Kambi ya upinzani mmetusaliti

Kambi ya upinzani mmetusaliti

KARLMARX.

Member
Joined
Jun 3, 2012
Posts
5
Reaction score
0
Bajeti iliyopita Mh. Zitto kwa kauli yako ulitushawishi wananchi wa vijijini tusiandamane kupinga bei ya mafuta ya taa kwa madai kwamba fedha itakayopatikana itapeleka umeme vijijini, mbona hatujaona hata dalili wala sijakusikia ukizungumzia hilo?

Mafuta ya taa yalipandishwa bei yawe sawa na dizel na petrol ili wafanyabiashara wasichakachue na kuharibu magari ya waheshimiwa hasa pale msafara wa JK ulipowekewa mafuta yaliyochakachuliwa siku ile? Kipindi cha kampeni.
Bei ya mafuta ya taa ni mzigo sana kwetu sisi wa vijijini, hatuna mbadala; mbona mmethamini magari yenu kuliko utu wa watu waliowapa madaraka?

OMBI LANGU NI KWAMBA M4C ISIMAMIE JAMBO HILI MAANA TULISHAKATA TAMAA NA HII SERIKALI YA MASHANGINGI NA MATANUZI NDO MAANA SIJAMUULIZA HATA MBUNGE WANGU WA MLALO MWANAJESHI MSTAAFU, HASSANI NGWILIZI. YEYE ALISHASEMA HATAKI KUPAYUKA LJKN VITENDO PIA HATUONI.:boxing:
 
Tena huko vijijini ndio mlikuwa mnaipigia CCM kura sana mkiandamana huko ffu mmoja tu anawatosha
 
Pole sana mkuu,
Zitto yumo humu atakupa jibu linalokuhusu.
Ila mimi ambaye sii mbunge, nasikitishwa na hatua ya wewe na wenzako kusaliti harakati za kutafuta maendeleo kwa kuchagua mbunge wa CCM.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
kumbe mbunge wako ni gamba,craaaaaaaaaaaaaaapppppppppppppp
 
Bilashaka Mh.Zitto atakupa jibu la kukuridhisha. Pia Inaelekea unaufahamu mzuri wa elimu ya kiraia, hivyo jaribu kuwafumbua macho na wenzio
 
Hivi hujasikia mikataba na wachina ya kufuwa umeme ya Mkaa wa mawe kuwa imesha sainiwa?

Pitia hapa uone miradi ya umeme inayoendelea sasa hivi, bonyeza kifungo "projects". Mambo siku hizi yako wazi, usingoje kuzugwa na upinzani. Welcome to TANESCO
 
Back
Top Bottom