Kampuni ya MediaTek imetoa chip mpya

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,337
c2428816c020b3f2d081e5c8a9f605ec.png

Kampuni ya MediaTek imetoa chip mpya ambayo itakuwa inatumika katika simu kali za bei nafuu ili kushindana na soko la Qualcomm. MediaTek inafahamika sana kwa kutengeneza processor za simu za bei nafuu kama vile Tecno, Realme, Oppo, Infinix n.k.

Dimensity 9000 ni ubongo wa kwanza wa simu kutumia processor ya teknolojia ya 4nm.

✺ CPU yake ni 1X Arm Cortex-X2 @3GHz; 3x Arm Cortex-A710 @ 2.85GHz; na 4x Arm Cortex-A510 @ 1.8GHz.

✺ GPU: Arm Mali-G710 GPU na uwezo Raytracing SDK kwa kutumia Vulkan ya Android.

✺ Display yake FHD+ 180Hz

✺ Akili Bandia yake ni 5th Generation ya APU

✺ Inaweza kurekodi video ya 4K HDR katika lens tatu kwa pamoja, ni nzuri katika picha za Night Mode, inakubali kamera ya 320MP.

✺ Inakubali 5G, Bluetooth 5.3, Wi-Fi 6E, download speed ni 7GB kwa sekunde na inatumia teknolojia ya TSMC 4nm class process.

Simu ya kanza kutumia chip hii itatoka mwanzo wa mwaka 2022.
 
Dimensity series ni soc nzuri za mediatek wanazotengeneza Kwa sasa.
Warekebishe kwenye swala long term support vinginevyo Qualcomm ataendelea kutawala sana.
 
Back
Top Bottom