Kampuni ya mtandao wa simu wa Tigo acheni matangazo ya udhalilishaji

jerryempire

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
5,128
8,650
Nimekuwa ni mpenzi wa mtandao wa Tigo kwa muda wa miaka zaidi ya 18 sasa kutokana na huduma zao nzuri na nafuu

Kilichonifanya kuleta malalamiko yangu hasa kwa mamlaka husika ni utumiaji wa watu katika matangazo hasa katika mtindo wa udhalilishaji kama njia ya kufikisha matangazo yao

Leo wakati natoka na usafiri asubuhi nilibahatika kupita maeneo ya Karume na kumkuta kijana akiwa amebeba bango la mtandao wa Tigo huku akiwa amevaa ki boxer tu huku akiwa amepakwa mirangi mwili mzima bila bila kuvaa nguo yoyote nyingine

Wakati natoka kwenye mihangaiko yangu jioni wakati narudi nmemkuta yule kijana mwenye miaka takribani 26 akiwa amesimama pale pale ikionyesha kuwa ameshinda kutwa nzima juani na akiwa nusu mtupu huku akiwa na kibango cha mtandao wenu huku akiwa kituko mbele za watu kwa kulaani kitendo hicho,kwani ni kitendo cha udhalilishaji na unyanyasaji wa watu

Hivyo ningeziomba mamlaka hasa za haki za binadamu na Serikali kwa ujumla kutokulifumbia macho hili kwani siyo kampuni hiyo tu yenye tabia ya matangazo ya namna hyo bali ni makampuni mengi yanayofanya udhalilishaji huo lakini hawachukui hatua

jb
mwananchi huru

Screenshot_20190913-212827_Gallery.jpeg
Screenshot_20190913-212819_Gallery.jpeg
Screenshot_20190913-213029_Gallery.jpeg
 
MKUU HAKUNA UDHARIRISHAJI MBELE YA PESA.MAADAMU NI HALALI NA SHERIA HAIJAVUNJWA ACHA VIJANA WAPIGE PESA
 
Hata Mie nilikua natoka kinondoni naelekea gongo la mboto , nilipofika kigogo kona niliona mtu kama huyo kwa akili za haraka nilijua ni sanamu. Ila baada ya kucheki kwa utulivu nligundua ni mtu daaa! niliwaza sikupata jibu why tangazo liwe kwa namna ilee?
 
Back
Top Bottom