LICHADI
JF-Expert Member
- Feb 4, 2015
- 4,418
- 12,236
Mwezi uliopita kampuni ya uzalishaji ndege yenye makao yake makuu france airbus, ilitangaza kuwa ifikapo mwaka 2021 itasitisha rasmi uzalishaji wa ndege zake kubwa za A380, walisema kwa masikitiko makubwa wanalazimika kusitisha uzalishaji wa ndege hizo kwa kuwa zimekosa order na wameona ndege ndogo ndizo zenye order nyingi zaidi
Taarifa zaidi zinadai kuwa mteja wao mkuu ambae alikuwa ni Fly Emirates alipunguza order ya uzalishaji wa ndege hizo 53 alizoziorder mwanzo hadi kufikia 14, kampuni hiyo imesema kuwa baada ya kumaliza kutengeneza ndege hizo, kuanzia 2021 watasitisha utengenezaji wa ndege hizo.
View attachment 1039375
Pia imekuwa ni masikitiko makubwa kwa maelfu wafanyakazi walioajiriwa kwa ajili ya program ya utengenezaji wa ndege hizo wakihofia kuwa ajira zao zinaweza kuwa hatiani, lakini kampuni ya Airbus imewahakikishia kuwa kusitishwa kwa uzalishaji wa ndege hizo hakutoathiri ajira zao, Airbus imeeleza kuwa wataamishwa katika vitengo vingine vya uzalishaji ndege ndogo
Sent using Jamii Forums mobile app