Kamati ya Mwinyi yaonywa Dodoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamati ya Mwinyi yaonywa Dodoma

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Nov 2, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Nov 2, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,572
  Likes Received: 82,101
  Trophy Points: 280
  Kamati ya Mwinyi yaonywa Dodoma Monday, 02 November 2009 07:47 *Yatakiwa isilenge kuziba midomo wabunge
  *Wabunge waapa hatutaburuzwa na serikali

  Na John Daniel, Dodoma
  Majira

  BAADHI ya wabunge wameonya kuwa iwapo Kamati ya Mwinyi inayokutana nao leo itakuja na sura ya kutaka waburuzwe na serikali Rais Jakaya Kikwete ajiandae CCM kupasukia mkononi mwake.

  Wabunge hao wametoa onyo hilo kamati hiyo ikiwa tayari imekutana na Kamati ya Uongozi ya Wabunge wa CCM chini ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na badaye kukutana tena na Kamati ya Uongozi ya Bunge chini ya Spika, Samuel Sitta kwa nyakati tofauti kwa lengo la kupata picha na kujua uelekeo wa kikao cha leo cha wabunge wote wa chama hicho.

  Kamati hiyo iliundwa na Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kwa lengo la kuchunguza mahusiano baina ya wabunge na serikali yao, hasa baada ya kauli ya za wabunge hao bungeni kuwakera viongozi wa serikali na wa chama hicho.

  Wakizungumza na Majira kwa nyakati tofauti jana, baadhi ya wabunge walisema lengo la kamati ni kuwaziba midomo ili kuacha hoja za msingi
  zinazotakiwa kujibiwa na serikali kwa ufasaha badala yake wakubali kuburuzwa jambo,ambalo limepitwa na wakati.

  "Hivi sasa tunasubiri majibu ya serikali kuhusu Richmond, huku TAKUKURU inataka kutuziba midomo, huku Kamati ya Mhe. Mzee Mwinyi nayo inataka kutuziba midomo, haya mambo tusipoyaangalia kwa makini wakati wa CCM kugawanyika mkono mwa JK umefika, kwanza kuwepo kwa kamati hii ni kuficha ukweli, chanzo cha tatizo kinajulikana lakini hawataki kukishughulikia, wananazunguka.

  "Chanzo cha tatizo ni kwamba kumejitokeza kundi dogo tu ndani ya CCM lenye nguvu ya fedha haramu, lenye lengo la kukibinafsisha au kukiendesha chama kama kampuni ya mtu binafsi, inapotokea wenye uchungu na nchi kuona hilo na kulipinga kwa nguvu zote matokeo yake ni kuundwa kwa kamati badala ya kushughulikia chanzo cha
  tatizo," alisema mbunge mmoja.

  Mbunge mwingine machachari wa CCM alisema yeye kama mwakilishi wa wananchi anasikitishwa na hali iliyopo ndani ya CCM ya sasa ya kuacha hoja za msingi na kupoteza muda kwa lengo la kuficha ukweli.

  "Ninachoweza kuzungumza kwa sasa ni kwamba tunasubiri sana hiyo Kamati ya Wazee wetu kesho (leo), ila tunasikitika sana kwamba tunapoteza muda wa kulumbana badala ya kung'oa mzizi wa fitna, tatizo linajulikana, kinachotusumbua ni kutokubali kuwa wawazi na wakweli.

  Hoja zinazotarajiwa kutawala mkutano ni pamoja na kuwepo kwa uhasama baina ya wabunge wa CCM, vikao vya CCM kushindwa kushughulikia matatizo ndani na kuyaweka hadharani bungeni na bunge kutumika kama rungu la kupiga serikali pamoja.

  Habari kutoka ndani ya Kikao cha Kamati na ile ya Uongozi wa Bunge, zilieleza kwamba kulikuwa na mjadala mkali kuhusu hoja hizo huku baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo wakiweka wazi kwamba kinachotakiwa ni kushughulikia matatizo si watu.

  Ilielezwa kwamba kikao hicho kilikuwa na mvutano mkali huku baadhi ya wajumbe wakionya kamati hiyo kwamba iwapo haitasoma alama za nyakati uenda kikao cha leo kitakuwa kigumu zaidi na hata kuweza kuvunjika kwa kuwa wabunge wanatambua kuwa kilichopo nyuma ya kamati hiyo ni kutaka
  kuwanyamazisha.
   
 2. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #2
  Nov 3, 2009
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,203
  Trophy Points: 280
  Nakumbuka siku moja nimekwenda kumtembelea JK.[JK Maana yake Jakaya Kikwete].
  Halafu nikamwambia kwamba,I said to him,I will paraphrase what I said to him,''paraphrase'',yaani,siyo hasa maneno niliyotumia,lakini,hiyo ndiyo maana yake.
  Nikamwambia,''Uchaguzi Mkuu unakaribia,utakuwa ni Uchaguzi Mkuu wa kwanza katika ambao takuwa ni Multiparty. Baada ya miezi mitatu watu watapiga kura. Lakini,ni ajabu kwamba ni Watanzania wachache sana wanaweza kusema kwamba wana fununu yoyote,ni nani anaweza kuwa Rais.'' JK akanitazama kwa mshangao. Hili lilikuwa ni jambo ambalo alikuwa hajalifikiria,ati kwamba kulikuwa na tatizo lolote katika election process jinsi ilivyokuwa inakwenda.
  Halafu mimi nikaamka kuondoka,na JK Alipokuwa anniaga pale nje,ilikuwa ni dhahiri alivyokuwa anavyofikiria,kwamba'' huyu mtu ni fake,why did it take me such a long time to notice it?''
  Baada ya hapo sikuonana na JK tena,mpaka baada ya muda mrefu nilipokuwa nyumbani Msasani alipofika Magige[ndugu yangu Magige]kutoka Butiama na kuniambia kwamba,''inaelekea kwamba rafiki yako Jakaya Kiwete amekaribia kuichukua nchi.'' Mimi nilistaajabu sana ,all this was news to me.
  Mwalimu alikuwa amemuagiza Magige,kwamba aulize kuhusu political situation ilivyo Dar es Salaam,aulize watu,lakini asiwafahamishe kwamba anawauliza kwa madhumuni gani,halafu akamwambia,''be sure to question Andrew.'' Kwa hiyo mimi sijui kama nilisema jambo lolote ambalo lilipelekea Mwalimu kuchukua maamuzi aliyofanya wakati ule.
   
 3. M

  Mkandara Verified User

  #3
  Nov 3, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  "Chanzo cha tatizo ni kwamba kumejitokeza kundi dogo tu ndani ya CCM lenye nguvu ya fedha haramu, lenye lengo la kukibinafsisha au kukiendesha chama kama kampuni ya mtu binafsi, inapotokea wenye uchungu na nchi kuona hilo na kulipinga kwa nguvu zote matokeo yake ni kuundwa kwa kamati badala ya kushughulikia chanzo cha
  tatizo," alisema mbunge mmoja.


  Mbunge huyu kafunga Mjadala!
   
 4. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #4
  Nov 3, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  mhh......
   
 5. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #5
  Nov 3, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kama hao wabunge wanajua CCM imeoza...si watoke huko!! Wanasubiri nini?
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Nov 3, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,572
  Likes Received: 82,101
  Trophy Points: 280
  Mkuu mimi nadhani waache wapambane humo humo mpaka kieleweke labda ile CCM tuliyoifahamu miaka ile inaweza kuibuka tena kama mafisadi watashindwa lakini kama wapiganaji wakishindwa basi huko tuendako kuna uwezekano mkubwa wa nchi kuingia kwenye matatizo ya kutisha.
   
Loading...