Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Bunge ina Maswali magumu ya kujibu

Mzalendo2015

JF-Expert Member
Aug 14, 2012
6,697
9,048
Haya ni maswali yanayotakiwa kujibiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Bunge.
Kwamba watu wasiojulikana waliwezaje kupenya mpaka ndani ya Viwanja vya Bunge wakimfuatilia Mhe. Tundu Lissu na dreva wake bila ya kutambuliwa getini au kizuizi chochote?? Lakini pia waliwezaje kupenya mpaka kwenye Makazi ya Waheshimiwa Wabunge bila ya kujulikana au kuonekana na mtu yeyote?

Baada ya kufanya shambulio la mauaji waliwezaje tena kutoroka kwa kupitia milango/mageti au maeneo au njia hiyo hiyo bila ya kizuizi wala kutambuliwa na mtu yeyote? Lakini jambo la kujiuliza pia ni kwamba ilikuwaje SMG ilipokuwa inakohoa(kutoa mlio wa bunduki kwa risasi 38)haikuweza kuwashtua wakazi wa maeneo ya jirani na makazi ya Waheshimiwa Wabunge. Je, hizo Bunduki walizotumia hawa wauaji zilikuwa na viwambo(Silencers)zinazozuia mlio au mwangwi wa risasi....??

Je, hakuna Mtandao wa Kamera (CCTV-Closed Circuit Television)kwenye viwanja vya Bunge na Makazi ya Waheshimiwa Wabunge ambazo zingeweza kuonyesha picha za Watu WASIOJULIKANA?? Kama zipo Je, ni mbovu au zilizimwa? Kama zilizimwa nina nani alizizima na alielekezwa na nani..?

Naomba Waheshimiwa Wabunge wote bila ya kujali itikadi za vyama vyeo waihoji Kamati yao ya Ulizni na Usalama inayohusika na Ulinzi wao ndani na nje ya Bunge. Kama wataingiza ushabiki wa ki-CCM kuna siku Al-Shaabab au Al-Qaeda wataingia viunga vya Bunge la Tanzania na kuwalipua wote kwa Bomu la muhanga mkiwa ndani ya Bunge maana hakuna ulinzi.

Naomba kuwasilisha.
 
Kama FFU waliofungua geti la viongozi na kuruhusu gari isiyo na plate namba ipite hadi sasa bado hawajakamatwa na kuhojiwa mjue hakuna upelelezi unaofanyika kilichopo ni kiini macho tu kinachoendelea. Ninavyojua lile geti la kuingia Area D upande wa nyumba za viongozi dodoma hulindwa 24/7 na FFU.

USHAURI:

Chadema, nafikiri mnalielewa jeshi letu la polisi jinsi linavyofanya kazi, mlipuaji wa bomu Arusha aliyerusha bomu mbele yenu na watu wakaanza kumfukuza ameshapatikana?

Nawashauri, kama mna MEANS zingine za kupeleleza na kumpata mhusika anzeni sasa kufanya mipango hiyo otherwise mwachieni Mungu a deal na mhusika. Msitegemee eti wahusika halisi watakuja kukamatwa na polisi hii, sana sana polisi kwa nia ya kujisafisha na kuwaridhisha watawaletea wahusika ambao sio.

Pambaneni na hali zenu.
 
Kikubwa tuendelee kumuombea uzima mwamba TL ili atakaporudi labda tuanzie apo maana hawa wengine tayari wameonyesha kutoweza kuwatambua hawa watu wasiojulkana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa hv polisi nao wanashinda humu kwenye mitandao ya kijamii wanafuatilia tu na kupima upepo kama watu wameanza kisahau. Maswali magumu kama haya hawayapendi kabisa maana yanaacha wazi nia ovu na kuwastua waliolala. Hiyo kamati ya ulinzi na usalama ya bunge huwa ipo kichama zaidi, kama tatizo halijamkuta mwanaccm kwao halina maana maana , kwao tatizo likimkuta mbunge wa upinzani ni haki yake haswa mbunge mwenyewe kama ni Lissu.
 
Kwa wabunge wa CCM:

"Wakimaliza" kuua wapinzani mtaanza kuuwawa ninyi wabunge wa CCM mtakaoonyesha chembechembe za "dissent"

Hapo ndipo akili zitawakaa sawa lakini mtakua mmeshachelewa maana hamtakuwa na wa kuwasemea. Mtanyamazishwa kwa jinsi upinzani unavyonyamazishwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo kwenye CCTV na walinzi wa mageti tu tukivipata tayar kazi imekwisha!
 
Kama FFU waliofungua geti la viongozi na kuruhusu gari isiyo na plate namba ipite hadi sasa bado hawajakamatwa na kuhojiwa mjue hakuna upelelezi unaofanyika kilichopo ni kiini macho tu kinachoendelea. Ninavyojua lile geti la kuingia Area D upande wa nyumba za viongozi dodoma hulindwa 24/7 na FFU.

USHAURI:

Chadema, nafikiri mnalielewa jeshi letu la polisi jinsi linavyofanya kazi, mlipuaji wa bomu Arusha aliyerusha bomu mbele yenu na watu wakaanza kumfukuza ameshapatikana?

Nawashauri, kama mna MEANS zingine za kupeleleza na kumpata mhusika anzeni sasa kufanya mipango hiyo otherwise mwachieni Mungu a deal na mhusika. Msitegemee eti wahusika halisi watakuja kukamatwa na polisi hii, sana sana polisi kwa nia ya kujisafisha na kuwaridhisha watawaletea wahusika ambao sio.

Pambaneni na hali zenu.
This is what they call GREAT THINKING

si sisiemu si sidiem ila ni MKEREKETWA
 
Hapo kwenye CCTV na walinzi wa mageti tu tukivipata tayar kazi imekwisha!
Hao ni wal wale wanapita popote kwa "kazi maalum"..... wana ID zao kabisa zile zile!! Wal walitumwa na aliowatuma! Stop killing........innocents.....you ..are a killer
 
Mh. Tundu Lissu na dereva wake ndio mashahidi muhimu zaidi katika tukio hili. Bila kuwahoji hawa Kamati itakuwa inatwanga maji kwenye kinu.
Kumuhoji mwenye premio... maana NAPE kasema hiyo Premio imekuwa ikiwafuatilia wabunge wengine pia
 
Back
Top Bottom