Kamati ya Zitto yatabiri kifo cha TBC | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamati ya Zitto yatabiri kifo cha TBC

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mtoboasiri, May 25, 2011.

 1. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #1
  May 25, 2011
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Kamati ya Zitto yatabiri kifo cha TBC
  NA RICHARD MAKORE
  24th May 2011  Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), imesema Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) liko hatarini kufirisika na kufa kama ilivyotokea kwa mashirika mengi ya umma hapa nchini kwa kuwa kumebainika kuwepo kwa matumizi mabaya ya fedha pamoja na kushindwa kukusanya madeni yanayofikia Sh. bilioni 4.8.
  Kadhalika, kamati hiyo imeshangazwa na TBC kuingia mkataba wa kufanya biashara na kampuni ya Star Media bila kuijulisha Wizara ya Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo ambayo shirika hilo lipo chini yake.
  Mjumbe wa kamati hiyo ambaye ni mbunge wa Jimbo la Mwibara mkoani Mara (CCM), Alphaxard Lugola alisema matumizi mabaya ya fedha kunatishia kuliua shirika hilo la umma.
  Alisema TBC lilipoanza wakati huo likiitwa TVT lilikuwa likienda vizuri lakini bahati mbaya hivi sasa linaelekea kufirisika na hatimaye kufa kabisa.
  “Kwa mwenendo huu wa mahesabu TBC halina muda mrefu kuendelea kuwepo kwa kuwa mmeshindwa kudhibiti matumizi yenu pamoja na kuwa wakali katika kukusanya madeni yenu” alisema.
  Aliongeza kuwa baada ya kusoma vitabu vya mahesabu ambavyo vilikabidhiwa kwa kamati alibaini kwamba Shilingi bilioni nane zilitumika kununua mafuta ya magari bila kufuata taratibu za manunuzi.
  Alikiri kuwa hakuna uhalali wotote wa matumizi ya fedha hizo kwa ajili ya kujaza mafuta ya magari katika kituo cha mafuta cha Victoria cha jijini Dar es Salaam.
  Alisema makubalinao ya mkataba wa kujaza mafuta hayo yalifanywa kwa mdomo badala ya maandishi kama sheria na taratibu za manunuzi ya serikali zinavyosema.
  Kuhusu mkataba kati ya TBC Star Media, wajumbe hao walisema ulisainiwa kirafiki bila hata wizara inyosimamia shirika hilo kujulishwa.
  Baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo walihoji kwa nini TBC inazidi kuporomoka badala ya kupanda kama ilivyoanza huko nyuma.
  Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Ludewa, Deo Filikunjombe, aliiambia kamati hiyo kuwa siku za TBC kuendelea kuwepo zinahesabika.
  Alisema TBC inakabiliwa na uhaba wa fedha za kuiendesha hatua ambayo imeanza kusababisha matatizo ikiwemo Televisheni yake kushindwa kufika baadhi ya mikoa hapa nchini.
  Kwa upande wake, uongozi wa TBC ulikiri kuwa matangazo yao hivi sasa hayawafikii wananchi wengi kutokana na mitambo yake kuchakaa na kwamba hakuna fedha za kuweza kununua mipya.
  Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Clement Mshana alijaribu kutoa majibu kwa kamati hiyo lakini mara kadhaa wajumbe wake walimkatisha baada ya kuhisi kama yalikuwa hayajitoshelezi.
  Kuhusu ukusanyaji wa madeni ya TBC kutoka taasisi za umma, Mshana alisema wameajiri kampuni ya udalali ya Majembe kwa ajili ya kufanya kazi hiyo.
  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #2
  May 25, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135

  Yaani huu ni wizi mchana kweupeeeeee yaani Tshs 8,000,000,000 kwa ajili ya mafuta? Unajua ukichukua hiyo no. ukagawa kwa siku 365 (mwaka) in maana TBC inatumia shilingi 21,918,000 kila siku kununulia mafuta, karibu milioni ishirini na mbili tena kwenye kituo kimoja. This can never be true na kama ni kweli is typical madness!!!!!!
   
 3. T

  The Priest JF-Expert Member

  #3
  May 25, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 1,026
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Sasa Tido alikuwa anafanya nini hapo Tbc,yaani hii ni hatari kwa taifa,media ya taifa kufilisika?ndio tunarudi nyuma tena kutegemea vyombo vya habr binafsi..
   
 4. w

  wasp JF-Expert Member

  #4
  May 25, 2011
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 206
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wacha ife maana ni TV ya Chama Cha Magamba
   
 5. s

  siame jg New Member

  #5
  May 25, 2011
  Joined: Apr 21, 2009
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Matumizi hayo ya mafuta ni baada ya kumtoa Tido au ??????
   
 6. J

  Japhet Mosi JF-Expert Member

  #6
  May 25, 2011
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 207
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakuna cha Tido Mhando bali ni wizi maana hawana magari ya kuweza hata kujazwa mafuta ya TZS 5m kwa siku na mishahara ya staff siyo mikubwa. Tupate maelezo ya kina hizo TZS 8 blillion zimetowekaje? Kama hizo fedha zilipelekwa kwenye kampeni za CCM uchaguzi mkuu October 2010 tuelezwe kinagaubaga.
   
 7. samito

  samito JF-Expert Member

  #7
  May 25, 2011
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 621
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  wanao filisi ni hao hao viongozi wanapoitwa kwa ajili ya kufanya mahojiano yoyote pale wanataka wapewe mafuta ya magari yao na allowance. Pale kila mtu alikuwa anataka kula ndio shida...

  Waswahili wanasemaaa "Mwenda tezi na omo hurejengea ngamani" tutarejea ngamani ITV na STAR TV

  Uganda M7 kawatimua wakurugenzi na bod of directors wote wa tv ya taifa UBC kwa ajili ya mambo kama hayo, kisa walinunua gari second hand afu kwa mabilion ya pesa na sasa alifanyi kazi istoshe hawampi mzee coverage ya kutosha, eti wanampendelea Besigye
   
 8. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #8
  May 25, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  kama CCM inakufa acheni na TBC ife maana haina manufaa yoyote kwa wananchi.
   
 9. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #9
  May 25, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  kufaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
  mumemtoa Tildo kwa dhuluma ni bora kufaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa tu
   
 10. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #10
  May 25, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Hii habari inanipa maswali:
  1. TBC wana magari mengi na majenereta makubwa kiasi cha kutumia mil 22 kila siku?
  2. Kama jibu la (1) ni hapana, je kuna uuzaji wa mafuta unaofanywa na TBC wakishayachukua toka Victoria?
  3. Kama jibu la (2) ni hapana, je Victoria service station inatumika kufisadi pesa za umma??
  4. Kama jibu la (3) ni ndiyo, implication zake ni zipi kwa mmilki wa Victoria (Bw. Harrod) kujitambulisha kuwa ni mtumishi wa Mungu na Kufungua kanisa pale??

  Mzee Harrod anatakiwa ajitokeze kusema kama kweli alilipwa hayo mabillioni au ni ujanja wa kimahesabu umefanywa ndani ya TBC.

  Miaka ya nyuma nimewahi kuwa naweka mafuta pale kwa bill, nilikuwa nalipa kwa mwenzi na tuliandikishana. Iweje taasisi kubwa kama TBC wapeane biashara ya billion 8 kwa makubaliano ya mdomo tu.
  Hii ni kusema kwamba TBC kujipendekeza kwa watawala ni kwa masilahi yao zaidi kuliko yale ya watawala maana wakiwa critical kwa watawala ya kwao yatafumuliwa.

  Kwa uchafu huu bado ule wimbo wa "Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote" una mantiki au tuupeleke makumbusho ya taifa???
   
 11. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #11
  May 25, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  NI BORA IFE TU kwanza hamna cha maana nimekiona tbc zaidi ya kukopi tu!Niko kwenye maombi ya kuiua TBC ,HAMNA KITU PALE NI UJINGA MTUPU!
   
 12. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #12
  May 25, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,481
  Likes Received: 12,756
  Trophy Points: 280
  Yani huwa nairuka hii station pamoja na ile redio ya kibondo total crap!
   
 13. L

  Ludewa JF-Expert Member

  #13
  May 26, 2011
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 215
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mambo yote hayo yamefanyika wakati wa utawala wa tido mhando.
   
 14. Mpandafarasi

  Mpandafarasi Member

  #14
  May 31, 2011
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Si tu kuiacha ife, bali wahusika watuambie hayo mabilioni wametumiaje?
   
 15. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #15
  May 31, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Maskini Mshana - alidhani amepata kumbe amepatikana!
   
 16. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #16
  May 31, 2011
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  TBC ni TV ya serikali.
   
 17. Mkubwa ndevu

  Mkubwa ndevu JF-Expert Member

  #17
  May 31, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 755
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Naomba nipewe maiti ya TBC kuizika nina kaburi kubwa itaingia huku shy town la futi 32 urefu na upana futi 16 ulale mahali pema TBC
   
 18. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #18
  May 31, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Kikwete anajisikiaje mashirika muhimu kama ATCL,TRL na TBC yote yanateketea wakati wa utawala wake? Tuombe Mungu muungano usife mikononi mwake; itakuwa noma!!
   
Loading...