Kamati ya kudumu ya bunge yapigwa butwaa Shinyanga, ni kuhusu kutokuuzwa mahindi kwa wananchi!

SULEIMAN ABEID

JF-Expert Member
Feb 26, 2013
390
385
SERIKALI imeshauriwa kuangalia uwezekano wa kuanza kuuza mahindi yaliyohifadhiwa katika maghala ya wakala wa Taifa wa Hifadhi ya chakula nchini (NRFA) ambayo baadhi yake yapo katika hatari ya kuanza kuharibiwa na wadudu waharibifu wa mazao.

Ushauri huo umetolewa juzi mjini Shinyanga na wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji, Kilimo na Mifugo iliyokuwa ikitembelea miradi mbalimbali iliyopo chini ya kamati hiyo inayotekelezwa mkoani Shinyanga.

Mbali ya hofu ya kuharibika kwa mahindi hayo ambayo kumbukumbu zinaonesha yalinunuliwa katika msimu wa 2014/2015 pia wabunge walishangazwa na kitendo cha serikali kuendelea kuyahifadhi wakati maeneo mengi nchini wananchi wanahitaji chakula cha kununua kwa bei nafuu kutokana na bei hivi sasa kuwa juu.

Wakiwa katika ghala la akiba ya chakula (NRFA) mjini Shinyanga wabunge wa kamati hiyo wakiongozwa na mwenyekiti wao, Mary Nagu walishuhudia sehemu ya magunia ya mahindi yaliyomo ndani ya ghala hilo yakiwa na wadudu na baadhi yake yakitoa ungaunga kuashiria kuanza kushambuliwa na wadudu.

Wabunge walionesha mshangao kutoka na hali waliyojionea ambapo walishangazwa na kitendo cha serikali kuendelea kuhifadhi idadi kubwa ya chakula katika maghala yake huku maeneo mengi nchini ikiwemo wilaya 55 zikiwa na uhaba mkubwa wa chakula na wananchi wakiuziwa debe moja la mahindi kati ya shilingi 20,000 hadi 25,000.

“Mheshimiwa mwenyekiti hii hali inatushangaza, ni ajabu kuona chakula kipo cha kutosha lakini huko nje wananchi wanahangaika na hivi sasa wanauziwa mahindi kwa bei kubwa, lakini cha ajabu haya yaliyopo hapa tumejionea wenyewe yameanza kubunguliwa na wadudu, ipo hatari yataharibika,”

“Katika taarifa ya NRFA wamesema moja ya changamoto waliyonayo ni uhaba wa fedha, hiki ni kichekesho, kwa nini wasiuze mahindi waliyonayo zaidi ya tani 8,000 wakati hali ya soko ni nzuri, ni bora wayauze ili wapate fedha na wanunue mengine mapya,” alieleza Mohamedi Mgimwa mbunge wa Mufindi Kaskazini.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Uzini, Salum Rehani alisema iwapo serikali haitochukua hatua ya kuruhusu kuuzwa kwa mahindi hayo ipo hatari yakakosa soko baada ya wananchi kuanza kuvuna mavuno mapya hivi karibuni na kwamba wanachohitaji wananchi ni chakula cha bei nafuu na siyo cha bure.

Hata hivyo kwa upande wake Kaimu Ofisa mtendaji mkuu wa NRFA, Deusdedit Mpazi alikanusha madai ya mahindi kuwa katika hatari ya kuharibika kwa vile mara kwa mara hufanyika ukaguzi wa kuangalia iwapo hayajaingiliwa wadudu waharibifu.

“Mheshimiwa mwenyekiti si kweli kwamba mahindi haya yapo katika hatari ya kuharibika, hawa wadudu mnaowaona hapa hawana madhara makubwa, ni wadudu visumbufu tu, na hivi karibuni tunatarajia kuanza zoezi la kupulizia dawa, hivyo hayawezi kuharibika kama mnavyohofia,” alieleza Mpazi.

Akizungumzia suala la mahindi hayo kutopelekwa kwa wananchi ili yauzwe kwa bei nafuu, Naibu waziri wa Kilimo, mifugo na uvuvi, Ole Nasha alisema hofu ya serikali ni kuona mahindi hayo yatakapopelekwa kwa wananchi kuangukia kwenye mikono ya walanguzi na kuuzwa kwa bei ya juu.

“Hatukurupuki kusambaza mahindi haya ovyo, tuko makini ili kuhakikisha pale yatakapopelekwa kwa wananchi yanawafikia walengwa husika, lakini pia tunasubiri kipindi halisi cha mavuno ili tuweze kuona kiasi halisi cha mazao kitakachopatikana, na hivyo chakula hiki kitapelekwa kwenye maeneo yenye upungufu mkubwa,” alieleza waziri.

IMG_20170322_115547.jpg

IMG_20170322_115608.jpg
 
Duh!sawa bhana.Maana sasa hivi kula ugali ni anasa,unga kilo moja mpaka 2,200/= halafu mahindi yamerundikwa kwenye maghala wanaona raha kupiga nayo selfie tu.Sababu wanazozitoa ni za kitoto,eti watu wanakufa njaa wao wanasema wanaogopa kuanza kuyasambaza kwani yanaweza kuangukia kwenye mikono ya walanguzi.Kwani wao hawawezi kudhibiti hiyo kitu?Maskini Tanzania yangu,ni nini umemkosea Mungu?
 
hahahahahahahahahaha hizo propaganda tu ili seriakli ya wanyonge ichukiwe na wananchi,kwa nini wanataka cha bei nafuu,waache uvivu wapige kazi wavune cha kwao,hicho ni cha serikali
 
SERIKALI imeshauriwa kuangalia uwezekano wa kuanza kuuza mahindi yaliyohifadhiwa katika maghala ya wakala wa Taifa wa Hifadhi ya chakula nchini (NRFA) ambayo baadhi yake yapo katika hatari ya kuanza kuharibiwa na wadudu waharibifu wa mazao.

Ushauri huo umetolewa juzi mjini Shinyanga na wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji, Kilimo na Mifugo iliyokuwa ikitembelea miradi mbalimbali iliyopo chini ya kamati hiyo inayotekelezwa mkoani Shinyanga.

Mbali ya hofu ya kuharibika kwa mahindi hayo ambayo kumbukumbu zinaonesha yalinunuliwa katika msimu wa 2014/2015 pia wabunge walishangazwa na kitendo cha serikali kuendelea kuyahifadhi wakati maeneo mengi nchini wananchi wanahitaji chakula cha kununua kwa bei nafuu kutokana na bei hivi sasa kuwa juu.

Wakiwa katika ghala la akiba ya chakula (NRFA) mjini Shinyanga wabunge wa kamati hiyo wakiongozwa na mwenyekiti wao, Mary Nagu walishuhudia sehemu ya magunia ya mahindi yaliyomo ndani ya ghala hilo yakiwa na wadudu na baadhi yake yakitoa ungaunga kuashiria kuanza kushambuliwa na wadudu.

Wabunge walionesha mshangao kutoka na hali waliyojionea ambapo walishangazwa na kitendo cha serikali kuendelea kuhifadhi idadi kubwa ya chakula katika maghala yake huku maeneo mengi nchini ikiwemo wilaya 55 zikiwa na uhaba mkubwa wa chakula na wananchi wakiuziwa debe moja la mahindi kati ya shilingi 20,000 hadi 25,000.

“Mheshimiwa mwenyekiti hii hali inatushangaza, ni ajabu kuona chakula kipo cha kutosha lakini huko nje wananchi wanahangaika na hivi sasa wanauziwa mahindi kwa bei kubwa, lakini cha ajabu haya yaliyopo hapa tumejionea wenyewe yameanza kubunguliwa na wadudu, ipo hatari yataharibika,”

“Katika taarifa ya NRFA wamesema moja ya changamoto waliyonayo ni uhaba wa fedha, hiki ni kichekesho, kwa nini wasiuze mahindi waliyonayo zaidi ya tani 8,000 wakati hali ya soko ni nzuri, ni bora wayauze ili wapate fedha na wanunue mengine mapya,” alieleza Mohamedi Mgimwa mbunge wa Mufindi Kaskazini.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Uzini, Salum Rehani alisema iwapo serikali haitochukua hatua ya kuruhusu kuuzwa kwa mahindi hayo ipo hatari yakakosa soko baada ya wananchi kuanza kuvuna mavuno mapya hivi karibuni na kwamba wanachohitaji wananchi ni chakula cha bei nafuu na siyo cha bure.

Hata hivyo kwa upande wake Kaimu Ofisa mtendaji mkuu wa NRFA, Deusdedit Mpazi alikanusha madai ya mahindi kuwa katika hatari ya kuharibika kwa vile mara kwa mara hufanyika ukaguzi wa kuangalia iwapo hayajaingiliwa wadudu waharibifu.

“Mheshimiwa mwenyekiti si kweli kwamba mahindi haya yapo katika hatari ya kuharibika, hawa wadudu mnaowaona hapa hawana madhara makubwa, ni wadudu visumbufu tu, na hivi karibuni tunatarajia kuanza zoezi la kupulizia dawa, hivyo hayawezi kuharibika kama mnavyohofia,” alieleza Mpazi.

Akizungumzia suala la mahindi hayo kutopelekwa kwa wananchi ili yauzwe kwa bei nafuu, Naibu waziri wa Kilimo, mifugo na uvuvi, Ole Nasha alisema hofu ya serikali ni kuona mahindi hayo yatakapopelekwa kwa wananchi kuangukia kwenye mikono ya walanguzi na kuuzwa kwa bei ya juu.

“Hatukurupuki kusambaza mahindi haya ovyo, tuko makini ili kuhakikisha pale yatakapopelekwa kwa wananchi yanawafikia walengwa husika, lakini pia tunasubiri kipindi halisi cha mavuno ili tuweze kuona kiasi halisi cha mazao kitakachopatikana, na hivyo chakula hiki kitapelekwa kwenye maeneo yenye upungufu mkubwa,” alieleza waziri.

View attachment 486030

View attachment 486031

Hii serikali ni kama imepumbazwa vile. Njaa ipo wanasema hakuna njaa, Chakula kingi wanacho wamebania na hawataki kusambaza na wananchi wake wanapata shida. Hii haingii akilini hata kidogo. Wakati mwingi serikali inafanya ndivyo sivyo.

Nina mashaka kabisa kwamba kuna kitu ambacho mimi siwezi kuelewa moja kwa moja kipo ndani ya serikali hii bila ya wao kutambua kama laana hivi. tabisa ya laana ni ndivyo sivyo ndivyo sivyo, si ugonjwa si uzima( haya ni mambo ya kiroho mtu asinihukumu wala kunilaumu).
 
Nakumbuka miezi michache iliyopita taarifa kama hizi ziliitwa ni za uchochezi.

Kweli muda ni hakimu wa haki!
Time always tells,yani watu wanakosa unga halaf wao wamelundika mahindi kwenye maghala yao yanaishia kuharibika2 wakati watu wengine hata hawajui jioni yao itakuwa vipi.Kiukweli hii ni dhambi
 
Halafu wanakataa mahindi kuanza kuharibika wakati kwenye picha unaona wadudu wanavyoyashambulia
 
Hii serikali ni kama imepumbazwa vile. Njaa ipo wanasema hakuna njaa, Chakula kingi wanacho wamebania na hawataki kusambaza na wananchi wake wanapata shida. Hii haingii akilini hata kidogo. Wakati mwingi serikali inafanya ndivyo sivyo.

Nina mashaka kabisa kwamba kuna kitu ambacho mimi siwezi kuelewa moja kwa moja kipo ndani ya serikali hii bila ya wao kutambua kama laana hivi. tabisa ya laana ni ndivyo sivyo ndivyo sivyo, si ugonjwa si uzima( haya ni mambo ya kiroho mtu asinihukumu wala kunilaumu).
umesema vizuri! lakin jitahidi uzi ukiwa mrefu, unapokomenti usikwoti uzi mzima!
 
Nope, serikali ilisema ina reserve ya kutosha, mbunge mmoja akadai ataacha kuwa mbunge iwapo ataonyeshwa hifadhi hiyo

Kabla ya hata huyo Mbunge kusema hivyo (na mpaka leo hawajamwonyesha hizo tani 1.5m za akiba ili ajiuzulu), Serikali ilipiga marufuku kuripotiwa kwa taarifa za njaa. Unakumbuka yule mwandishi wa ITV kule Kagera aliwekwa ndani kwa sababu gani?? Unajua mwisho na aibu iliyowapata watesi wake?

Usiwe msahaulifu ndugu au mwenye kutaka kusikia habari fulani tu. Kwa urahisi wa rejea hebu tafuta majarida na clips za siku zile kauli hizi zilipotolewa ".....Serikali haina shamba....hatutampa mtu chakula ....."
 
Mahindi yana shibongi/dumuzi bado mnayangangania tunanunua debe elfu 20, bado mwezi mmoja mahindi mapya yaive mashambani bado tu mnayatizama tu.

Hayo ya mwaka huu mtayaweka wapi wakati stoo ziko tuti?

Kwasasa mahindi yanayolika nchini yanatoka kenya na uganda yawakulima wetu yalishakwisha siku nyingi bado tunakomoa walaji au tukianza kubadilisha ngombe moja kwa debe moja ndio mtuletee?

Ukienda bandarini meli za waganda zinashinda hapo wakiuza akiba yao ya mahindi tayari kununua msimu mpya, sie tunapiga nayo picha tu, hapa tunahitaji kuimport wanaume tupate mbegu mpya ya watanzania
 
SERIKALI imeshauriwa kuangalia uwezekano wa kuanza kuuza mahindi yaliyohifadhiwa katika maghala ya wakala wa Taifa wa Hifadhi ya chakula nchini (NRFA) ambayo baadhi yake yapo katika hatari ya kuanza kuharibiwa na wadudu waharibifu wa mazao.

Ushauri huo umetolewa juzi mjini Shinyanga na wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji, Kilimo na Mifugo iliyokuwa ikitembelea miradi mbalimbali iliyopo chini ya kamati hiyo inayotekelezwa mkoani Shinyanga.

Mbali ya hofu ya kuharibika kwa mahindi hayo ambayo kumbukumbu zinaonesha yalinunuliwa katika msimu wa 2014/2015 pia wabunge walishangazwa na kitendo cha serikali kuendelea kuyahifadhi wakati maeneo mengi nchini wananchi wanahitaji chakula cha kununua kwa bei nafuu kutokana na bei hivi sasa kuwa juu.

Wakiwa katika ghala la akiba ya chakula (NRFA) mjini Shinyanga wabunge wa kamati hiyo wakiongozwa na mwenyekiti wao, Mary Nagu walishuhudia sehemu ya magunia ya mahindi yaliyomo ndani ya ghala hilo yakiwa na wadudu na baadhi yake yakitoa ungaunga kuashiria kuanza kushambuliwa na wadudu.

Wabunge walionesha mshangao kutoka na hali waliyojionea ambapo walishangazwa na kitendo cha serikali kuendelea kuhifadhi idadi kubwa ya chakula katika maghala yake huku maeneo mengi nchini ikiwemo wilaya 55 zikiwa na uhaba mkubwa wa chakula na wananchi wakiuziwa debe moja la mahindi kati ya shilingi 20,000 hadi 25,000.

“Mheshimiwa mwenyekiti hii hali inatushangaza, ni ajabu kuona chakula kipo cha kutosha lakini huko nje wananchi wanahangaika na hivi sasa wanauziwa mahindi kwa bei kubwa, lakini cha ajabu haya yaliyopo hapa tumejionea wenyewe yameanza kubunguliwa na wadudu, ipo hatari yataharibika,”

“Katika taarifa ya NRFA wamesema moja ya changamoto waliyonayo ni uhaba wa fedha, hiki ni kichekesho, kwa nini wasiuze mahindi waliyonayo zaidi ya tani 8,000 wakati hali ya soko ni nzuri, ni bora wayauze ili wapate fedha na wanunue mengine mapya,” alieleza Mohamedi Mgimwa mbunge wa Mufindi Kaskazini.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Uzini, Salum Rehani alisema iwapo serikali haitochukua hatua ya kuruhusu kuuzwa kwa mahindi hayo ipo hatari yakakosa soko baada ya wananchi kuanza kuvuna mavuno mapya hivi karibuni na kwamba wanachohitaji wananchi ni chakula cha bei nafuu na siyo cha bure.

Hata hivyo kwa upande wake Kaimu Ofisa mtendaji mkuu wa NRFA, Deusdedit Mpazi alikanusha madai ya mahindi kuwa katika hatari ya kuharibika kwa vile mara kwa mara hufanyika ukaguzi wa kuangalia iwapo hayajaingiliwa wadudu waharibifu.

“Mheshimiwa mwenyekiti si kweli kwamba mahindi haya yapo katika hatari ya kuharibika, hawa wadudu mnaowaona hapa hawana madhara makubwa, ni wadudu visumbufu tu, na hivi karibuni tunatarajia kuanza zoezi la kupulizia dawa, hivyo hayawezi kuharibika kama mnavyohofia,” alieleza Mpazi.

Akizungumzia suala la mahindi hayo kutopelekwa kwa wananchi ili yauzwe kwa bei nafuu, Naibu waziri wa Kilimo, mifugo na uvuvi, Ole Nasha alisema hofu ya serikali ni kuona mahindi hayo yatakapopelekwa kwa wananchi kuangukia kwenye mikono ya walanguzi na kuuzwa kwa bei ya juu.

“Hatukurupuki kusambaza mahindi haya ovyo, tuko makini ili kuhakikisha pale yatakapopelekwa kwa wananchi yanawafikia walengwa husika, lakini pia tunasubiri kipindi halisi cha mavuno ili tuweze kuona kiasi halisi cha mazao kitakachopatikana, na hivyo chakula hiki kitapelekwa kwenye maeneo yenye upungufu mkubwa,” alieleza waziri.

View attachment 486030

View attachment 486031
Akiba haiozi, yatauzwa ya CHAKULA itakapokuwa mbaya kuliko ilivyo sasa!! Big up JPM!!!!!
 
hayo mahindi muyaache kama yalivyo kwani nchi hii haina njaa na tulishawaonya wakuu wa wilaya/mikoa kutangaza maeneo yao kuwa na njaa,hayo magunia tumeweka kwa ajili ya maonyesho tu!na kiharibika tunayutupa tunanunua mengine na uzuri mahindi hayawezi ku expire,fanyeni kazi hakuna mahindi hapa!
 
Tukisema JPM anahujumiwa mnakataa....anyway kuna mbunge alisema kama ghala la taifa lina tani ngapi sijuhi, anajiuzulu ubunge!
 
hahahahahahahahahaha hizo propaganda tu ili seriakli ya wanyonge ichukiwe na wananchi,kwa nini wanataka cha bei nafuu,waache uvivu wapige kazi wavune cha kwao,hicho ni cha serikali
Mi sijui watu engine huko kichwani mmebeba nini.. Hivi serikali ni nani? Na hayo mahindi yamenunuliwa kwa kodi za wananchi, kwani wananchi wakiuziwa shida iko wapi? Acheni kujishushia hadhi namna hiyo
 
Back
Top Bottom