Kampuni inakufaje? Insolvency and Bankruptcy

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,495
5,529
Habari,

Leo natka nilete mada ndogo ndani ya mada ndogo

Katika media tumewahi kukutana na maneno Insolvent na Bankruptcy. Pia kama ni mfanya biashara umewahi kusikia pia neno KUFILISIKA au KUFILISIWA au KUFILISI. Umewahi pia kusikia mali za kampuni zikipigwa mnada au kampuni kuwekwa chini ya "Receivership". Unapokuwa mmiliki wa kampuni unapaswa kufahamu kwamba kampuni inakulinda wewe dhidi ya kufilisika au kufilisiwa lakini haijilindi yemyewe dhidi ya kufilisiwa. Unapofanya biashara kama mtu binafsi (Sole Proprietor) huwa ni tofauti. Utafilisiwa wewe na utafilisiwa kweli kweli.

Kampuni ambayo ina ukomo wa hisa au biashara yoyote ile huwa inakuwa na madeni ambayo huwa katika taarifa huitwa Liabilities. Liabilities zinaweza kuwa ni madeni, mikopo ambayo inapaswa kulipwa na kampuni. Kampuni inaposhindwa kulipa madeni yake kufika siku 90 inakuwa katika hatari ya kutangazwa muflisi. Kwa mfano kama kampuni/biashara inapitisha miezi mitatu bila kulipa wafanyakazi wake mishahara au kulipa watoa huduma wengine inaweza kufilisiwa.

Vile vile kampuni inapokuwa na kiwango kikubwa cha madeni kuliko Mali inazomiliki nayo ni hatari. Ndio maana wahasibu katika taarifa yao huweka neno "Going Concern in the foreseeable future" ambapo huwa wanachotka kusema ni kwamba madeni ambayo kampuni inadaiwa ni stahimilivu. Sasa inapotokea madeni yanazidi uwezo wa kampuni kuyalipa au yanaziida thamani ya Assets za kampuni tunasema kwamba kampuni ni insolvent. Kuna njia nyingi sana za kujikwamua katika hali kama hio ambapo inategemea na kampuni yenyewe.

Kuna kampuni ambazo zikifikia hatua hii hukaa mezani na wadeni wake ni kufanya mabadiliko (Restructuring) ikiwamo kupunguza gharama za uendeshaji, kubadilisha deni kuwa hisa, kuuza deni kwa kampuni nyingine, kupunguza wafanyakazi, kupunguza mishahara au kuingiza wawekezaji wapya. Hili linafanyika katika kampuni za aina zote zikiwamo binafsi na hata za umma.

Kampuni nyingi zinapoanzishwa wamiliki na wakurugenzi huingia katika mtego wa kutokutunza kumbukumbu vizuri na kuchanganya shughuli binafsi na za kampuni. Matokeo yake ni kwama ama hujikuta hawajui ukomo wa kampuni ni upi au mtindo wao wa uendeshaji huzuia kampuni zao kukua kwa sababu wanaizuia kukua. Unapoamua kumiliki kampuni ni lazima uwe tayari kuiruhusu kampuni yako ikue. Kuna hatua inafika lazima uamue kuhakikisha kwamba kila unachokifanya kinaipa kampuni nafasi ya kujenga asset base yake. Lakini pia ni lazima uhakikisha kwamba kampuni yako wakati wote inakuwa na asset base zinazoweza kulipa madeni yake. Sio vyema kuwa na kampuni ambayo inataka tender ya bilion 1 lakini asset base yake ni ndogo kama hauna mkakati mbadala na wa kueleweka.

Karibu tuendelee kujadili masuala ya kisheria yanayohusu ufilisi wa makampuni na ni wakati gani kampuni inapaswa kufilisiwa kwa hiari na ni wakati gani inafilisiwa kwa lazima.

Karibu
 
Eti ukienda mahakamani kutangaza umefilisika, wadeni wako hawaruhusiwi kukudai eee?
 
Eti ukienda mahakamani kutangaza umefilisika, wadeni wako hawaruhusiwi kukudai eee?
Watakudai ila kwa namna amayo wewe unakuwa na Control kiasi na serikali itakusaidia kuhakikisha haukufi
 
Back
Top Bottom