Wito umeendelea kutolewa kutoka sehemu mbalimbali duniani kwa serikali ya Tanzania kutoa ufafanuzi kamili kuhusu hatma ya mwandishi habari Azory Gwanda baada ya waziri ya mambo ya nje nchini, Profesa Palamagamba Kabudi, kusema katika mahojiano na BBC kwamba 'Azory Gwanda aliyetoweka ameshafariki'.
Kamati ya kuwalinda waandishi wa habari CPJ imeeleza kwamba tangu kutoweka kwa mwandishi huyo wa kujitegemea, serikali ya Tanzania haijatoa taarifa zaidi baada ya kuahidi kuchunguza mkasa wa kupotea kwake.
"Kwa mwaka mmoja na nusu familia ya Azory Gwanda na vyombo vya habari Tanzania, wameiomba serikali kufafanua kilichomfika mpendwa na mfanyakazi mwenzao bila mafanikio, halafu ghafla, Waziri wa Mambo ya Nje anataja kwamba mwandishi huyo amefariki. Hili kwa jumla haliridhishi na linatia wasiwasi. Ni lazima serikali itoe taarifa nzima kwa umma kuhusu hatma ya Gwanda." amesema Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa CPJ Robert Mahoney, New York.
Gwanda alitoweka mnamo Novemba 21 2017, baada ya uchunguzi kuhusu maujai ya kiholela na yasioeleweka na kupotea kwa watu katika pwani ya wilaya ya Kibiti.

Tanzania yashinikizwa kutoa ufafanuzi kuhusu Azory Gwanda - BBC News Swahili
Serikali ya Tanzania yashinikizwa kutoa ufafanuzi kuhusu 'kifo' cha mwandishi habari aliyetoweka Azory Gwanda.
www.bbc.com