Ibrahim K. Chiki
JF-Expert Member
- Apr 5, 2011
- 594
- 163
Hivi karibuni kumekua na ukaguzi wa mashirika ya umma unaofanywa na kamati ya bunge. Ni kweli kwamba kamati hizo zimefanikiwa kuibua madudu mengi ndani ya mashirika ya umma. Kwa mfano swala la tbs, ila cha kushangaza ni kwamba pamoja na ushahidi wa kamati hizi kutosheleza bado watuhumiwa hawajawajibishwa, zaidi tunaona wakiumbuliwa na kupata vigugumizi tuu mbele ya tv na magazeti. Inapaswa wawajibishwe ili kupisha sheria kuchukua mkondo wake na siyo blah blah tuu za kwenye media. Nawasilisha wadau.