Kamilisha Tafsiri Ya Valentine Kwa Kufanya Haya

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
213
Pumzi anayotupa ni rasimali muhimu isiyoweza kufananishwa na kitu chochote, kwahiyo ni uungwana wetu kumshukuru yeye Muumba wa vyote, kwa upendeleo aliotupa mimi na wewe. Unadhani ni wangapi walitamani kuiona leo, lakini imeshindikana?

Ukiweza kujiuliza swali hilo kikamilifu, hapo itakuwia rahisi kupata jawabu kuwa umependelewa, hivyo si vibaya ukiwakumbuka kwa kuwaombea ndugu na jamaa wenye matatizo au hata wale waliokwisha tangulia mbele ya haki.

Ni mara nyingine, tunakutana katika kona yetu ya Love and Marriage ambayo kama ‘kawa’, hukuletea mada mbalimbali zinazohusu masuala ya kimapenzi, lengo kuu likiwa ni kupeana darasa tosha la uhusiano ili wewe ndugu yetu usiachwe njiani katika muktadha huu.

Tunazungumzia mapenzi, pia tupo kwenye wakati wa maadhimisho ya siku hiyo ya mapenzi. Hii inaitwa Valentine Day, bila shaka kila mmoja ambaye anaye wake mwenzi wa maisha, hivi sasa anajiwinda ili itakapowadia, aweze kushehekea ipasavyo.

Ni siku maarufu katika ulimwengu wa sasa, na aghalabu, wanachama wenye jinsia ya kike hutinga viwalo vyenye rangi nyekundu, huku wale wa kiume, huipatia sana kwa kukong’ota pamba za cream. Endapo utafanikiwa ‘kunyuka’ suti ya rangi hiyo, basi kwako siku itakuwa murua ile mbaya.

Inapozungumzwa Valentine, kwa mtazamo wa haraka inakuwa inawagusa zaidi wale ndugu zetu wenye mitazamo ya kisasa zaidi, kwa wengine wanaodhani mapito ya utandawazi yamewapita kushoto, huwa hawana habari na siku hiyo kabisa.

Unadhani lipi ni sahihi? Jibu ni kwamba kila mmoja anao uhuru wa kusherehekea siku hii kwa ‘raha zake’. Dhana ya Valentine kama ilivyoasisiwa na St. Valentine, haiweki matabaka katika kusherehekea, inaamini kila mtu ana uhuru wa kupenda, hivyo yupo huru ‘kujiachia’.

Aidha, haisemi yule asiye na mwenzi wa maisha, aione siku hii haimhusu, bali inampa mwanya wa kumchangua valentine wake katika siku husika. Yote kwa yote ni kuthibitisha kuwa siku hiyo, haimtengi mtu, bali ni rafiki wa watu wote.

Valentine, anaweza kuwa baba, mama, dada, kaka, mjomba, shangazi au ndugu mwingine yeyote. Hata hivyo, kwa jinsi inavyochuliwa, siku hii hunoga zaidi, iwapo wenzi wenye uhusiano wa kimapenzi, watakuwa bega kwa bega.

Pamoja na hali hiyo, ni vizuri kutambua ya kwamba hata babu na bibi yako wanahitaji kuona mapenzi yako, hivyo nao unatakiwa uwakumbuke kwa staili yao.

Pengine hawahitaji kadi kwakuwa hawana mzuka na mambo ya ‘uzungu’, lakini hiyo haikufanyi ushindwe kuwazawadia vitu ambavyo vitawafanya wakenue kwa meno yote 32.

Umeshawahi kujiuliza kuhusu watoto yatima na wajane? Ni vizuri ukatambua kuwa siku hiyo ni ya wapendanao, kwahiyo nao hawatakiwi kutengwa, hivyo pamoja na kubanwa na mwenzi wako, akitaka muwe pamoja kwa saa 24, lakini upendo wenu kwa watu hao ni muhimu.

Valentine Day ni nini? Tafsiri iliyo karibu ni kuwa hiyo ni siku ya wapendao ambayo huadhimishwa kila Februari 14 ya kila mwaka. Leo ni Februari 8, hivyo zimebaki siku 5 tu ili kufikia kilele cha sherehe hiyo.

Hivyo basi, ndiyo maana nikateua Love and Marriage ya leo na ile ya Jumatatu inayokuja, tuizungumzie siku hiyo kwakuwa sisi wana Mapenzi na Ndoa, inatugusa moja kwa moja.

Hata hivyo, yapo mambo ambayo endapo yatazingatiwa, ndiyo yanayoweza kueleza tafsiri hali ya Valentine na ukiyatekeleza, yatakufanya nawe uwe umesherehekea sikukuu hiyo kikamilifu.

Yafuatayo hapa chini, baadhi ya mambo ambayo, yakitimizwa kikamilifu, yatatoa tafsiri sahihi ya Valentine Day

UWAZI
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom