Kamati ya Bunge na Uamuzi holela | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamati ya Bunge na Uamuzi holela

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nicas Mtei, Mar 29, 2012.

 1. Nicas Mtei

  Nicas Mtei JF-Expert Member

  #1
  Mar 29, 2012
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 11,569
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Nimesikia juzi kupitia vyombo vya habari kuwa kuna kamati ya bunge imeamuru jenereta inayotumiwa na mkurugenzi wa Tanesco Ndugu Muhando itolewe.

  Je kwa kumpora hyo jenereta ndo tutakuwa tumemaliza tatizo la mgao unaoendelea nchini?

  Yeye(Mhando) ndo alikuwa anatumia umeme mwingi sana kiasi kwamba hata mgao ukawa mkali?

  Je hlo jenereta walilochukua kwa Muhando limetoa msaada gani katka kukomesha mgao wa umeme?

  Kuna kitu gan kipo nyuma ya maamuzi hayo ya kamati? Je ni chuki binafsi au hila za kukomoana?

  Je matatizo ya mgao yameletwa na Muhando,Tanesco au serikali kwa ujumla?
  Kwa nini wasichukue jenereta anayotumia Ngeleja au ile anayotumia Malima?

  Karibuni tujadili kwa pamoja.
   
 2. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #2
  Mar 29, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Wachukuwe la Ikulu
   
 3. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #3
  Mar 29, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Haya maamuzi hata mimi yamenishangaza sana! Ingekuwa kila idara tunafanya maamuzi kama haya sijui tungekuwa wapi sasa hivi. Kama ile ni incentive ambayo ipo kwenye package yake basi hata hao watakaoenda kuizima ni lazima watageukia njiani kwa aibu. Tatizo hili la umeme ni kubwa kuliko Eng. Mhando mwenyewe. Hawa wanasiasa, huko Serikalini ndio wametufikisha hapa.

  Ndiyo haya sasa ninayosema


  Chanzo: Mwananchi, Washindwa kutekeleza agizo la kamati
   
 4. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #4
  Mar 29, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  akili zako haziko sawa sawa ilichokifanya kamati ni kumuonyesha huyo DG wa TANESCO kuwa watanzania hawana mbadala umeme unapokatika, hawana huduma ya jenereta kama yeye anavyopata tena kwa malipo ya watanzania , ni jambo la msingi Kamati imeamua ili Ndg mhando naye anunue mafuta ya jenereta lake na sio TANESCO wamlipie, kwako unaweza usione mantiki ya uamuzi huu, ila waulize wasomi waliobobea kwenye masuala ya corporate good gorvanance watakuambia.
   
 5. K

  Kintiku JF-Expert Member

  #5
  Mar 29, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 611
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 45
  NI maamuzi dhalili ya mchanganyiko na hasira, visasi, udini, woga na kupenda sifa. ZItto hajawahi kumpenda Mhando hilo liko wazi kabisa. Angekuwa siriasi angechukua Jenerata la Ngeleja au Malima. Kwa maaana nyingine hawa mawaziri ni maji marefu kwa Zitto (au ni washkaji zake Rostam.....connection).

  NI Kamuzu Banda ndo alikuwa anaweza enzi ziiile za Malawi..umeme ukikatika DG wa umeme umepoteza kazi, alifanya vile kwa vile uhakika wa umeme ulikuwa 100%.
   
 6. Escobar

  Escobar JF-Expert Member

  #6
  Mar 29, 2012
  Joined: Sep 16, 2011
  Messages: 576
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 60
  Mimi binafsi naunga mkono hoja ya kulichukua! Ukiangalia kwa haraka haraka unaweza kuona halina madhara lakini ukweli ni kwamba tukiruhusu mfumo huu ni hatari sana. Hebu tujaribu kuangalia gharama za uendeshaji wa majenereta haya yaani la mkurugenzi na vigogo wenzake wa shirika na mameneja wa mikoa na wilaya yanatugharimu shilingi ngapi kwa mwaka? Ukumbuke haya yote yanagharamiwa na kodi zetu za tozo la huduma. Hivi ni kweli mtndaji wa kata anayehudumia wananchi kilasiku bila umeme hastahili kuwa na jenereta? Je ni vituo vingapi vya afya havina umeme? Sasa inakuwaje mtu mmoja tu kwa sababu ya cheo chake apewe mshara mkubwa, gari na mafuta bure, dereva, nyumba, na jenereta bure. Sasa mshahara anapewa wa nini? Liondolewe haraka anunue lake ili ajue na bei za mafuta
   
 7. Nicas Mtei

  Nicas Mtei JF-Expert Member

  #7
  Mar 29, 2012
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 11,569
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Haohao wasomi ndo wamelfksha taifa katika mgao wa umeme na hali ngumu tulionayo.

  Kumpora hlo jenereta Eng. Mhando kumepunguza vp tatizo la mgao? Je deni wanalodaiwa lmepungua walivyoamuru hlo jenereta lichukuliwe?

  Ni wakurugenzi wangapi wa mashirika ambayo yana matatzo wanatumia mali za umma? Je ni Mhando pekee? Nini kmefanyika kwa hao wengne?

  Je Ngeleja hana jenereta? Na Malima je? Zmetolewa?
   
 8. Nicas Mtei

  Nicas Mtei JF-Expert Member

  #8
  Mar 29, 2012
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 11,569
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Swali langu ni je ni impact gan zatajtokeza baada ya kumpora hlo jenereta? Mgao utapungua? okay wamelchukua, amenunua la kwake, what is next? Bdo kwake umeme utakuwepo. Je atakuwa na wazo la kudeal na mgao?
   
 9. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #9
  Mar 29, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Bora wamelichukua ili tulingane si anapata mshahara? na aingie gharama za kupata umeme kwa jasho lake na si kodi yangu na la Ngeleja na Malima pia naomba wachukue ili kama ni machungu tuyapate wote jamani.
   
 10. Jiwe Linaloishi

  Jiwe Linaloishi JF-Expert Member

  #10
  Mar 29, 2012
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 3,736
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Kama wameanza kwa Mhando na wengine wafuatie isiwe kwa mmoja tu na huu utaratibu wa kuwawekea viongozi majenereta ufe ikiwa ni pamoja na kuondoa magari ya uma yanayohudumia wake zao kwa shughuli binafsi, kuna mianya mingi sana kodi zetu zinavuja ndio maana hatuwezi kupiga hatua kama hatutaithibiti.
   
 11. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #11
  Mar 29, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
   
 12. kupelwa

  kupelwa JF-Expert Member

  #12
  Mar 29, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 874
  Likes Received: 139
  Trophy Points: 60


  Si vyema mtu mzalendo kuwa mbinafisi is na kutetea hoja ya ufisadi.katika package ya motisha ya tanesco hakuna mahala ambapo wakurungezi wakuu wanapashwa kulipiwa majenereta wala mafuta ya kuyaendesha.kama inafanyika hivyo ni kinyume.Kama ni kinyume kwanini isirekebishwe?kamati ya bunge kuamuru hivyo ni namna ya kurekebisha maamuzi yasiyo sahihi.Pia ikumbukwe kuwa tanesco inapata hasara ya mapatao ya ke kwa tshs 64 bil kwa mwaka .Je kama inapata hasara inatakiwa kupunguza ghrama za uendeshaji.Hii ni pamoja na kuruhusu wakurungezi wakuu kulipiwa majenereta na mafuta yeke.jamani lazima tukubari utawala bora.
   
 13. HISIA KALI

  HISIA KALI JF-Expert Member

  #13
  Mar 29, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 694
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Kwani hiyo kamati ilitoa sababu zipi?

   
 14. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #14
  Mar 29, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  u mean akiwa na umeme hatakua na wazo la kudili na mgao,hata kama atanunua la kwake?akoding to ur last sentensi!
   
 15. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #15
  Mar 29, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  anatumia mafuta ya raia,aone adha ya kuwa bila umeme,arudishe gen la walala hoi
   
 16. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #16
  Mar 29, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Kama ameshindwa kazi AONDOLEWE!! Mnachukua Generator then what?
   
 17. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #17
  Mar 29, 2012
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ni mwanzo mzuri wanachotakiwa sasa kufanya ni kupitisha sheria inayokataza serikali kulipia wafanyakzi wake matibabu kwenye hospitali binafsi na hata nje ya nchi.
  Baada ya hapo pia iwazuie watendaji wake wakuu kusomesha watoto wao kwa gharama za serikali kwenye shule binafsi ama nje ya nchi. Na kuwalazimisha kujiuzuru mawaziri ambao hawatumie huduma zinazotolewa na serikali (shule-hata kama watalipa wao, matibabu ya familia zao-hata kama wanajilipia)
  Tukifanya hivyo nina uhakika huduma za jamii zitaboreshwa haraka
   
 18. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #18
  Mar 30, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  ni jazba tu
   
 19. S

  Sam Upendo Member

  #19
  Mar 30, 2012
  Joined: Jan 22, 2012
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kumnyanganya Genereta ni sawa kabisa ili aone adha yas kukosa umeme. Unaelewa ni kwa nini Pilot wa ndege za kiraia haruhusiwi kuwa na mwavuli ya kuokoa maisha (Parachute?). Ili atambue kwamba asipokuwa makini yeye pamoja na abiria wake wote kwa pamoja wataangamia.
   
 20. p

  pat john JF-Expert Member

  #20
  Mar 30, 2012
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 245
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama ni Good Govenance kwa nini wasianzie kwa watunga sera? Eng. Mhando ni Agent tu wa kutekeleza sera zao.
   
Loading...