Kampuni ya Israel inayoweza kudukua simu yeyote

Kampuni ya Israel inayoweza kudukua simu yeyote

Bakulutu

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2011
Posts
2,596
Reaction score
1,865
1474896521269.jpg

Kampuni moja ya Israel inayowasaidia polisi kudukua simu za washukiwa wa uhalifu nchini Israel Cellebrite, imesema kuwa inaweza kudukua simu yoyote aina ya smartphone.

Kampuni hiyo iligonga vichwa vya habari mapema mwaka huu wakati ilipodaiwa kuwasaidia maafisa wa ujasusi nchini Marekani FBI kudukua simu aina ya Iphone iliotumiwa na muuaji wa San Bernardino.

Cellebrite sasa imeieleza BBC kwamba inaweza kuingia katika simu yoyote ya smartphone.

Lakini imekataa kusema iwapo inasambaza teknolojia hiyo kwa serikali za kiimla.

Wiki iliopita kampuni hiyo ilialikwa katika hoteli ambayo maafisa wa polisi kutoka kote nchini Uingereza walionyeshwa vifaa na programu zinazoweza kutoa data ya simu za wahalifu
Source: BBC
 
tuishi leo ila maisha kama ya jana. matumizi ya barua
matarishi(messenger)
n.k

hapo usiri utakuwa wa kutosha.
 
Hao wajue tu kudukua,
Soon tutawafikia ngoja viwanda vyetu vikamilike tu[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji16]
 
..safi sana
Genda Heka linakuona
 
tuishi leo ila maisha kama ya jana. matumizi ya barua
matarishi(messenger)
n.k

hapo usiri utakuwa wa kutosha.
[emoji16] [emoji16]

MPE messenger siku moja barua ya kumwachisha kazi(messenger huyo) ampelekee HR manager atie sahihi....

Subiri sana uone kama itafika
 
[emoji16] [emoji16]

MPE messenger siku moja barua ya kumwachisha kazi(messenger huyo) ampelekee HR manager atie sahihi....

Subiri sana uone kama itafika
ahahaha hao ma HR barua zao wanazikuta kwa makatibu muhtasi asubuhi na mapemaaa

kabla hajaingia ofisini kwake anaambiwa bosi kuna. barua yako hapa.....
 
tuishi leo ila maisha kama ya jana. matumizi ya barua
matarishi(messenger)
n.k

hapo usiri utakuwa wa kutosha.
Hata barua mkuu...njiani si inafunguliwa tuu....kama unatafuta taatifa zako.....
Labda umtume mtu moja kwa moja ....kama alivyokuwa akifanya osama....
 
Hata barua mkuu...njiani si inafunguliwa tuu....kama unatafuta taatifa zako.....
Labda umtume mtu moja kwa moja ....kama alivyokuwa akifanya osama....
ndio maana nimesema tarishi
 
Back
Top Bottom