Kampuni ya Landfall Universe Limited yapitisha Sh 1.4 trilioni haramu

Mkuu nitake radhi, Lissu sio Boss wangu na sijamtaja popote kwenye bandiko langu, nimevutiwa na uwezo wa mleta mada kwenye kufanya uchunguzi ndio nikamuomba atusaidie kutafuta taarifa za Mayanga Construction, unadhani mleta mada angeridhika na taarifa zilizopo Brela angeweza kufichua haya yote?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana ndugu, ila hiyo kampuni ipo tanzania tofauti naa ile ya mleta mada mpaka sasa haijulikani kwani kila sehemu hakuna taarifa zake ila mayanga ipo na inapatikana.

Na kwa kuwa Lisu ndo amekuwa akiishutumu basi wale wenye wasiwasi wanatakiwa kuja na jambo kuwa hiyo kampuni ni halali au nayo ni hewa. Na kama ni halali basi watwambie je kwa kuwa kampuni hiyo ina ukaribu na raisi basi kisheria haitakiwi kupata tenda hapa nchini hadi raisi huyo atoke madarakani?

Lakini kwa kumuuliza lisu tu ni kwamba. Kuna kampuni ilichukuwa tenda pale chadema na kumekuwa na taarifa kuwa inalipwa milioni 60 kila mwezi na ni ya shemeji yake na mbowe.

Je, anasemaje kuhusu hizo shutuma?

Ameshawahi kuhoji hilo au kwa kuwa inawahusu basi hawezi kuhoji?
 
Tunapoteza muda na fedha kufukua makaburi yasiyolipa. Tulishapigwa sasa ni kuzuia tusipigwe tena sio huu umbea.
Kama kawaida yenu, TUKISHAPIGWA MNATAKA YAACHWE! Kwa mtazamo huu, hatuna sababu ya kuwa na mahakama, MAANA ZINATOA HUKUMU KWA YALIYOKWISHA TOKEA.

Na siku zote huoni mtazamo wa majizi.... yakishapiga yanataka yaachwe simply because yameshatokea... UJINGA MTUPU
 
michezo ya ki spy iyo.....

ili kutekeleza dili la namna hiyo sio rahisi kama mnavyodhan maana yake lingehusisha watu wengi na ikshakua watu wengi then usalama unakua mdogo (iko siku ingelik


Kama nmeelewa maana yake hiyo pesa inatumwa hk tokea tz?
*kuna wàkwepa kodi
*kuna watakatisha fedha
*kuna michezo ya ki spy
*kuna biashara ya nchi na nchi(yakificho)
*pia wachina sio watu wazuri kwe madini jpm kidigo kawapunguza
*au hata north Korea wanatumia tz kusafirisha pesa zao walzochuma africa toka biashara halili au sizo halali maana wanavikwazo hawa...


😂😂sina uhakika na niliyo sema kwa sio mm
 
Kusajiliwa kwa kitambulisho cha NIDA ndiyo nini..!? Hujawahi ona mwanamke namba yake ina jina la kiume au kinyume chake..!? Kama namba ina kazi maalumu inawezanpewa jina lolote...
 
Duh! Mafisadi katika ubora wao. Tusishangae kusikia kuna walio ndani ya Serikali wahusika wa huu upigaji.

Duuh, inatisha sana hii..

Ni fedha nyingi sana hizi halafu zinapita kwenye mabenki yetu kiharamu kwa miaka takribani mitatu pasipo mamlaka zetu zenye jukumu hili kugundua....

Shaka yako ni very genuine, kuwa baadhi ya maafisa wakubwa ndani ya serikali ya Tanzania ni washiriki wa ufisadi huu....

Hawa STANCHARD BANK wanajua kila kitu, tusidanganyane...!

Kwa hakika kukiwa na "seriousness" kulichunguza jambo hili na benki husika iliyopitisha fedha hizi ikibanwa vizuri watawasema wahusika wa huu uharamu....!!

Likipita hili kimya kimya, tujue kabisa "vigogo wakubwa" wenye mamlaka makubwa serikalini wanahusika...

Mambo kama haya ndiyo yanayoleta UGUMU wa kuiondoa serikali ya CCM ya madarakani...

Kwa sababu, licha tu ya kwamba CCM inatakiwa ishindwe uchaguzi wa mwaka huu katika SANDUKU LA KURA, lakini pia haya ni mapambano makali kati ya HAKI na kundi kubwa na hatari linaloitumia DOLA kufanya ugaidi huu wa kiuchumi...

Na kulifuta kundi hili inahitajika nguvu ya ziada kubwa zaidi ya kutegemea BALLOT BOX...!!

Yaani mimi picha hii inanipa hisia kuwa, CCM hawawezi kuachia nchi iingozwe na chama na watu wengine kupitia SANDUKU LA KURA....

HAKUNA, HAKUNA, HAKUNA..!!!
 

Mlungula unamfanya anayesajili kukubali jina lolote lile. Sasa huyo Mchina kuwa na kitambulisho cha NIDA kwani yeye ni Mtanzania?
 
Magufuli akiwashughulikia watu kama hawa, chandimu wanapinga!
 
Kusajiliwa kwa kitambulisho cha NIDA ndiyo nini..!? Hujawahi ona mwanamke namba yake ina jina la kiume au kinyume chake..!? Kama namba ina kazi maalumu inawezanpewa jina lolote...
Asante sana Mkuu, kwa kunifungua macho. Hapa sasa ndiyo tunaanza kufungua box ili tuone kilichomo ndani.
 
Mlungula unamfanya anayesajili kukubali jina lolote lile. Sasa huyo Mchina kuwa na kitambulisho cha NIDA kwani yeye ni Mtanzania?
Aisee, kweli niliipitia kwa haraka taarifa hii. Hata hivyo, Mkuu tuna watanzania wenye asili ya China, bahati mbaya sana kwa hapa tunawaita wa Wachina. Nao wanapewa vitambulisho na NIDA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…