Kampeni za udiwani Songea, Hebu cheki jinsi Abwao alivyofunika

Dullo

JF-Expert Member
Oct 24, 2009
251
64
3.JPG

Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Songea Peter Mboya akiwasalimia wananchi wa Kata ya Lizaboni wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya sokoni wa kumsaka Diwani wa Kata hiyo ambapo chama hicho kimemsimamisha Alanus Mlongo
8.JPG

Mwenyekiti wa Jimbo la Songea ambaye ni Diwani wa Kata ya Majengo Idd Abdalah akizungumza kwenye mkutano huo
SAM_0711.JPG

Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Ruvuma Joseph Fuime akinada sera za chama hicho kwenye kampeni za uchaguzi zinazoendelea kata ya Lizaboni
SAM_0718.JPG

Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Songea Peter Mboya, mgombea wa Udiwani wa Kata ya Lizaboni Alanus Mlongo, Mbunge wa Vitimaalum na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema Chiku Abwalo. Katibu wa Chadema Mkoa wa Ruvuma Dorphini Ghazia wakimsikiliza kwa umakini Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Ruvuma Joseph Fuime hayupo pichani wakati wa mkutano wa kampeni zinazoendelea kwenye Kata ya Lizaboni

SAM_0758.JPG

Wananchi wakisikiliza viongozi wakati wa mkutano wa kampeni wa Chadema Kata ya Lizaboni uliofanyika kwenye viwanja vya Sokoni

2.JPG

Mbunge wa Vitimaalum na Mjumbe wa Kamati kuu ya Chadema Taifa Chiku Abwalo akiwahutubia wananchi wa Kata ya Lizaboni waliofika kwenye viwanja vya Sokoni kusikiliza mkutano huo.

Picha zote kwa hisani ya Stephano Mango, Songea
 
Moto huu wa cdm wa kuuzima kwa hapa tza hayupo ,aliyesema cdm ni chama cha msimu nadhani jibu analipata sasa.
 
Big up Mama yetu Mhe Chiku Abwao, salam za ukombozi toka CHADEMA zifike kwa kila mwananchi katika kila kijiji kote Bara na Visiwani.

Hakuna kulala mpaka ukombozi toka kwa MAFISADI upatikane. Vijana wenzetu hapo Songea pamoja na BAVICHA, kazi iendelee tena kwa ushirikiano mkubwa ajabu mpaka MAFISADI waduwazwe!!
 
shida hawana Vitambulisho vya kupiga kura,hii ndio shida peekee.

Plan ahead to get ahead..Mkuu 2015 wote watakuwa navyo...tusikatishwe tamaa na matokeo ya hizi chaguzi za sasa hivi...elimu ya uraia ni muhimu sana kwa sasa pengine kuliko kutwaa jimbo au kata kwa kipindi hiki.
 
Hii inatia moyo, taratibu tunakaribia kwenye ukombozi wa kweli wa nchi hii.
 
Moto huu wa cdm wa kuuzima kwa hapa tza hayupo ,aliyesema cdm ni chama cha msimu nadhani jibu analipata sasa.

Tatizo huu moto wa CHADEMA ni kama wa karatatasi unaowaka kwa kasi na baada ya muda mfupi unazimika. Hii ina maana kuna mwamko mkubwa wa watu kwenda kuwasikiliza viongozi mbalimbali wa CHADEMA wanapohutubia kwenye majukwaa na wanasisimka kwelikweli wanaposikia maneno matamu ya wapiga kampeni. Lakini inapofika wakati wa kupiga kura wanakuwa wameshapoa na hata hamu ya kwenda kupiga kura zenyewe inakuwa haipo. Upande wa CCM ina wapiga kura ambao wala hawaendi kwenye mikutano ya kampeni lakini siku ya kupiga kura wanakuwa wa kwanza vituoni kwa ajili ya kupiga kura kwa mtu aliyeteuliwa na chama chao kuwa mgombea. Yaani wapiga kura wa CCM wanapigia kura chama kwa mazoea na hawahitaji kusisimuliwa kwa hotuba zilizojaa maneno matamu matamu. Ni mtazamo wangu tu.
 
Hao wanaoukataa ukweli watabaki hivyo hivyo tu, maana kama mtu anabisha hata ushahidi wa picha basi ni hatari
 
Kwa kweli Mama huyu Chiku Abwao ni mchapa kazi hakuna mfano wake.

Laiti Ukuu wa Wilaya isingekua ni miliki, haki na hifadhi ya Wana-CCM peke yao, huyu mama anazo dalili zote za kuweza kusaidia taifa kuhamasisha wananchi zaidi na zaidi kujiletea maendeleo kuliko hawa wengine ambao kwao Ukuu wa Wilaya ni ufalme tu wa mtu kujikweza nayo bila tija kwa taifa.
 
Tatizo huu moto wa CHADEMA ni kama wa karatatasi unaowaka kwa kasi na baada ya muda mfupi unazimika. Hii ina maana kuna mwamko mkubwa wa watu kwenda kuwasikiliza viongozi mbalimbali wa CHADEMA wanapohutubia kwenye majukwaa na wanasisimka kwelikweli wanaposikia maneno matamu ya wapiga kampeni. Lakini inapofika wakati wa kupiga kura wanakuwa wameshapoa na hata hamu ya kwenda kupiga kura zenyewe inakuwa haipo. Upande wa CCM ina wapiga kura ambao wala hawaendi kwenye mikutano ya kampeni lakini siku ya kupiga kura wanakuwa wa kwanza vituoni kwa ajili ya kupiga kura kwa mtu aliyeteuliwa na chama chao kuwa mgombea. Yaani wapiga kura wa CCM wanapigia kura chama kwa mazoea na hawahitaji kusisimuliwa kwa hotuba zilizojaa maneno matamu matamu. Ni mtazamo wangu tu.
CCM ni wezi wa kura full stop!
 
tazama hii halafu linganisha na mtazamo wako
igunga
2010 kura o
2011 kura 23,000 .........halafu tume ya uchaguzi na kila kitu ni cha ccm piga picha 2015 nakura za ccm zimepungua

Back
Top Bottom