Kampeni za Uchaguzi zaanza kwa kasi Rwanda..

Kampeni za Uchaguzi zaanza kwa kasi Rwanda..

Interest

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2015
Posts
3,434
Reaction score
7,096
Kampeni za wagombea Urais watatu zimeanza rasmi leo nchini humo ambapo kura zitapigwa kuanzia tarehe 5 Agosti mwaka huu..

Rais Paul Kagame naye amejitosa kuwania nafasi hiyo kwa mara nyingine tena na kwa awamu hii uchaguzi huu umeonakana kuwa na upinzani mkali ukilinganisha na kipindi kilichopita.

Wagombea pekee wanaogombea urais mwaka huu ni Paul Kagame wa chama cha Rwanda Patriotic Front (RPF-Inkotanyi); Frank Habineza wa Democratic Green Party of Rwanda na mgombea binafsi, Philippe Mpayimana.

index.jpeg
 
Kuna mazuri mengi sana Paul Kagame Amefanya kwa mkono wa chuma ikwa na pamoja na kuleta utulivu nchini Rwanda - hongera sana.
Hata hivyo kanuni za maisha zinaonesha kuwa kadri mtu anapokaa Madarakani muda mrefu ndivyo anavyokosa mvuto, kukosa maono, kukosa mbinu bora za kiutawala , kutumia nguvu nyingi ili akubaliwe watu na kutengeneza maadui wengi. Mwishowe mwenendo huo huondoa mazuri yote ambayo huyo mtu aliyafanya akiwa kama Kiongozi huko nyuma.
Hivyo ili Paul Kagame abakie na hayo mema aliyoyafanya huko nyuma , ni vyema akaongoza mhula huu tu. Baada ya hapo awachie na wengine vinginevyo atachafua kumbukumbu zake nzuri za nyuma. Atazame alama za nyakati.
 
Chama kikuu cha Upinzani kinaunga Mkono Serikal ya Paul Kagame! Hiyo ndo Africa
 
Wanaigiza... kodi ya wananchi inapotea wakati raisi ni Kagame

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom