Kambi za starehe uraiani

Kiby

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2009
Posts
6,933
Reaction score
4,709
Jamani naomba msaada hasa wa kisheria. Kuna ukumbi wa starehe umefunguliwa karibu na makazi yetu hapa ni siku ya tatu leo nyumbani hatusikilizani. Ninataka kujua;
(1) Naweza kumfungulia mwenye ukumbi mashtaka?
(2) Nimfungulie shitaka gani?
(3) Ninaweza kudai fidia ya usumbufu wa kutokulala kwa sababu ya kelele?
(4)*kama nitaamua kufungua kesi mtoa vibali vya kumbi za night club katika makazi ya watu ninaweza kumjumuisha katika shtaka?

.
My take serikali yetu ndio imekuwa orijojo katika kusimamia seria na kanuni za mipango miji au ni raia wameamua kujichukulia sheria mkononi? Aah mimi bana nimechoshwa na hii mikelele kiasi kwamba ndani kwetu kuwasiliana inakulazimu kutumia nguvu nyingi ili usikike.
Naondoka zangu kwenda nje ya mji(kibaha) kupumzika na familia yangu mpaka mikelele ipungue. Hata hivyo nnani atanilipa gharama zangu za kwenda nje ya mji?
Hebu tusaidiane mawazo wanajamvi.
.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…