PreGE2025 Kamati ya bunge ya utawala, katiba na sheria yapongeza uwekezaji wa TASAF sekta ya elimu

PreGE2025 Kamati ya bunge ya utawala, katiba na sheria yapongeza uwekezaji wa TASAF sekta ya elimu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Just Pray

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,142
Reaction score
4,779
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imeeleza kuridhishwa na uwekezaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika miundombinu ya elimu katika mikoa ya Tanga na Pwani, ikisema miradi hiyo ni hitaji kubwa kwa wananchi wa maeneo husika.

Kamati hiyo imetoa pongezi hizo siku ya Ijumaa baada ya kutembelea na kukagua ujenzi wa vyumba sita vya madarasa, ofisi za walimu, pamoja na matundu 12 ya vyoo katika Shule ya Sekondari Magila (Muheza, Tanga) na Shule ya Sekondari Mwavi (Bagamoyo, Pwani), miradi inayotekelezwa na TASAF.

Pia soma Pre GE2025 Miradi kuelekea Uchaguzi Mkuu: Mhandisi Kundo akagua mradi wa maji unaonufaisha zaidi ya wakazi 200,000 Chalinze

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Dkt. Joseph Mhagama, amesema miradi hiyo inaonesha dhamira ya Serikali katika kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora na kutimiza ndoto zao.

"Tunaipongeza Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa usimamizi mzuri wa miradi iliyo chini yake. Tumeshuhudia miradi ya TASAF iliyotekelezwa kwa viwango vya juu, na hii ni kazi nzuri inayofanywa chini ya uongozi wa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan," amesema Dkt. Mhagama.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deus Sangu, amesema miradi ya TASAF inalenga kuboresha huduma za kijamii kwa wananchi kwa kujenga shule, madarasa, vituo vya afya, barabara, madaraja, na miundombinu ya maji.

Amesema kukosekana kwa shule katika Kijiji cha Mwavi, wilayani Bagamoyo, kuliwalazimu wanafunzi kutembea umbali mrefu, lakini ujenzi wa shule mpya kupitia TASAF utarahisisha mahudhurio na kuinua kiwango cha ufaulu.

Aidha, Sangu amesema Kamati hiyo imeridhishwa na thamani ya fedha katika utekelezaji wa miradi hiyo, ikibainisha kuwa baadhi ya majengo yaliyochakaa tangu mwaka 1932 sasa yamebadilishwa kwa uwekezaji wa kisasa wa TASAF, hali inayowapa wanafunzi mazingira bora ya kusoma.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria inaendelea na ziara yake siku ya Jumamosi katika Mkoa wa Kilimanjaro, ambapo itakagua miradi inayotekelezwa na TASAF na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
1742115411113.jpeg
1742115431351.jpeg
1742115451740.jpeg
 
Back
Top Bottom