DOKEZO KERO Kilio cha NFRA kuchelewesha malipo ya pesa za mahindi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Wakulima wa mahindi katika kituo cha NFRA cha kununulia mahindi kilichopo kijiji cha Muze wilaya ya Sumbawanga vijijini hawajalipwa na NFRA pesa za mauzo ya mahindi kwa zaidi ya mwezi mmoja tofauti na ahadi waliyo pewa wakulima ya kulipwa pesa ndani ya siku 14 toka tarehe ya kupima mzigo.

Wananchi wanaomba ufafanuzi kutoka kwa serikali na wakala wa hifadhi ya chakula (NFRA) ni lini wakulima watalipwa pesa zao.

Wananchi wanahitaji kulipwa pesa zao kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa kilimo ambao unaanza siku chache zijazo.

Pia soma
 
Back
Top Bottom