Kamati yaundwa kurekebisha STAMICO | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamati yaundwa kurekebisha STAMICO

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Rutashubanyuma, Jan 21, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 21, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 414,924
  Trophy Points: 280
  Kamati yaundwa kurekebisha STAMICO


  Na David John

  SERIKALI imeunda kamati ya watalaamu ya kurekebisha Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) ambalo ufanisi wake umekuwa hafifu.Hatua imeelezwa kuwa
  inalenga kuboresha, kusimamia na kuendeleza rasilimali za madini nchini kwa kuzingatia sheria ya madini ya mwaka 1977.

  Hayo yalizungumzwa jana Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Bw. David Jairo wakati akizundua Kamati ya Wataalamu ya Kurekebisha STAMICO.

  Bw. Jairo alisema kuwa shirika hilo lilikuwa ndiyo nguzo kwa maendeleo ya taifa katika sekta ya madini tangu lilipoanzishwa mwaka 1972.

  Kwa mujibu wa Katibu Mkuu huyo, mwaka 1980 serikali ilianza sera za kubinafsisha mashirika ya umma pamoja na zilizokuwa kampuni za umma, lakini shirika hilo kwa kutambua uwezo wake, lilitolewa katika mpango huo wa ubinafsishwaji.

  Alisema shirika hilo lina mchango mkubwa katika kuimarisha uchumi wa nchi, hivyo kwa kuzingatia hilo, Serikali imeamua kuliunda upya kutokana na mtazamo wa sura nyingi za zamani ili kuleta ufanisi.

  Bw. Jairo alisema kwa sasa shirika linahitaji wataalamu ili kuweza kukabiliana na changamoto zilizopo ikiwa ni pamoja na kuajiri vijana wa Kitanzania wenye uwezo wa fani mbalimbali.

  Alisema sheria ya migodi ya mwaka 2010 ilitoa fursa kwa Serikali kushiriki kiuwekezaji katika migodi, lakini hisa zote zitasimamiwa na STAMICO.

  Majukumu mengine ambayo shirika hilo litasimamia ni pamoja na kuwaendeleza wachimbaji wadogo wadogo.

  Bw. Gray Mwakarukwa ambaye ni Mkurugenzi wa Shirika hilo alisema kwa kuwa shirika linafufuliwa upya, linahitaji msingi imara wa mtaji na kwamba msingi huo wa mtaji utakuwa na maana kama kutaandaliwa mpango wa utekelezaji wa muda mrefu na mrefu.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 21, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 414,924
  Trophy Points: 280
  tatizo la serikali yetu ni kutojifunza kutokana na historia yetu................Sisi ni wabia wa Mwadui DIamonds lakini hakuna tunachovuna kule..............sasa huu ushiriki wa migodi kwa serikali kunaelekea zaidi kuvuta pumzi ya waporaji kuendeleza game yao..........................ya uporaji..........................serikali kupita STAMICO ingelibaki katika kupanga, kusimamaia na kudhibiti sera na wala siyo umiliki wa migodi.......................
   
 3. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #3
  Jan 21, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  De'Javu ,ufisadi game reloaded,tunaanza tena ufisadi kwa style ya kisasa zaidi,tanzania nchi yangu nakupenda sana lakini watuongozao wanatuvunja moyo
   
Loading...