Kamilius Membe, tunaomba Usubiri 2025

Mwingereza

JF-Expert Member
Jan 21, 2014
1,115
2,771
Ndugu Kamilius Membe (Kachero Mbobezi) Tunakuomba upumzike usubiri 2025. Kwa hali ya sasa, kama kweli una dhamira ya kuleta mageuzi, inabidi umwachie Tundu Lissu apambane na Magufuli. Huyu ndio mtu pekee anayeweza kupambana na Magufuli na kumshinda.

Uking'ang'ania kugombea, utaoneka pandikizi huku unijua wazi kabisa hauwezi kushinda. Miaka hii mitano inakutosha kuzijua siasa sa upinzani na ugumu wake na watanzania watakuamini na hata kukupa kura. Kwa sasa utazigawa tu kura za upinzani.

Kumbuka haba na haba hujaza kibaba. Tunakuomba uende kusini uibomoe CCM huku kwingine utakuwa kama wakina Mbatia, Lowassa na Mrema.
 
Huyu ndio najua pa kushika ili akitoe sisiem ni Kachero wengine hawa mtakula kekundu tu
 
Ni kweli kwa sasa ajikite kukijenga chama chake kipya.....pia apate muda ya kuonja shuruba za siasa za upinzani...

Kwa sasa akili ya watanzania wote IPO kwa Lissu Antipas.
 
Tafakari yangu ni hii: uchaguzi wa mwakao huu unachangamoto kubwa mno na ushindi siyo dhahili. Hapa kama Membe mnamtaka agombee 2025 msije mkamuharibia maana uchaguzi huo utakuwa ni rahisi sana kushinda. CCM haitakuwa na mwenyewe wkati huo. Hivyo karata lazima zichangwe vizuri.
 
Pengine mleta mada amekumbwa na mhemko. Membe atamuachiaje Lissu agombee peke yake halafu Chadema kitarajie kushinda uchaguzi wakati kimeshindwa kuweka wagombea katika majimbo yote 264? Chadema kimeweza kupata wagombea 163, nakisi ni wagombea 101.

Bila shaka umeelewa kuwa kinachotakiwa kufanyika kwa sasa ni Lissu kushirikiana na Membe kupata synergies za kuifurusha CCM madarakani asubuhi na mapema. Umoja ni nguvu.....usipalilie utengano.
 
Sidhani kama amekuelewa!
 
Back
Top Bottom