Kampuni ya BM coach sasa mnaharibu, kulikoni?

Kampuni ya BM coach sasa mnaharibu, kulikoni?

NGOMEKONGWE2021

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2021
Posts
616
Reaction score
1,253
Hii kampuni ilianza vizuri hasa safari za Dom-Dar-Dom....wakawa na huduma nzuri sana....wakapata wateja wengi ambao walihama kutoka makampuni mengine makongwe kama Shabiby, ABC etc..kila kitu kilikuwa on time...Sasa wamevimba kichwa ...Yaani hawana ratiba inayoeleweka kabisa..

Yaani siku hizi kuambiwa gari muda wa kuondoka umesogezwa mbele(gari itachelewa) au safari ya jioni haipo hivyo wenye tiketi wapande gari ya mapema zaidi (gari itawahi) ni kawaida kabisa....Siku hizi si ajabu ukakaa ukisubiri gari pale ofisini kwao Dsm au Dom mnakuwa kama vifaranga vya kuku vimeloa maji na gari haionekani, muda unakwenda ......na wafanyakazi wao wapo wapo tu hakuna anayetoa updates zozote.....hata mkiwa njiani dereva anaweza kusimama ghafla, barabarani bila kuwaeleza abiria nini kinachendelea, mnakaa nusu saa au lisaa limoja.

Kwa ufupi wamekuwa na kiburi sana sana......wiki iliyopita nikiwa Dom kwenda Dar ilkuwa hivyo hivyo kila mtu analalamika kwamba sasa amechoka na anahamia mabasi mengine ..kichekesho wakati wakurudi nikiwa pale Shekilango ofisini kwao pia abiria walikuwa wanalalamika hivyo hivyo.....yaani wapo very dis-organised....niliwahi kumuuliza mmoja wa wafanyakazi wake akaniambia wanadhani wamelogwa na Shabiby manake hata wao hawajielewi ,wanasema inaonekana amewapania sana kwani wanamuharibia biashara...sasa sijui hii imekaaje wadau....Kama kuna wahusika humu watuambie kulikoni?
 
Yaan unasema wakati wa kwenda Dar ulipata sana shida na watu walikuwa wanalalamika kuwa huduma ni mbovu, ila wakati wa kurudi ukaenda tena kwenye kampuni hiyo hiyo iliyokupa shida. Tukisema ww ni muongo upo hapa kuchafua biashara ya watu tutakuwa tumekosea!???
 
Apige juju wafanyakazi wakiona lami tu wanaendesha
 
Zinakuja nyingine mpya
20220428_195225.jpg
 
Ujumbe Utamkuta Boss Wao Nadhani Yupo Morogoro Sijui Vile
 
Natumia BM tangu ilivyoanza route ya Dar - Moro, na kwa sasa naitumia sana Dar - Dom sijaona shida unayosema nimeitumia wiki mbili zilizopita kwenda na kurudi
Route ya Arusha - Dar nayo naitumia sana

Huyu mangi anaijua Fitna ya hii biashara, kuweza kumtingisha Abood kwenye route ya Dar Moro sio kazi ndogo, hakuna tajiri alikuwa anathubutu hiyo route japo ina faida sana.

Akitaka kukamata route anafanya kama ndege, yani muda wa kuondoka ukiwa ni labda saa 3,ikifika 3 kamili chuma inang'oa hata kama ina abiria 20.
Niliwahi kutoka Moshi na ile luxury ikiwa na abiria nusu.

Sasa nafikiri Shabibby ameanza ku feel ule utawala na hadhi yake unatikiswa na BM kwahiyo Fitna lazima ziwe nyingi
 
Back
Top Bottom