Kampeni ya Kuhamia Dodoma na Kufuta Sitting Allowances

Kampeni ya Kuhamia Dodoma na Kufuta Sitting Allowances

Onesmo Kyauke

Member
Joined
Feb 9, 2015
Posts
67
Reaction score
119
Kwanza nichukue nafasi hii kumpongeza Mh Rais kwa jitihada zake za kujaribu kupunguza matumizi ya serikali yasiyo ya lazima. Ultimatum mabovu limekuwa tatizo kubwa sana Tanzania kwani hata wageni wanatucheka kwa kukosa vipaumbele. Unakuta akina mama wajawazito wanalala chini, watoto wa shule wanakaa kwenye vumbi lakini wafanyakazi wa serikali wanatanua na magari ya bei mbaya na kulipana posho zisizo na lazima.

Kuna maeneo mawili ambayo ni mirija ya kula hela ya umma. Kwanza ni serikali kutohamia Dodoma hivyo mfanyakazi ambaye kituo chake cha kazi kipo Dodoma anakaa Dar hivyo serikali inaingia gharama kubwa kuwalipa hawa wafanyakazi ambao ni wengi.

Pili, posho. Tumesema sana kwamba wafanyakazi wanalipwa mishahara hivyo haiingii akilini kwamba mtu anapewa sitting allowance wakati muda wa kikao upo ndani ya muda wa kazi ambao tayari ameshalipwa mshahara.

Nini kifanyike? Nashauri serikali ya Dr Magufuli iamue kuhamishia makao makuu Dar au kuhamia Dodoma ili kupunguza matumizi ya umma. Pili, posho zote zifutwe ili serikali ipate fursa ya kuangalia upya mishahara ya wafanyakazi wote. Ni dhahiri kwamba posho za vikao zinanufaisha wakubwa peke yao huku wadogo wakiuguza maumivu.

Naomba kuwasilisha.

Onesmo
 
Hili limesemwa sana, lakini nimeona mahali kama mkulu kaagiza wabunge wasiwe wajumbe wa bodi wala taasisi za umma, agizo hili litekelezwe mala moja
 
Teh teh

Kuhamia dodoma.

Safi sana

Kuna wengine wataacha kazi
 
Mkuu ameleta thread hii tufanye kampeni ili kuleta shinikizo la matakwa yenye maslahi kwa umma. Kwahiyo kupitia uzi huu naunga mkono pia suala la wabunge kufutiwa sitting allowance na ikiwezekana kupunguziwa mishahara ili iendane na watumishi wengine, sambamba na kutopewa mikopo kutoka ofisi ya bunge, na badala yake wakakope benki na kulipa kodi. Kampeni iendelee.
 
Kiukwel kama asopoangalia hali za wafanyakazi wa chini watoa huduma kwa kuwapa maslai ya kuridhisha hatari IPO. Mwl. ambae analipwa kiasi cha tsh. 400000 kwa mwezi bila kuwa na posho wala nni halafu ana familia ni vigumu sana kufanya Kazi yake kwa ufasaha ukilinganisha na MTU anaepewa pesa hiyo kama posho ya kikao cha nusu saa. Kiukwel na hii ya kufuta michango ambayo walimu walitegemea walau kupata elfu mbili mbili za nauli ndo italeta shida zaidi. Yaani bora ianzishwe posho kwa wafanyakazi wote wa umma ili isaidie kupata nauli na usimamizi uongezwe.
 
Serikali ifute mpango wa kuhamia Dodoma, sasa sio zama zile za zamani za hofu ya kiusalama sasa ni zama za hofu ya kiuchumi. Hatuwezi kama nchi kuingia gharama tena ndani ya karne ya 21 eti kuhamisha makao makuu ya nchi. Dhana hiyo ilikuwa na nguvu mpaka miaka ya 90 hasa kipindi cha vita baridi. Katika zama za sasa za decentralization and devolution dhima ya "makao makuu" au "mjini mkuu" ni ndogo sana. Tuimalishe halmashauri zetu za wilaya, miji na majiji na wala sio "mjini mkuu".
 
Serikali ifute mpango wa kuhamia Dodoma, sasa sio zama zile za zamani za hofu ya kiusalama sasa ni zama za hofu ya kiuchumi. Hatuwezi kama nchi kuingia gharama tena ndani ya karne ya 21 eti kuhamisha makao makuu ya nchi. Katika zama za sasa za decentralization and devolution dhima ya "makao makuu" au "mjini mkuu" ni ndogo sana. Tuimalishe halmashauri zetu za wilaya, mini na makini na wala sio "mjini mkuu".

Wabunge wajengewe hostel na watasafiri kwa usafiri maalum wa pamoja ili kupunguza matumizi yasiyo na lazima.
 
Wabunge wanunuliwe basi moja kubwa lakuwapelekw na kuwarudisha kutoka kwenye vikao vyao
 
Hoja ya msingi sana.

Pia JPM ageukie magari ya serikali. Huko nako kuna ufujaji wa pesa kupindukia. From fuel, purchasing of the cars and maintenance.
 
Kwa akili yangu nashauri serikali ijenge kitu kama hostel pale Dodoma. Design inakuwa na partition. Apartment moja inakuwa na vyumba viwili (self contained), sebule, jiko na dinning na stoo. Na pawe na appartments zitakazotosha wabunge wote.
Wakati wa vikao Dodoma, hakuna cha kwenda hotelini, kila mmoja bwenini kwake ili pasiwe na sitting allowance. Kwa kuwa wana mishahara, watajua watakulaje watakapokuwa Dodoma maana hapo watakapoishi kuna jiko. asiyetaka akale hotelini kwa gharama yake.
 
Serikali ifute mpango wa kuhamia Dodoma, sasa sio zama zile za zamani za hofu ya kiusalama sasa ni zama za hofu ya kiuchumi. Hatuwezi kama nchi kuingia gharama tena ndani ya karne ya 21 eti kuhamisha makao makuu ya nchi. Dhana hiyo ilikuwa na nguvu mpaka miaka ya 90 hasa kipindi cha vita baridi. Katika zama za sasa za decentralization and devolution dhima ya "makao makuu" au "mjini mkuu" ni ndogo sana. Tuimalishe halmashauri zetu za wilaya, miji na majiji na wala sio "mjini mkuu".

Kuhamia dodoma kuna faida kubwa sana kuliko hasara unayoiwaza.

Dar limeshabanwa na shughuli mbalimbali, serikali ibaki dodoma na dar kubaki biashara.
 
Wabunge wajengewe hostel na watasafiri kwa usafiri maalum wa pamoja ili kupunguza matumizi yasiyo na lazima.
Wasafiri kwa usafiri wa pamoja kutoka wapi kwenda wapi? Kila mbunge anatakiwa kuishi jimboni kwake. Hii habari ya wabunge wote kutaka kuishi dar ndiyo inasababisha wengine wanakwenda jimboni akitembelea huko kiongozi au wakati wa kampeni ukikaribia.
 
Wengi wao si wanaishi Dar, kwahiyo watasafiri kwa pamoja, watakutana stand ubungo na safari kuanza. Hilo la kukaa majimboni ni suala lililo mikononi mwa wananchi ambao ndio huwachagua wabunge. Kwahiyo wananchi wakisema wanataka mbunge akae jimboni halafu akakaidi wanampiga chini tu kwenye uchaguzi mwingine.

Swali la kizushi, PM majaliwa na mawaziri ambao ni wabunge wa majimbo yaliyo mbali na ofisi zao za kiserikali nao wakae majimbonj mwao?
 
Pili, posho. Tumesema sana kwamba wafanyakazi wanalipwa mishahara hivyo haiingii akilini kwamba mtu anapewa sitting allowance wakati muda wa kikao upo ndani ya muda wa kazi ambao tayari ameshalipwa mshahara.

Nini kifanyike? Nashauri serikali ya Dr Magufuli iamue kuhamishia makao makuu Dar au kuhamia Dodoma ili kupunguza matumizi ya umma. Pili, posho zote zifutwe ili serikali ipate fursa ya kuangalia upya mishahara ya wafanyakazi wote. Ni dhahiri kwamba posho za vikao zinanufaisha wakubwa peke yao huku wadogo wakiuguza maumivu.

Naomba kuwasilisha.

Onesmo

hilo limeshughulikiwa leo
 
Attachments

  • AkkuOY8kohklTFLcOocdCqYpYioYKIiuZENvu_4VPU11.jpg
    AkkuOY8kohklTFLcOocdCqYpYioYKIiuZENvu_4VPU11.jpg
    60.2 KB · Views: 371
Serikali ifute mpango wa kuhamia Dodoma, sasa sio zama zile za zamani za hofu ya kiusalama sasa ni zama za hofu ya kiuchumi. Hatuwezi kama nchi kuingia gharama tena ndani ya karne ya 21 eti kuhamisha makao makuu ya nchi. Dhana hiyo ilikuwa na nguvu mpaka miaka ya 90 hasa kipindi cha vita baridi. Katika zama za sasa za decentralization and devolution dhima ya "makao makuu" au "mjini mkuu" ni ndogo sana. Tuimalishe halmashauri zetu za wilaya, miji na majiji na wala sio "mjini mkuu".

Kwani makao makuu official ya nchi yako wapi?
 
Magufuli abaki dar tu, akihamia dom mijizi itaiba huku, bora abaki hapa hapa Tanzania, maana dar ndio Tanzania
 
Wengi wao si wanaishi Dar, kwahiyo watasafiri kwa pamoja, watakutana stand ubungo na safari kuanza. Hilo la kukaa majimboni ni suala lililo mikononi mwa wananchi ambao ndio huwachagua wabunge. Kwahiyo wananchi wakisema wanataka mbunge akae jimboni halafu akakaidi wanampiga chini tu kwenye uchaguzi mwingine.

Swali la kizushi, PM majaliwa na mawaziri ambao ni wabunge wa majimbo yaliyo mbali na ofisi zao za kiserikali nao wakae majimbonj mwao?
PM na Mawaziri wanao ofisi zao Dar es Salaam, hawawezi kukaa majimboni. Vipi kuhusu wabunge, si wanatakiwa kuwa na ofisi zao majimboni (katika hali ya kawaida)?...
 
Back
Top Bottom