Kampeni ya Usafi Dar es Salaam Yashindwa

Kichakoro

JF-Expert Member
Sep 10, 2008
3,302
6,115
Hakuna anependa uchafu awe masikini au tajiri, ila kukosekana kwa mpango maalumu kwenye eneo husika mara nyingi huwa ni chanzo cha uchafu maana kila mmoja anategemea mwenzake afanye na hivyo kutokufanyika na maeneo yetu kuwa machafu.

Ndio maana kwenye nyumba za kupanga tunamoishi kama hakuna utaratibu wa usafi eneo husika huwa chafu (watu huishia kufanya usafi ndani kwao na kuacha).

Nilipoona Kampeni ya ufanyaji usafi imeanzishwa Dar es salaam nilifurahi kwani niliona sasa tutakuwa na mfumo wa usafi kwenye maeneo yetu kila mara na kufanya jiji lionekane safi kwa masikini na kwa matajiri.

Hata hivyo nilipata wasiwasi baada ya kuona ile kampeni imefanywa ni mtu badala ya wanajamii. alikua akisifiwa kiongozi asiyetaka uchafu badala ya kuielekeza namna jamii inaweza kuandaa na kufanya usafi kwenye maeneo husika (hili limeondoa umiliki wa kampeni yenyewe kutoka kwa watu kwenda kwa mtu yaani kiongozi). kampeni kama hii ilipaswa kuwekeza kwa watu zaidi ya kiongozi ili kuweka umiliki kwa watu husika. Matokeo yake watu wamekosa umiliki morali imepotea kidogo kidogo tunaanza kurudi kwenye uchafu hata kile kidogo kilichoanza naona kinakufa.

Pili siku ya uzinduzi wa kampeni yenyewe nilifikifiri viongozi wa kampeni ile wangeweka nguvu nyingi kwenye maeneo machafu zaidi (hasa yaliyokumbwa na kipindupindu, masoko machafu n.k) badala yake viongozi hao walienda zaidi sehemu maarufu wakaacha sehemu zinazojulikana kuwa chafu na hata kusababisha kipindupindu. hii nayo imewafanya kufikiri wao sio wachafu kiivyo ama kampeni ile iliwahusu zaidi watu wa masaki, upanga, kinodnoni n.k

Tatu hakukuwa na ushirikishwaji wa kutosha wa viongozi wa mitaa, na kamati za mazingira kuleta kampeni ile kwa watu wa chini kabisa. Huku ndiko kwenye wachafuzi na wasafishaji hivyo wangepewa hamasa hiyo, wangewekeza zaidi huko kuliko kwenye radio na TV leo hii tungeona matokeo lakini hakuna wachafuzi na wasafishaji wameendelea kusubiriana nani afanye usafi.

Nini kifanyike

kwanza kuanza kampeni upya ili kuhamasiaha jamii na sio kusifia viongozi wanaopenda usafi ikiwezekana kampani hiyo ifuate utaratibu huo hapo chini

pili mamlaka zitoe waraka uanishe kila mtaa ufanye kikao cha dharura jumamosi ya kwanza ya mwezi wateue uongozi katika mtaa na sheria ndogo ndogo za usafi mfumo wa usafi kwenye mtaa wote (majumbani na sehemu za umma). Jumamosi pili serikali ya mtaa ikae kikao kuawabaini viongozi wa mitaa na kupitisha sheria ndogo ndogo za serikali za mtaa. wiki ya tatu kata kupitisha maazimio ya huku chini.

Baada ya hapo wiki ya nne utekelezaji unaanza usafi kwenye mitaa yetu, public places, na ikibidi uwe endelevu kila jumamosi na tathmini zifanyike kila mtaa kila jumamosi. viongozi wa serikali za kata na mtaa wafanye tathmini pia mitaa gani inafanya vizuri ama vibaya chanzo ni nini na nini kifanyike kuboresha.

viongozi wakuu wilaya na mkoa washiriki kwa kuwatia moyo hasa maeneo yale yenye uchafu uliokithiri. Kama ikikubalika kwenye sheria ndogo ndogo zikubaliane hakuna kufungua biashara kabla ya muda wa kufanya usafi kukamilika. Serikali ya wilaya na mkoa kuhakikisha taka zinachukuliwa na makandarasi kwa wakati kabla hazijasaambaa mtaani tena.

Mwisho maeneo yote ya wazi, bustani, barabara zinazoweza kuoteshwa maua, ukoka na vitu vya kupendezesha mji viorodheshwe na mamlaka husika ziombe makampuni mbali mbali yaliyopo jijini yahudumie maeneo hayo. Mfano round about zote Moshi zinahudumiwa na Bonite Botlers, eneo la barabara Lugalo linahudumiwa na Jeshi limependeza sana. Hivyo basi jiji waombe makampuni na mashirika yaliyopo Dar wapendezeshe jiji letu.


TUSISUBIRI AJE OBAMA ndio MJI UFANYIWE USAFI


Vile vile omba omba wamerudi jiji? je katazo lile limefutwa?
 
Aiseeeee, tumeshindwa kwenye hii kampeni tumebakia kuwaumiza watu wasifungua maduka kabla ya saa nne
 
Back
Top Bottom