Thanks Regia, mimi naamini hakuna kamati kuu ya chama chochote iliyo makini kama ya CDM hivyo hata maamuzi yao hayana walakini. Kazi ni moja sasa.Mwl Joseph Mwandu Kashindye kuipeperusha bendera ya CHADEMA Igunga.Kamati Kuu imempitisha.Kila la heri Kamanda.
Mwl Joseph Mwandu Kashindye kuipeperusha bendera ya CHADEMA Igunga.Kamati Kuu imempitisha.Kila la heri Kamanda.
Dah,ni balaa kama hali yenyewe ndo iko hivi kweli,....Mheshimiwa Regia nakubali CDM mko serious lakini jambo dogo tu huwa tunamalizwa na CCM, mimi ni mzaliwa wa igunga na nimeishi igunga muda mrefu sana kwahiyo nafuatilia kwa karibu mchakato wa igunga tangu kujiuzulu kwa rostam, nawajua wafuasi wa CCM na CDM. weakness ya CDM Igunga hakuna uongozi imara wa CDM, nasema hivyo kwasababu mwenyekiti wa wilaya Majimoto, Kashindye na Pili mnene (amekuwa mwenyekiti wa wanawake wa chadema wilaya tangu kujiuzulu kwa rostam kabla ya hapo alikuwa ccm) walikuwa wakala wa rostam uchaguzi wa 2010.
Majimoto alijitoa kugombea ubunge kwa kupewa fungu na rostam, Kashindye alteuliwa kuhamasisha kura za uraisi kwa jakaya kwa kauli mbiu aliyokuwa anawambia wanaigunga vijijini kuwa DR. SLAA ni fisadi wa mapenzi ili wanawake wasimpigie kura. Pili Mnene amejengewa nyumba na rostam na mpaka sasa anasomesha mtoto wake chuo kikuu. Mheshimiwa diwani wetu wa chadema kwenye vikao vya council anapokea posho anayotoa RA ili kuweza vikao vya madiwani vipitishe matakwa yake kwa remote wakati yeye anakula raha jijini.
Sasa kabla ya kupitisha mgombea wenu kesho mheshimiwa kashindye muhakikishe mmesafisha jambo hilo kwani walimu wote wanajuwa kuwa alikuwa kibaraka wa rostam kufanya kampeni za ccm 2010 sasa wapiga kura wenu watakuwa na imani nae vipi kwasababu wanamtambua kama CCM na kwataarifa nilizo nazo hadi sasa wamekorofishana na DC igunga kwa kuwa wanajuwa kilichofanyika mwaka jana. Na siku chache baada ya kujiuzulu RA, Bashe alivyokuja igunga alimtumia Kashindye kuwapelekea wenyeviti wa kata salamu kutoka kwa rostam na kuwajulisha kuwa yupo nao pamoja fungu alilopewa alimficha boss wake DC na badala yake akatumia gari la ukaguzi na mafuta ya serikali bila kumgawia boss wake fungu.
TUPO NJIA PANDA wanaigunga kwa maana kwamba tutapata bora mbunge kwa maslahi yake mbunge na kuongeza fungu la posho kwenye chama au tunapata mbunge ili kuweza kuwatumikia wanaigunga? NITOE NJIA PANDA KESHO
Nyie mnaolazimisha CDM iungane na CUF kwanini CUF wasiungane na CCM halafu mtuambie ni wapi wapinzani waliungana wakashinda,
kama ni kugawana kura hata CCM itagawana na CUF maana CDM wanaenda bila kuwa na kura hata moja, ngoja niwape mahesabu yatavyokuwa,
Uchaguzi uliopita CCM walipa kura 35,000 safari hii watapata nusu ya hizo nusu iliyobaki itakwenda Chadema yaani 17,500.
CUF walipata kura 11,000 safari hii hata nusu yake hawapati basi tuwape nusu 5,500 na nusu iliyobaki itakwenda Chadema yaani 5,500.
Final results
Chadema kura 17,500 + 5,500 = 23,000.
CCM kura 35,000/2 = 17,500.
CUF kura 11,000/2 = 5,500.
chadema wanayo nafasi ya kushinda ila wako mtegoni mpaka sasa, CUF msijisumbue sana bora muwaunge mkono ccm kwani Dr. Kafumu ameyavulia nguo maji na hana budi kuyaoga mpaka ameacha budget ya wizara yake haijapita yupo kwenye mchakato. DANGER, mzimu wa rostam unasumbua igunga bado.
..ndivyo inavoelekea kuwa,ktk mazingira haya ya utawala wa ccm, wapo watu wa kuwaamini but si watu wa caribre ya Kashindye, ccm wanaweza kutumia fedha kununua madiwani zaidi ya sita sembuse mtu mmoja tena mwajiriwa wa serikali wanayoiongoza..!lini ccm wameanza siasa za ustaarabu..? wanayo karata moja tu karata waliyobaki nayo sasa KUNUNUA WAGOMBEA NA KUWAFANYA MAMLUKI..!hawana uwezo wa kushinda uchaguzi kwa hoja! hata wakeshe majukwaani!
Hivi mnawajua waratibu kata wa vijijini nyie? na jinsi wanavyopata hizo nafasi..? kwa anejua Bw. Kasindye is not a person to trust as a material candidate! labda CHADEMA wakiamua kusindikiza uchaguzi wa lgunga
Mara nyingi retreat is not Ignorance na sio sign ya weakness,...Hata kwenye movies tunaona ili umshinde adui lazima sometimes u-salende kwenye kambi yakethen from ndani ndo utajua jinsi ya kupigana nao.Chadema haina nguvu Igunga,sikatai kwamba wasisimamishe mgombea maana wakisimamisha ndo itakua mwanzo wa chadema kuanza kufahamika vyema huko.Lakini ukweli ni kwamba chadema kushinda Igunga kwenye huu uchaguzi mdogo ni sawa na ngamia kupita kwenye tundu la sindano ila kushiriki kwao Igunga ni maandalizimazuri ya 2015.Kama ni kweli chadema inakubalika Igunga kama alivosema sis.Regia na "mamia" waliwapokeabasi usingekawia kuona picha hapa,....trust me.Anyway,i wish them the best katika maandalizi ya 2015 sio saivi,.....i still stand on my bet kwamba chadema will rank number 3 kwenye huo uchaguzinyuma ya CCM na CUF,......Lets be realistic kidogo
Speaker
Comments zako ni interesting. Namkumbuka Maggid Mjengwa. Naye alitabiri kuwa Chadema ingeibuka ya tatu kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka jana based on historical evidence...za nguvu ya kafu na ushindi wao wa huko nyuma. You know what happened.
Utabiri wako, kama wa Maggid, unaacha some important variables in the model.
Mwl Joseph Mwandu Kashindye kuipeperusha bendera ya CHADEMA Igunga.Kamati Kuu imempitisha.Kila la heri Kamanda.
@speaker
vyama vingi vinapoteza ushindi katika chaguzi ndogo kwasababu ya mbinu na kutokuwa na mamlaka juu ya tume za uchaguzi, nadhani kuna vyama vyenye uwezo ata wa kumshinikiza muhusika wa daftari la wapiga kura kuondoa au kuongeza majina ya wapigakura(ghost voters)
Ahsante kwa taarifa mpiganaji wetu.zingatieni kua magamba ni wazuri sn katika rafu na rushwa katika uchaguzi
na ni vema mkumbuke kua cuf hawaipendi cdm na wapo tayari kuwasaport ilimradi cdm ikose ushindi.
Hivyo nashauri makamanda muwe makini na mumtumie sn huyo diwani wetu wa hapo igunga.
Mkuu,
hawa watu wanaharibu kwa kukosa maarifa.
haiwezekani unajua kabisa swali flani formula yake ni xxxx alafu unaingia
kwenye mtihani bila kuifanyia kazi hiyo formula,.....
ukifeli una lalamika kuonewa na mwalimu.
Kwanini CUF wasiungane na CCM kumsimamisha mgombea wao mmoja? au wewe hujui kuwa CUF na CCM lao ni moja?