Elections 2010 Kampeni za CCM

rendezvous

Member
Nov 23, 2009
18
0
Habarini bandugu, nilipenda kujua kitu kimoja, juzi siku ya jumapili nilikuwa maeneo ya mwananyamala kituoni nasubiri daladala kuelekea stesheni nikaona vijana wadogo wako kikundi kama 30 hivi wana mnadi mgombea wa kinondoni kupitia tiketi ya CCM. Kwa umri niliowaona sidhani kama alikuwepo aliyevuka miaka 18 na walikuwa wanaonekana kulewa na walikuwa wanapiga ngoma na kucheza ovyo barabarani.

Je inaruhusiwa kwa watoto kuchukuliwa na kunadi wagombea ??. kwa taarifa niliyodekezwa na jamaa wa pale kituoni kaniambia kuwa hao ni watoto wamechukuliwa kutoka kwenye vituo vya kulelea watoto yatima na wengine ni watoto wa mtaani. Wamepewa hela shilingi 5,000 na kuvalishwa tshirt za CCM.

Sasa hayo ndio malezi jamani. Tunaelekea wapi ???
 
Back
Top Bottom