PreGE2025 Kamati ya Hesabu za Serikali imekagua mradi wa Wakala wa Maji Vijijini RUWASA na kutaka ukamilishwe kwa wakati

PreGE2025 Kamati ya Hesabu za Serikali imekagua mradi wa Wakala wa Maji Vijijini RUWASA na kutaka ukamilishwe kwa wakati

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Just Pray

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,142
Reaction score
4,779
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imekagua mradi wa Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida tarehe 15 Machi, 2025.

Mradi huo hadi kukamilika kwake unatarajiwa kugharimu shilingi bilioni 13 na unatarajiwa kunufaisha vijiji 11 vilivyopo katika Halmashauri ya Manyoni.

Pia soma Pre GE2025 Miradi kuelekea Uchaguzi Mkuu: Mhandisi Kundo akagua mradi wa maji unaonufaisha zaidi ya wakazi 200,000 Chalinze

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa mradi huo katika kijiji cha Lusilile kilichopo Kata ya Kintinku, Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Joseph Kakunda amewaelekeza RUWASA kuhakikisha kuwa asilimia 2 za mradi zilizobaki zinakamilishwa ndani ya mwaka huu wa fedha.

Aidha amewaasa Wananchi waliokuwepo katika eneo wakati wa ukaguzi kuhakikisha kuwa wanauutunza mradi huo ili udumu kwa muda mrefu na uendelee kuwanufaisha.

"Mradi ukiharibika ni hasara kwa Wananchi, kwa hiyo ni jukumu lenu wananchi kuhakikisha mradi huu mnautunza ili nao uweze kuwasaidia," alisema.

Kakunda pia alielekeza Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya kuhakikisha wanasimamia ulinzi wa miundombinu ya mradi huo na kuwachukulia hatua kali wale wote watakaojaribu kuihujumu.
1742117180619.png
1742117195162.png
 
Back
Top Bottom