Upanga Mkali
Member
- Dec 24, 2014
- 96
- 83
.Washambulia kila anayetajwa kwenye urais
.Magazeti ya Mtanzania, Rai yapewa maagizo maalum
KAMBI ya mbunge wa Monduli Edward Ngoyai Lowassa, imeanza kutetereka na tayari hofu ya mgombea wao kupitishwa na vikao vyenye maamuzi ndani ya CCM imetanda.
Inaelezwa, nafasi ya Lowassa kupenya na kuteuliwa katika kinyang'anyiro cha urais kwenye uchaguzi mkuu ujao, ni finyu ukiachilia mbali udhaifu wa afya yake, sifa zinazotajwa kwa mgombea anayehitajika nazo zinamkwaza.
Taarifa kutoka ndani ya kambi hiyo, zinasema kutajwa kwa Waziri wa Miundombinu, John Magufuli, Jaji mstaafu Agustino Ramadhani, kumemtisha Waziri Mkuu huyo aliyejiuzulu kwa kashfa ya RICHMOND na kukwamisha zoezi lake la kutangaza nia ya urais kama ilivyoelezwa kwamba angefanya hivyo 19, Februari.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Arusha, baadhi ya watu wanaomuunga mkono mbunge huyo wa Monduli wakiwemo baadhi ya vijana wa CCM, tayari waliingia mjini Arusha kuanzia 18 Februari kwa ajili ya kuhudhuria zoezi hilo lililotarajiwa kufanyika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
"Kusema ukweli hali ni mbaya, mzee ameanza kukata tamaa ya urais kutokana na watu wanaotajwatajwa, kuwa na sifa zinazohitajika na chama ikiwemo uadilifu, sasa mzee wetu hana hiyo sifa na inajulikana hilo kwa watanzania wote"
"Ndio maana kuna ukimya fulani, hata kwenye mitandao wengine tumeanza kupunguza mashambulizi maana hali haieleweki kamanda na unaweza kumtukana mtu kumbe ndiye rais ajaye halafu ikawa tabu" alisema kijana mmoja kutoka mkoani Mara, ambaye amekuwa akijitambulisha kuwa ni mmoja wa wasuka mipango wa kambi hiyo.
Kijana huyo ambaye mara zote amekuwa akijitambulisha kuwa ni Mkuu wa Wilaya mtarajiwa wa wilaya moja Mkoani Mtwara kwenye serikali ya Lowassa, hivisasa anadaiwa kutafuta ukaribu na makada wengine wa CCM wanaotajwa kwenye mbio za urais.
Taarifa zaidi zinasema, katika kuhakikisha Lowassa anabaki kwenye chati ya urais, msemaji wake Hussein Bashe ambaye anaonekana kupambana kuhakikisha anaokoa jahazi, ametoa maagizo kwa gazeti la Mtanzania na Rai, linalomilikiwa na Rostam Aziz, kuhakikisha waandishi na wahariri wa gazeti hilo wanashambulia watu wanaowadhani ni kikwazo kwa mgombea wake (Lowassa).
Inaelezwa waandishi wanaopeleka habari zinazomsaidia Lowassa, mbali na mshahara wanaolipwa, wameongezewa posho kwa ajili ya kazi hiyo, hivyo imewapa hamasa waandishi wengi kutafuta habari za watu hao na wakati mwingine wamekuwa wakitengeneza habari za uongo ili wapate chochote.
"Bashe ametoa maelekezo kwamba, tumpiganie bwana mkubwa maana hali imeanza kuwa mbaya, anasema mabosi wake wamempa maagizo ya kuhakikisha kila anayeonekana kikwazo kwenye harakati zao, ashambuliwe na kila anayefanya kazi hiyo aongezewe maslahi" alisema mmoja waandishi ambaye pia ni kiongozi wa CCM anayedaiwa kuwa njiani kuhamia kwenye kambi ya mbunge wa Mtama, Bernard Membe anayetajwa kwenye mbio za urais.
Mwandishi huyo alisema, tayari gazeti hilo limemshambulia Jaji Agustino Ramadhani siku chache baada ya kutajwa kuwa miongoni mwa warithi wa Rais Kikwete, mwingine ni John Magufuli na mara kadhaa wamekuwa wakiandika habari mbaya juu ya Waziri Membe.
Inaelezwa, hata chanzo cha Lowassa kushindwa kuhudhuria msiba wa mama wa Jaji Ramadhani, ni kukwepa aibu baada ya gazeti hilo kumshambulia jaji huyo mstaafu na minong'ono msibani hapo ikadai yalikuwa ni maelekezo ya Lowassa.
"Maagizo yaliyotolewa hivisasa ni kumshambulia Prof. Muhongo na kuna mwandishi anaitwa Evans amepewa kazi maalum ya kuhakikisha anapata taarifa za Muhongo baada ya akina Bashe kudhani pengine anaweza kujitosa kwenye urais"
Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi umebaini tayari kambi hiyo ya Lowassa imeishiwa mbinu za kumsaidia mgombea wao kupenya kwenye kinyang'anyiro cha urais, na kazi iliyobakia ni kufanya vurugu na kushambulia makada wa chama hicho wanaotajwa kwenye urais.
Hivi karibuni, kambi hiyo imepata pigo kubwa kufuatia kukanushwa kwa kila taarifa ambazo zinasambazwa na vyombo vya habari kwa lengo la kumjenga Lowassa, ambapo habari iliyokanushwa kwa nguvu kubwa ni madai ya wabunge 150, kumuunga mkono mbunge huyo wa Monduli.
Habari nyingine ni ile iliyodai wanachuo wa IFM kumuunga mkono Lowassa, madai ambayo yamekanushwa na serikali ya wanafunzi wa chuo hicho.
Inaelezwa, watu wanaohusika na masuala ya kusuka propaganda ndani ya kambi hiyo, wamekuwa na uwezo mdogo wa kufanya kazi hiyo na kujikuta wakimpotosha Lowassa kwa taarifa za uongo ili waendelee kulipwa mishahara minono wanayolipwa, na badala ya kumsaidia, wanammaliza.
"Hawa jamaa akina Hemed (Hemed Ally) na wenzake wameshindwa kazi kabisa, wanasambaza propaganda za kitoto kabisa wanadai eti kuna wabunge 150 wanamuunga mkono Lowassa wakati ukweli ni wabunge 15 tu na wengine wameshamkana, huu ni utoto, tatizo wanalipwa hela nyingi sana, sasa hawataki kuzipoteza ndio maana wanatunga hata uongo ili waonekane wanafanyakazi" alisema kada wa CCM ambaye alizungumza na mwandishi wa habari hizi jirani na ofisi ndogo za CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo, kwa upande mwingine baadhi ya wapambe wa Bashe, ambao bado wanaamini Lowassa anaweza kuwa rais, wamekuwa wakijigamba kwamba hakuna ‘mpuuzi' yeyote anayeweza kukata jina la Lowassa na wamekuwa wakitoa matusi ya nguoni dhidi ya Rais Jakaya Kikwete na familia yake.
Aidha, wapambe hao wamekuwa wakitishia baadhi ya watu wanaomshambulia Lowassa.
Chanzo: ...