Kenya yani unaweza pokea pesa kwa njia nyingi kupitia safaricom.
Ila bot wameweka makufuli mengi eti wanazuia money laundering wakati london imejaa fedha ya ma oligarch, uswiss imejaa pesa ya viongozi wa afrika na wa asia
Mimi mwenyew siwezi anzisha kampuni ya tech. Nikaweka headquarters Tanzania. Ni Rwanda au kenya huko
 
Vijana wenye akili kubwa kama hao ni mwiba kwa watawala wengi wa Afrika. Kwa mtu yoyote mwenye akili kubwa Afrika sio sehemu sahihi ya kuishi. Yeye mwenyewe sio mjinga kuweka makao makuu ya kampuni yake uko Kenya hii ni kwa sababu anajua figisu za wanasiasa wa bongo ni mabingwa wa kupenda kuvuna ambapo hawajashiriki kupanda, kampuni yake angeweka Tanzania izo bilioni 100 Mwigulu angeshazitolea macho. Vijana wa aina ya mwijaku na Lucas Mwashambwa ndio wanahitajika zaidi na watawala wa Afrika
Kenya Kuna positive energy zaidi kuliko Tz thus kitambo sana wajanja top management wanaajiri Wakenya.
Pana wabongo wana mashamba ya vitunguu,parachichi nk wameajiri Wakenya wapo mbali sana kiuchumi.
Mtza amejaa negative energy zaidi
 
Kweli kabisa mkuu. Kwenye hilo wazo nililotoa kwa hiyo kampuni kubwa ya simu wala si uongo na kama naongopa mwenyezi Mungu ananiona. Na sikufaidika na hilo wazo na hata sina pa kuanzia.
Nakuamini 100%

Kupigwa sio kosa, Iła kurudia kupigwa ndio kosa.

Mawazo ya kuwapa hela wengine hakikisha unayatoa kwa njia sahihi, ambayo awafaidiki bure bure na mgongo wako.

Sina sababu ya kubisha ukishadhulima mara moja ni kosa (kama una ushahidi wa kudai haki yako) Iła usiruhusu wengine wachukue mawazo yako ya kutengeneza hela mara ya pili

Nakuwelewa sana sometimes ili ndoto zitimie unahitaji mtaalamu fulani, kazi ambayo inabidi wengine waifanyie kazi; lakini akili ya wazo ni lako. Ukienda kichwa kichwa hasa kwenye taasisi wanaiba wazo na kufaida nalo wao.
 
Back
Top Bottom