Kambi ya Lowassa yaibuka kidedea UVCCM Arusha

Acha kuonyesha upumbavu wako!!! Kama huna cha maana cha kuandika ni bora ukae kimya.

 
Huyu mwandishi amekaa sana kishabiki,ataharibu Mauzo ya gazeti,azingatie Taaluma ya Uandishi,au angeomba msaada kwa yule bwana wa kijaluo anaemuandikiaga Story,mbali na hapo basi anausaka UDC ambao hatoupata kwa njia ya kishabiki,nani alisema yeye ni wa Membe humo ndani?au wa Lowassa?
 
kabisa. wao ccm si wanajifanya nchi ni ya kwao sasa wasubiri 2015 tutakapo waonesha watanzania tunataka nini kwa maendeleo yetu.

Hao hao chama cha magamba wanaomshangilia leo ,ndio hao hao watakaomuangusha akipambana na Chadema kesho!! Anaweza kuwahonga hao magamba wachahce lakini hawezi kuhonga umma wote wa Tanzania!!!!
 
KATIBA MPYA itatuepusha na wagombea wa aina ya Lowasa. Rais wa WATANZANIA lazima aelezwe vizuri na katiba hii. Endeleeni kumpumbaza Lowasa wenu hukohuko CCM. Mzee JS Warioba, SAS, Prof Baregu, Mzee Butiko wanafahamu tatizo tulilonalo la kuwapata wagombea safi wa URAIS.
 

Hayo ni maneno ya kujifariji,na hayo yanatokea ndani ya ccm,bt kwa huku nje hana chake,hata wao ccm wanajua hilo
 

c tunamsubiri nje ya cccm,full stop!
 
Waandishi wa habari Tanzania bado sana.Unapojaribu kumshindanisha Benard Membe katika uchaguzi unaofanyika Arusha mahali alipozaliwa na kuishi muda mrefu waziri mkuu aliyesusa uwaziri mkuu kwasababu ya kuingiza nchi katika mkataba tata wa Richmond ni kutaka kutulazimisha kuamini Laigwanani ana nguvu sana.

Siasa za makundi ni chanzo kikuu cha kuiangamiza CCM,viongozi wanachaguliwa kwa kuangaliwa wanawakilisha kundi gani na si ubora wake !.

Kama Lowassa ana nguvu kiasi hicho ni kwanini alishindwa kumsaidia mtoto wake kushinda uchaguzi wa Arumeru ?.
 
Hawa ndio journalists wetu TZ ambao wanatakiwa wafanye kazi kubwa ya kutoa taarifa sahihi za rushwa na uovu wote wa watawala na mafisadi. Tunategemea washiriki katika kutoa elimu ya uraia ili watanzania wakaeliewa ni koingozi gani anayefaa. They are sometimes regarded as muhimili wa 4 usio rasmi. We need to get rid of these kanjanjas wa vibahasha ili ukombozi wa mtanzania upatikane.
 
wanaomshangilia ni wana ccm sio wananchi wote,na huko anaposhinda ni kwenye chaguzi za ccm anashindana na membe,sitta na wajinga wenzie.amini nawaambia pakiwepo uchaguzi huru na haki ccm hawatamshinda hata kobe.
 
Kambi inayoongozwa na mbunge wa monduli EL imeendelea kung"ara baada ya kumwagwa LOOTA SANARE aliyekuwa anatetea nafasi yake ukatibu na uenezi kupitia mkoa wa Arusha,Ambapo mfuasi mkubwa wa LOWASSA diwani wa MONDULI MJINI ISACK JOSEPH AMESHINDA kwa kura 46 huku Loota Sanare ameambuli kura 28 tu.
 
Huyo ndiyo lowasa the greatest,huyo ndiyo zuma wa tanzania,huyo ndio raila wa tanznia na huyo ndiyo gamayel wa tanzania.
 
Fisadi Lowassa nani ataweza kumshika wakati nchi yote inanuka rushwa!? Nchi ingekuwa na utawala bora huyu hata asingethubutu kutamka kama anataka kugombea ubalozi wa nyumba kumi kumi!!! achilia mbali kutaka kuwa Rais.
BAK wengi wetu hatutaki kukiri kwamba rushwa nchini mwetu imefikia kiwango cha kijamii na kimfumo. Tatizo tunafikiri kwamba rushwa za wengine ndiyo rushwa za kwetu "tunasaidiana" Unafiki huu utampa Lowassa nchi!!
 
Last edited by a moderator:
Reactions: BAK
Inasikitisha sana kusema kweli kuona ndani ya CCM hakuna mtu yeyote hata wale wastaafu kama akina SAS, Warioba, Msuya n.k. watoe kauli thabiti kuhusu fisadi Lowassa kutostahili kupewa dhamana ya kuongoza nchi. Huyu fisadi amekuwepo ndani ya Serikali kwa miaka mingi sasa akishika nyadhifa mbali mbali katika Wizara tofauti lakini ukiangalia rekodi yake ya utendaji haina lolote lile ambalo linaloonyesha huyu anastahili kukabidhiwa uongozi wa nchi.

Kibaya zaidi ufisadi aliuanza miaka mingi sana na ndio maana yuko kimya kabisa kuhusiana na ufisadi uliokithiri ambao unaitafuna nchi yetu kwa kasi ya kutisha. Anatumia mabilioni yake ya kifisadi kutoa rushwa kwa kiwango cha juu kabisa ili ajiweke katika nafasi nzuri ya kuwa mgombea wa magamba 2015.

Angalia jinsi DHAIFU alivyokuwa anawaogopa wale wote waliombeba kwa michango ya kifisadi, akina (Rostam, Jeetu, Manji, Subhash n.k.) ili kuhakikisha anaangia madarakani. Fisadi Lowassa naye ndio itakuwa hivyo hivyo atakuwa busy kusaini mikataba ambayo haina maslahi kwa Watanzania ili yeye na wapambe wake waendelee kujilimbikizia mali kwa kasi ya kutisha huku wakiwaacha Watanzania walio wengi wakiishi katika ufukara wa kutisha na nchi kurudi nyuma kimaendeleo pamoja na kuwa na rasilimali kubwa zenye utajiri ambao unaweza kabisa kuinua hali ya maisha ya Watanzania walio wengi.


BAK wengi wetu hatutaki kukiri kwamba rushwa nchini mwetu imefikia kiwango cha kijamii na kimfumo. Tatizo tunafikiri kwamba rushwa za wengine ndiyo rushwa za kwetu "tunasaidiana" Unafiki huu utampa Lowassa nchi!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…