KAMERA DARAJA LA MFUGALE KUKAMILIKA WIKI 2 ZIJAZO

KAMERA DARAJA LA MFUGALE KUKAMILIKA WIKI 2 ZIJAZO

diana chumbikino

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
428
Reaction score
368
1552644735630.png


UTEKELEZAJI wa agizo la Rais John Magufuli la kufungwa kamera kwenye Daraja la Juu la Mfugale, Tazara jijini Dar es Salaam utakamilika ndani ya wiki mbili kuanzia sasa baada ya kamera 14 zilizobaki, kuwasili nchini jana.

Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi na Mikataba cha Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) mkoani humo, Abednego Lyanga alisema hadi sasa kamera mbili zilishafungwa na zilizobaki ni 14 na zitafungwa kuanzia leo. “Kamera mbili zilifungwa mwishoni mwa Januari mwaka huu na kamera nyingine 14 zilikuwa bado, kampuni ya E 1 ndiyo ilishinda zabuni ya kazi hiyo ya kuzinunua na kufunga na wamesema walishaagiza kamera zilizobaki nje na zinaka leo (jana) kazi ya kuzifunga itachukua takribani wiki mbili kuanzia sasa, hivyo wiki ijayo huenda zikawa tayari,” alisema Lyanga.

Alisema katika daraja hilo na eneo hilo kwa ujumla zinahitajika kamera 16 ambazo zitakuwa zikionesha matukio yote yanayoendelea katika eneo hilo na iwapo makosa ya usalama barabarani yatafanywa na madereva, itakuwa rahisi kuwabaini na kuchukua hatua. Alisema kamera hizo zitakuwa zinafanya kazi muda wote na zinafungwa ili kuhakikisha miundombinu ya eneo hilo inakuwa salama na pia kubaini madereva wanaokiuka sheria za barabarani ili vyombo husika viwachukulie hatua.

Awali, agizo la kufungwa kamera hizo lilitolewa Septemba 27, 2018 na Rais Magufuli wakati akizindua daraja hilo na kusisitiza kuwa kamera hizo zitawabaini wanaoendesha vyombo vya moto bila kufuata taratibu wakiwemo walevi. Miezi mitatu baada ya agizo hilo la Rais, utekelezaji ulianza kwa kamera mbili kufungwa mwishoni mwa Januari mwaka huu na sasa hizo 14 zilizobaki zitafungwa muda wowote kuanzia sasa. Lyanga alisema makubaliano ya mzabuni ambaye ni kampuni hiyo ya E 1 ni kufunga kamera 16 na wameshafunga mbili na zilizosalia zinatarajiwa kufungwa kuanzia leo
 
Nitapambana Na Rushwa Bila Kigugumizi Chochote Na Dawa Ya Jipu Ni Kulitumbua
 
Back
Top Bottom