Kambi ya mateso yagunduliwa Zimbabwe

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
8 Agosti 2011 11:28

?


BBC Panorama imegundua kwamba, kambi ya mateso inayosimamiwa na majeshi ya usalama ya Zimbabwe inafanya shughuli zake katika eneo lenye utajiri wa almasi, Marange.

Kipindi hicho kilizungumza na walioathirika hivi karibuni wakielezea walivyopigwa sana na kudhalilishwa kijinsia.

Madai hayo yanatolewa huku Umoja wa Ulaya EU ukishinikiza kuruhusu baadhi ya almasi zilizopigwa marufuku kutoka nchi hiyo inayoongozwa na Rais Robert Mugabe kurejeshwa kwenye masoko ya dunia.

Serikali ya Zimbabwe haijasema lolote kuhusu utafiti huo wa BBC.

Katika nyaraka iliyoonekana na BBC, EU ulisema kuwa sasa una imani kuwa migodo miwili eneo hilo zinafikia viwango vya kimataifa na kutaka almasi zinazoztoka eneo hilo kuidhinishwa haraka iwezekanavyo ili ziuzwe nje, ambayo itaondoa kizuizi cha biashara kilichowekwa mwaka 2009.

Kuzuiwa huko kuliwekwa na Kimberly Process (KP), shirika la kimataifa linalosimamia almasi, kufuatia ripoti za mauaji ya watu chungu nzima na udhalilishaji unaofanywa na majeshi ya usalama ya Zimbabwe katika eneo la machimbo la almasi huko Marange.
 
BBC- hawa wanawalilia babu zao waliotimuliwa hakuna lolote, kwani BABU zao waliwafanyia nini MAUMAU si walikuwa na kambi za mateso zaidi ya hizo, Hizi propaganda tumechoka nazo, wanachokitaka ni ukubaliane nao kwa kila kitu ukitofautiana nao wewe ni adui,
 
Back
Top Bottom