Kambi ya Upinzani yataka Posho zifutwe na Wabunge wasiochangia hoja na Bungeni wakatwe mishahara!

SeriaJr TW

JF-Expert Member
Oct 21, 2012
246
224
Shemu ya hotuba ya msemaji wa Kambi ya Upinzani kuhusu masuala ya fedha na Bajeti, Mh Silinde David inasomeka hivi...

"Mheshimiwa Spika, kabla sijatoa maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani kuhusu bajeti ya Serikali ya 2016/17, napenda kuweka rekodi sawa kuhusu upotoshaji unaofanywa na Wabunge wa CCM kwamba Wabunge wa Upinzani wanaisaini mahudhurio bungeni na kuchukua posho bila kufanya kazi. Napenda mkumbuke kwamba, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imekuwa ikisisitiza kufutwa kwa posho za vikao kwa maana ya “Sitting allowance”, lakini serikali imekuwa ikipata kigugumizi, hivyo basi Kambi Rasmi inasema kama kweli Serikali ya Rais John Pombe Magufuli inania thabiti ya kubana matumizi ya Serikali basi inoneshe uthabiti huo kwa kuifuta posho ya vikao na fedha hizo zipelekwe kwenye miradi ya maendeleo hususani kuwapatia Watanzania maji safi na salama. Hata hivyo, tunashauri, wale wanaokaa bungeni bila kuchangia hata kwa maandishi na kuchukua posho, wafuatiliwe na wakatwe mishahara yao, kwa kuwa hawajafanya kazi na hansard itumike kuwabaini.

Mheshimiwa Spika, katika jitihada kuongeza mapato, Serikali katika bajeti hii imekusudia kukata kodi ya asilimia 5 kwenye kiinua mgongo cha wabunge. Kambi Rasmi ya Upinzani haina tatizo na pendekezo hilo, ila inaitaka Serikali kwenda mbali zaidi kwa kuifanyia marekebisho sheria ya mafao ya viongozi wa kisiasa ambayo kwa sasa imewapa misamaha ya kodi ya viinua mgongo viongozi wakuu wa kisiasa kama Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Mawaziri, Spika, Naibu Spika, Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya ili sasa na wao walipe kodi hiyo. Hata hivyo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaikumbusha Serikali kwamba kiinua mgongo cha wabunge hutolewa mwisho wa uhai wa bunge husika, hivyo haioni mantiki ya kutoa pendekezo hili sasa kwa kuwa halina impact kwa bajeti ya 2016/17..."
 
AKA posho ya makalio!!! Kwa maoni yangu hii ilipaswa kufutwa zamani sana. Haina maana yoyote mtu kufika Dodoma ukapewa posho ya kujikimu na ya usafiri halafu eti kitendo cha kuingia bungeni na kukaa upewe posho nyingine "ya makalio". Inaweza kuwa ni kwa mujibu wa kanuni lakini it does not make sense at all. Wa ulevini lumumba hawawezi kukubali ikatwe. Hivyo basi, kanuni zapaswa kubadilishwa, posho ya makalio iondolewe kabisa.
 
Kambi Rasmi ya Upinzani haina tatizo na pendekezo hilo, ila inaitaka Serikali kwenda mbali zaidi kwa kuifanyia marekebisho sheria ya mafao ya viongozi wa kisiasa ambayo kwa sasa imewapa misamaha ya kodi ya viinua mgongo viongozi wakuu wa kisiasa kama Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Mawaziri, Spika, Naibu Spika, Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya ili sasa na wao walipe kodi hiyo."

Kwa maslahi mapana ya taifa hoja ina mantiki...
 
Hii ishu iko sawa kimantiki, ila kiuwajibikaji bado inatufanya twendelee kuelewa kumbe kiuharisia Tz haina wapinzani makini bali ina wajanja wajanja na watu wa fursa kibao wanaojiita wana siasa. Kwahiyo sasa tuwaone leo ndo wamegundua kumbe hii ni hoja? kumbe wamekuja sasa na mbinu ya kumwaga ugari na mboga, tukose wote? Na wakati wa kupata tukipata sote wala si shida? nimekubali sana pia kwamba ukila na kipofu usimshike mikono. Jamaa kumbe walifurahi kuendelea kula posho ila sasa imewagusa baada ya kuambiwa "wao" hawataipata. Hizi ni hasira za kitoto mno, wala si kwamba eti wanatuonea huruma. Ni kwamba wote wanashindana kula na kukosa, matumbo ndo tatizo. Mie napendekeza watanzania tukomae kiakiri, tuachane na hawa wanasisa "kula", tuachane na huu upuuuzi wa wanasiasa, hii nchi inakwama na inakwamishwa na hawa hawa na siasa zao za " kula" na "tukose" sote, ni upuuzi mtupu kuwahi kutokea.
 
Vaa pempasi unye ulale
 
Back
Top Bottom