Fastjet Shikamoo! Kwa kweli Tanzania hii inahitaji mabadiliko makubwa sana kwenye sekta ya usafiri wa anga. Nadhani Fastjet bila kutazamwa na serikali wamejiwekea uzio wa kutokamatika kisheria. Jana usiku saa 3:15 tumeruka kutoka JNIA kuelekea KIA na tulipokaribia kutua control tower wakaripoti kuwa kuna hitilafu ya umeme hivyo hatuwezi kutua kwa sababu taa za runway zimezima. Tukarudishwa JNIA..tukaambiwa ndege inajaza mafuta turudi KIA kwa sababu tatizo limekwisha.
Wakati tunashangaashangaa tunashushwa kwenye ndege na kuambiwa kuwa masaa ya crew yamekwisha hivyo tusingeweza kuruka tena. Na wanasema ndege iliyopo ni ya leo saa 5 asubuhi. Wamekataa kutoa nafasi kwa ndege ya saa 12 asubuhi KIA - Jomo Kenyatta ambayo inaweza kubeba abiri wote tulioshindwa kutua KIA usiku wa jana. Maamuzi yote yanafanywa London,...tumepiga simu London kwa simu zetu na kueleza ugumu uliopo kwetu abiria na udhalili wa mazingira ya airport kama mnavyoona kwenye picha akina mama wamelala kwenye conveyor belt baada ya uchovu kuwazidia.
Jitihada zetu zimeishaia patupu na ukweli wenzetu wa ulaya hawaoni kama sisi huku unyanini tunastahili kupata treatment kama watu wa huko kwako. Tumepata emergency lakini wao wanaichukulia kama kitu ya kawaida sana. Hapa kuna watoto wadogo..wagonjwa...wamama wajawazito...na watu wenye mahitaji maalum. Fastjet kwa kujidai wao ni "low cost" airline hawatoi malazi, nauli za kurudi majumbani, chakula wala viburudisho panapotokea kuahirishwa kwa safari. Nimemua nikae hapa na wenzangu kama 60 nione mwisho wake itakuwaje.
Wanachokifanya Fastjet ni kinyume na Conventions na Protocol zinazohusu usafiri wa anga pamoja na sheria yetu ya ndani..masharti yao kwenye mtandao ambayo ni sehemu ya ticket yanamkandamiza sana abiria bila kujali sheria za ndani na kimataifa wa hali halisi kwa wakati husika..hiki kiburi wamekipata wapi? Nataka nikirejea nipeleke petition ya kufanya yafuatayo: moja ni kupata declaration kuwa Fastjet haistahili kuwa kwenye category ya "low cost airlines " na pili ilazimishwe kutekeleza matakwa ya sheria za kitaifa na kimataifa za uendeshaji wa huduma za usafiri wa anga na wawajibike kisheria kwa mteja kwa wanavyofanya Precision Air na ATCL...nadhani katika Afrika ni Tanzania peke yake ambapo Fastjet inaendeshwa kama local flight na hizo local flights nasikia zina faida zaidi ya maradufu kulinganishwa na international flights.
Nchi yetu kwa nini tuteseke? Au kuna watu wanafurahia hawa akina Fastjet kuendelea kuiibia ATCL soko la ndani kwa hila na kuwahi ticket mapema kwa 200,000/= na kulipa 700,000/= siku ya safari au kwa kubadili siku au muda wa kusafiri?. Sitasubiri raisi awatumbue....watanikuta FCT...#pingaukolonina unyonyaji#