Kamati: Mwezi haujaandama

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,219
103,809
Kamati ya kuthibitisha kuandama kwa mwezi Zanzibar ambayo ipo chini ya Ofisi ya Mufti wa Zanzibar, inawajuulisha kuwa, leo Jumamosi, tarehe 24, Juni, 2017 sawa na mwezi 29 Ramadhani, mwezi HAUKUANDAMA. Hivyo, waumini wa kiislamu watakamilisha siku 30 za mwezi wa Ramadhani kesho na Sikukuu ya Eid El Fitri itakuwa Jumatatu tarehe 26, Juni, 2017, na jumanne tarehe 27 Juni 2017 (Eid pili).

Anaripoti Kamanda OKW
 
Hahaaa, bakwata na mwezi wao na mjiandae kuwalipa hao mnaowadanganya na kugawana madhambi ya kufunga ck ya eid
 
Kuna Nchi nyingi sana saa hizi wapo Swala na bata la Eid litaendelea punde.
 
Fungeni mkiuona, fungueni mkiuona.

Sio fungeni mkiuona, fungueni mkithibitishiwa kuonekana.
Changamoto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…