Kampuni ya Apple imesitisha kuuza simu za iPhone na bidhaa zake nyingine nchini Urusi na kujiunga na Kampuni nyingine mbalimbali ambazo zimetangaza kujiondoa Urusi baada ya kuivamia kijeshi Ukraine.
Wafanyabiashara wengine wakubwa wa teknolojia kama Google na Twitter pia wamepunguza biashara zao nchini Urusi ‘tunaungana na wote wanaotaka amani duniani’ imeeleza taarifa ya Apple.
Pamoja na kusitisha uuzaji wa bidhaa, Apple inasema duka lake la programu za simu linazuia upakuaji wa RT News na Sputnik News kutoka nje ya Urusi zikiituhumu mitandao hiyo kuwa inarusha habari za propaganda kutokea Ofisi za Serikali ya Urusi.
Apple pia imesitisha kutuma location za moja kwa moja kwenye ramani za Apple nchini Ukraine kama hatua ya usalama, sawa na hatua ambayo tayari Google imechukua.
Apple nyambafu sana wakati dunia inashughudia maangamizi Itaq syria Linya na Afghanstan walikua wanaona ni sawa?
Kampuni ya Apple imesitisha kuuza simu za iPhone na bidhaa zake nyingine nchini Urusi na kujiunga na Kampuni nyingine mbalimbali ambazo zimetangaza kujiondoa Urusi baada ya kuivamia kijeshi Ukraine...
Hahaha sasa mbona kama Pakistan katafuta upenyo wa kutolipa madeni?Putin anaendelea kupata mapigo kote, na Warusi wengi ukiingia kwenye mitandao yao wamenza kumchukia na sio muda mrefu watamgeuka hali ikizidi kuwa ngumu.
Dunia iendelee kumpa vikwazo vya kila aina. Pakistan alishasema hatomlipa madeni yake, asusiwe na wote....
Hahaha sasa mbona kama Pakistan katafuta upenyo wa kutolipa madeni?
Hivi hadi sasa kuna kauli yoyote kutoka kwa putin
ngoja tusubiri liwalo na liwe
Mkuu vikwazo vinapiga kote kote, aliewekewa anaumia na alieweka anaumia.Russia hataweza kustahimili haya mapigo na mwisho wa siku ataomba poo kwani hakuna nchi inayoweza kuishi kama kisiwa. Wananchi wa Russia tayari wameshaanza kapanga foleni kununua bidhaa kama ilivyokuwa wakati wa USSR. Ruble imeshapoteza asilimia 30 ya thamani yake.
... But not on equal footing, on ratio it's 75/25%.Mkuu vikwazo vinapiga kote kote, aliewekewa anaumia na alieweka anaumia.
Mkuu Apple ni kampuni kutoka nchi gani? Je kuna kampuni yoyote ya kutoka Urusi iliyoacha kuiuzia Urusi bidhaa yake kwa sababu imeivamia Ukraine? Kama jibu ni hapana basi umeshapata jibu la swali lako kama Apple walikuwa likizo ama lahWakati marekani ilipovamia Sirya Libya Afaghanistani Iraq hao Apple walikuwa likizo?
Russia inajitosheleza kwa kila kitu acheni kuweweseka
Mkuu hata Tanzania mnaweza kumwekea Marekani vikwazo, yeye hazuii nchi yoyote kumwekea vikwazo. Wew weka kama unao uwezo wa kuishi bila yeye.Wasiuze tu kwani wao ndio MUNGU pumbavu sana. Marekani anajiona mungu sana fala huyu. Yeye kuwawekea wenzake vikwazo ila sio yeye kuwekewa vikwazo.
Sent using Jamii Forums mobile app