Mkwe wa Lowassa ajitosa kuwania nafasi ya U-NEC Arusha

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Kinyang'anyiro Cha uchaguzi Ndogo wa kuziba nafasi mbalimbali zilizoachwa wazi ndani ya CCM Mkoa wa Arusha baada ya makada wake kupata nafasi zingine za Ubunge na udiwani kimeanza kwa kasi baada ya wanachama kadhaa wa CCM kujitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali ikiwemo ya mjumbe wa halmashauri kuu ya Taifa (NEC) mkoa wa Arusha.

Akiongea na waandishi wa habari ofisni kwake jana Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, Musa Matoroka amesema kuwa zoezi la uchukuaji wa fomu lilianza mapema Februari 10 na kumalizika February 13 mwaka huu huku fomu hizo zilitolewa bure Bila malipo.

Akizungumzia nafasi ya NEC Mkoa wa Arusha amesema kuwa jumla ya makada wapatoa 32 akiwemo aliyekuwa mtia nia wa ubunge Jimbo la Arumeru Magharibi, Noel Severe ambaye ni mkwe wa waziri mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowasa wamejitokeza kuchukua fomu na Kati yao 28 ndio wamefanikiwa kurejesha.

Severe, ambaye pia ni Mtoto wa aliyewahi kuwa mkurugenzi wa wanyamapori nchini,Emmanuel Severe ambaye aliwahi kuwa na mgogoro wa kiuongozi na Anthony Diallo jina lake lilikatwa katika kura za maoni za CCM mwaka Jana na kuteuliwa,Noah Lembris ambaye ndiye mbunge wa Arumeru Magharibi kwa Sasa.

Matoroka,Alisema nafasi zingine zinazowaniwa ni Katibu Itikadi na Uenezi wilaya ya Arusha na Karatu ambapo Kati ya wanachama 36 waliochukua fomu wilaya ya Arusha na 34 wamerejesha, huku wilaya ya Karatu waliochukua wakiwa 12 na wote wamerejesha.

Nafasi nyingine inayowaniwa ni Mwenyekiti wa wazazi wilaya ya Karatu na Arumeru ambapo wanachama 5 waliojitokeza kuchukua fomu wilaya ya Karatu na wote wamejeresha na katika wilaya ya Arumeru 10 wakichukua fomu na tisa wamerejesha.

Pia katika wilaya ya Ngorongoro wanachama wa CCM 8 wamejitokeza kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa umoja wa wanawake UWT na wote wamerejesha fomu.

Matoroka ameongeza kuwa baada ya fomu hizo kurejeshwa upembuzi akinifu utafuata ikiwemo baadhi ya nafasi za wagombea fomu zao Itaenda makao makuu ya chama na zingine zitapitiwa na kamati mbalimbali Mkoani hapa na kupanga tareje za uchaguzi.

Ametoa rai kwa makada hao kuacha kujihusisha na vitendo vya Rushwa au kufanya kampeni kabla ya kuruhusiwa na kwamba atakayebainika chama kutafuta jina lake na kumchukulia hatua Kali.

Ends...
 
Kwani ukishika nafasi za ubunge/udiwani hurusiwi kuwa mNEC?
 
Huyu Mama walipokuwa Chadema alipewa Heshima kubwa sana kule..
 
Back
Top Bottom