Kampeni Igunga zatawaliwa na vituko badala ya Sera | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kampeni Igunga zatawaliwa na vituko badala ya Sera

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Makupa, Sep 24, 2011.

 1. M

  Makupa JF-Expert Member

  #1
  Sep 24, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Tulitegemea kuwa kampeni za Igunga zingetawaliwa na sera za vyama husika ili wananchi maskini wa nchii waweze kutambua ni mgombea yupi anafaa ili aweze kuwahudumia wanachi wa Igunga, badala yake tumeshuhudia vituko vya kila aina ambavyo ni aibu kwa demokrasia yetu changa.
   
 2. Kijuche

  Kijuche JF-Expert Member

  #2
  Sep 24, 2011
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 419
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Labda navyo ni sehemu kampeni.
   
 3. d

  dotto JF-Expert Member

  #3
  Sep 24, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  ILi wasijitokeze wengi kupiga Kura! Ni namna ya kuvuruga wapiga Kura hasa pale umeshajua mambo magumu! NI uhuni. SAsa sijui Mhuni ni yupi kati ya Tume ya UCHAGUZI NA WENYE VYAMA.
   
 4. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #4
  Sep 24, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  CHONDE TAASISI ZINAZOTUONGOZAA KIDINI NCHINI ZISIWE ZIKIKIMBILIA SANA KWENYE KIOO KUTEKELEZA MATAKWAA YA WANASISA WAASIOAMINIKA KATIKA JAMII

  Ama kweli ajizi nyumba ya njaa; CCM kumbe walikua wamewaingiza porini kabisa baadhi ya ndugu zetu Waislamu kwa taarifa za uongo kama hivi???

  Kwa kweli sikujua kwamba ni yule yule mama Kimario jirani yetu kule Mbezi ndiye aliyekua akizungumziwa muda wote. Jamani yule mama wala si Muislamu ni mkristo safi tena Mzee wa Kanisa pale Wazo, duuuhh hawa jamaa jamani!!!!!!

  JF team tayari ilishazuru kule kwenye shamba lake la pili kule Tegeta na picha zote za shamba lake tayari ziko hewani JF kusaidia kuthibitisha ukweli kwamba kasingiziwa na CCM taarifa hizo hapo juu.

  Mpaka hapa sasa sijui kwamba BAKWATA watalazimika kuitisha mkutano mwingine kukana taarifa zao za awali juu ya huyu mama. Jamani
  si kila Fatuma ni Muislamu WAKATI MWINGINE NI JINA TU LA UKOO hivyo kukimbilia kutolea tamko hata mtandio tu wa urembo mtu eti ni hijabu ni makosa sana tu.

  Hijabu sisi sote tunaifahamu na kuiheshimu sana; kwa kawaida hutanda kichwani hadi miguuni tena kushitiri mwili mzima sembuse kale ka ulimi wa ng'ombe aliojitupia Mama Kimario kuwahi kwenye kutengeneza misheni za kura zisizoibika Igunga???????????
   
 5. Naibili

  Naibili JF-Expert Member

  #5
  Sep 25, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,680
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  basi kama ni uwanjani hapa kuna watu watafunga magoli mengi lakini kati ya hayo mengi watajifunga wenyewe, kama tunategemea siasa hizi ndo zionyeshwe 2015 basi tuna kazi kweli kweli, inabidi tuwaombe wakina ocampo waweke kambi hapa nchini kwa kipindi hicho ili ushahidi uwepo wa kutosha!
   
 6. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #6
  Sep 25, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  mbona wameumbuka
   
 7. usininukuu

  usininukuu JF-Expert Member

  #7
  Sep 25, 2011
  Joined: Aug 8, 2011
  Messages: 380
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante mkuu kwa taarifa Njaa za viongozi wa dini Zisitupelekee Uchochezi.
   
 8. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #8
  Sep 25, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,592
  Likes Received: 4,697
  Trophy Points: 280
  Hivi hii ndoa ya CCM na BAKWATA itatuletea mtoto gani watanzania? Na Waislamu wa kweli mko wapi kuwakemea hawa mashehe matumbo wanaoudhalisha Uislamu kiasi hiki?
   
 9. O

  Omr JF-Expert Member

  #9
  Sep 25, 2011
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 1,160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo ni sawa kudhaliliswa kwa kuwa yeye ni Mkristo na sio mwislamu?
   
 10. Nsiande

  Nsiande JF-Expert Member

  #10
  Sep 25, 2011
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 1,649
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Si sawa kudhalilishwa,

  ila si sahihi kwa BAKWATA kutolea tamko muislam swafi ilhali anafuga haram shambani kwake

  Serikali huko Igunga kwa maana ya jeshi la polisi etc ndio ilitakiwa itoe tamko hilo na si BAKWATA kwa niaba ya waislam

  Za kuambiwa changanya na zako!
   
 11. O

  Omr JF-Expert Member

  #11
  Sep 25, 2011
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 1,160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Na je Kanisa likitoa tamko la kupinga udhalilishaji uliofanyika kwa huyu mama, Jf watafanya kazi za ziada kama walivyo fanya wakati BAKWATA ilivyo lalama?
   
 12. O

  Omr JF-Expert Member

  #12
  Sep 25, 2011
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 1,160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hiyo haramu ni dili bibie, kipato chake ni kizuri sana. Mnyama sio haramu kumla ndio haramu. Kwani wanao fuga paka na mbwa wanawala?
   
 13. Nsiande

  Nsiande JF-Expert Member

  #13
  Sep 25, 2011
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 1,649
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Omr kama umehalalisha mimi sina tatizo kabisa
   
 14. silver25

  silver25 JF-Expert Member

  #14
  Sep 26, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Misiwe na Roho ngumu nyinyni au na nyinyi mmetumwa kuja ivuruga JAMII FORUMS, kwani nyie hamjui jinsi CCM wanavyo wadanganya BAKWATA na wao wanatoa kura kisha kuwageuka?
  Suala la Mahakama ya kadhi likowapi,, lakini KIKWETE si aliwaahidi na wao wakampa kura haya sasa kiko wapi,, hao jamaa wanambinu nyingi na wameona kuwaingia Wakristo ni ngumu wana wadanganya WAISLAM sasa na sisi waislam tuseme kwa pamoja HATUDANGANYIKI SASA HIVI,, chukua CCM tupa kuleeeee chagua chama kingine kifanye kazi
   
 15. Mtoto Wa Mbale

  Mtoto Wa Mbale JF-Expert Member

  #15
  Sep 26, 2011
  Joined: May 15, 2011
  Messages: 458
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Inasikitisha ccm wameamua kuwagawa watanzania kwa misingi ya dini. Hii ni mbegu mbaya sana kuipandikiza kwa wananchi na matokeo yake tutayaona.

  Sitarajii dini zingine kuingilia suala la kisiasa kama ilivyofanya BAKWATA ambao walienda mbali zaidi na kuwataka wananchi wa Igunga wasichague CDM. Nimesikitishwa na kitendo cha serikali kutshindwa kukemea tamko hilo. Hata tume ya uchaguzi na polisi wameamua kwa makusudi kunyamazia kitendo hicho hatari kwa mustakabali wa Amani ya nchi yetu. Sasa ni dhahiri ccm iko tayari kumwaga damu ilimradi wang'ang'anie madaraka hata pale wananchi wanapowakataa!

  Nawaomba wana Igunga muwe jasiri, msikubali kuyumbishwa. Chagueni kiongozi atakayesimamia vyema rasilimali za watanzania kwa faida ya watanzania.
   
 16. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #16
  Sep 26, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Vioja vya ccm vinazidi kuongezeka
   
 17. M

  Mantaleka Senior Member

  #17
  Sep 26, 2011
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mhn ! aibu ehh !!
   
 18. k

  kiloni JF-Expert Member

  #18
  Sep 26, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 575
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tunafahamu hata kule mgombani kwao akinamama wote wanajitanda kanga kichwani!
  Huyo ni mkristo MAGAMBA kimenuka! leteni jingine>!
   
 19. fikramakini

  fikramakini JF-Expert Member

  #19
  Sep 26, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 247
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu kama hii habari ni ya kweli, basi hatuna BAKWATA wala hatuna CHAMA TAWALA.
   
 20. fikramakini

  fikramakini JF-Expert Member

  #20
  Sep 26, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 247
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Zishauri zile timu za mpira za visiwani basi zisikatae ufadhili wa TBL kwani nao wanaleta kipato
   
Loading...